Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa agizo hilo wakati akifanya ziara ya kutembelea mitaa mbalimbali ya kariakoo wilaya ya Ilala na kutoa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kwa wafanyabiashara wadogo kariakoo kuacha kufanya biashara barabarani na mbele ya maduka ya watu badala yake wao pia wafanye biashara zao kwenye vyumba vya maduka
Akizungumza leo Septemba 24, 2026 RC Chalamila amesema baada ya kufanya ziara amebaini uwepo wa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kuweka meza zao juu ya mitaro ya maji, mbele ya maduka ya watu wengine pamoja na kuziba barabara hivyo amewataka wafanyabiashara hao wadogo kuhamia kwenye maduka ndani ya muda huo wa mwezi mmoja
Aidha RC Chalamila amemtaka RPC ilala kumkamata mmiliki wa jengo eneo la Kariakoo aliefanya utiririshaji wa maji taka, jambo ambalo ni kinyume na sheria huku akimuelekeza mkuu wa Wilaya ya Ilala kuendelea na oparesheni ya dhidi ya wanaofanya biashara juu ya mitaro ya maji
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema wilaya hiyo imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kulifungua Soko la kariakoo na kuhakikisha linapitika huku akieleza baadhi ya changamoto zilizopo kwenye eneo hilo ikiwemo wafanyabiashara kuziba mitaro, kuingiza majiko kupika kariakoo na kushusha mizigo kuziba njia
Vilevile Mwenyekiti wa wafanhabiashara wadogp maarufu kama machinga eneo la kariakoo Livingston Lusinde kwa niaba ya wafanyabiashara wadogo amesema wafanyabiashara wadogo wapo tayari kuondoka kariakoo na kwenda kufanya biashara eneo walilotengewa la Jangwani na kuiomba Serikali kueleza mchakato wa ujenzi wa soko hilo huku Mwenhekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara kariakoo Severin Mushi akiipongeza Serikali kwa kuendelea kuiboresha kariakoo ikiwemo kuwaondoa wamachinga mbele ya maduka.




