Kesi ya Uhaini ya Lissu Yaahirishwa Hadi Septemba 28, 2026

Global Publishers
September 25, 2026
18 views
0 Comments

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa mchana huu wa Septemba 25, 2026 hadi jumatatu Septemba 28, 2026, ambapo itakuja kuendelea katika usikilizaji wa uwasilishaji wa hoja za mwisho (Final Submission) kutoka kwa mshtakiwa.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dunstan Ndunguru ambaye anaongoza Jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo.

Kabla ya majaji kuamua kesi kuendelea Jumatatu, Lissu aliomba muda wa mapumziko kama ilivyo katika siku zingine baada ya kufika saa saba kamili, ndipo majaji wakaja na uamuzi huo.

Lissu alikuwa akiendelea kuwasilisha hoja zake tisa za mwisho, ambapo hadi uamuzi huo unapotolewa alikuwa amefika katika hoja ya saba inayosema “kama Jamhuri ya Muungano ilitishika” kwa maneno ambayo yametumika kumshtaki Lissu.