Video: DCEA Yakamata Mirungi na Bangi Zikisafirishwa kwa Mabasi na Magari

Global Publishers
September 29, 2026
6 views
0 Comments

DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata watuhumiwa waliodaiwa kutumia vyombo vya usafiri kusafirisha dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa DCEA, watuhumiwa watatu walikamatwa wakisafirisha bunda 238 za mirungi zenye uzito wa kilogramu 125.33, kwa kutumia basi la kampuni ya RATCO lenye namba za usajili T 443 EMG, lililokuwa likifanya safari kati ya Tanga na Dar es Salaam.

Katika tukio jingine, DCEA imekamata kilogramu 21.95 za bangi katika Wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

Bangi hiyo ilidaiwa kuwa inasafirishwa kwa gari aina ya Tata lenye namba za usajili T 381 DW, lililokuwa likifanya safari kati ya Uyui mkoani Tabora na Kahama mkoani Shinyanga.

Katika tukio hilo, jumla ya watuhumiwa watano walikamatwa na wanatarajiwa kufikishwa katika hatua za kisheria kwa mujibu wa taratibu.

DCEA imeendelea kutoa tahadhari kuhusu matumizi ya vyombo vya usafiri katika kusafirisha dawa za kulevya, huku ikiimarisha operesheni za kudhibiti usafirishaji na biashara ya dawa hizo nchini.