Video: Lissu Kufungwa Miaka Minne Gerezani Mwanasheria Afunguka Mazito Global Radio

Global Publishers
November 6, 2026
18 views
0 Comments

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uchochezi.

Hukumu hiyo imetolewa leo, Ijumaa, Novemba 6, 2026, na jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, huku majaji wengine wakiwa James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.