Kaka wa Lissu, Wakili Alute Mughwai Lissu Afariki Dunia

Global Publishers
November 1, 2026
12 views
0 Comments

Wakili Alute Mughwai Lissu, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 1, 2026.

Taarifa za kifo cha Wakili Alute zimethibitishwa na dada yake, Rose Masesa.

Akizungumzia chanzo cha kifo hicho, Rose amesema kwa sasa hawezi kutoa maelezo zaidi kuhusu mazingira ya kifo hicho, huku akithibitisha kuwa msiba upo jijini Arusha.

“Ni taarifa za kweli, msiba upo Arusha na mimi naelekea huko,” amesema Rose kwa ufupi.

Hadi sasa, familia haijatoa taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo hicho, huku ndugu, jamaa na marafiki wakitarajiwa kuungana na familia katika kipindi hiki cha majo