Global Publishers
September 28, 2026
0 views
0 Comments
Doha, Qatar – Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametembelea Maktaba ya Taifa ya Qatar, maarufu kama Qatar National Library, jijini Doha.
Dkt. Mwigulu amefanya ziara hiyo Jumapili, Septemba 27, 2026, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya ziara yake ya kikazi nchini Qatar.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alipokelewa na Rais wa Maktaba ya Taifa ya Qatar, Dkt. Mohamed Bin Ahmed Bin Twar Al Kuwari, ambapo alipata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo.
Miongoni mwa maeneo aliyopata taarifa ni namna maktaba hiyo inavyoshiriki katika kuhifadhi, kukuza na kuwezesha upatikanaji wa maarifa, pamoja na kulinda na kuendeleza urithi wa kiutamaduni.
Ziara hiyo imefanyika wakati Dkt. Mwigulu akiendelea na ratiba ya shughuli mbalimbali nchini Qatar, ambako yupo kwa ziara ya kikazi.





