MAGEREZA WANAWAKE YAIBOMOA NGOME JWTZ 3 – 0 YATWAA UBINGWA BAMMATA 2026

Na. S’sgt Mawazo Mtondo – MWANZA

Timu ya mpira wa wavu wanawake ya Jeshi la Magereza imehitimisha kwa kishindo ushiriki wake katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3–0 dhidi ya timu ngumu ya Ngome ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mchezo huo, uliokuwa wa ushindani mkubwa ukihusisha mbinu, mipango na umakini wa hali ya juu kutoka kwa pande zote mbili, umefanyika leo Oktoba 1, 2026 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ushindi huo umeiwezesha timu ya wanawake ya Kanda ya Magereza kutwaa ubingwa wa mpira wa wavu wanawake BAMMATA 2026, baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo yake yote.

Katika michezo yake ya awali timu hiyo, iliifunga Polisi wanawake kwa seti 3–0, kabla ya kuendeleza kasi hiyo kwa kuichapa timu ya SMZ kwa seti 3–0. Katika mchezo mwingine, Magereza iliibuka na ushindi wa seti 3–1 dhidi ya JKT Tanzania.

Matokeo hayo yameifanya timu ya wanawake ya Kanda ya Magereza kumaliza mashindano ikiwa mabingwa wa mpira wa wavu wanawake kwa kutopoteza mchezo hata mmoja katika mashindano ya BAMMATA 2026, huku ikionesha uwezo mkubwa katika mashindano hayo.

‎

 

Fursa za Ajira Saudi Arabia na UAE Zatangazwa kwa Watanzania

Global Publishers
October 1, 2026
12 views
0 Comments

BRAVO JOB CENTER AGENCY LIMITED inatangaza fursa za ajira kwa waombaji wenye sifa mbalimbali za kufanya kazi Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE).

NAFASI ZA MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA – SAUDI ARABIA

Waombaji wanahitajika kuwa na:

✅ Uzoefu wa kuendesha magari makubwa wa angalau miaka 2
✅ Leseni halali ya udereva
✅ Rekodi nzuri ya udereva
✅ Umri wa miaka 35 au zaidi
✅ Uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu/shift ndefu

💰 MASLAHI YA MADEREVA

✅ Mshahara unaoshindana na viwango vya soko
Usafiri wa kwenda kazini kila siku
✅ Posho za safari
✅ Bima ya afya inayotolewa na kampuni
✅ Tiketi ya ndege

🇦🇪 FURSA ZA AJIRA – UAE

BRAVO JOB CENTER AGENCY LIMITED, kwa kushirikiana na SAEY BUSINESS – Misri, inatangaza fursa za ajira nchini UAE.

🎁 MASLAHI YA MFANYAKAZI

✅ Mshahara na posho kulingana na mkataba wa mwajiri
✅ Malazi hutolewa
✅ Huduma za matibabu bure
✅ Usafiri hutolewa kila siku kwenda kazini
✅ Chakula/kitchen facility hutolewa
✅ Saa 8 za kazi kwa siku, siku 6 kwa wiki
✅ Siku 1 ya mapumziko kwa wiki
✅ Overtime hulipwa
✅ Likizo ya siku 30 zenye malipo baada ya kutimiza miezi 12
✅ Tiketi ya kurudi UAE–Tanzania baada ya kukamilika kwa mkataba
✅ Mkataba wa awali wa miaka 2, unaoweza kuongezwa kwa makubaliano
✅ Bima na fidia kwa mujibu wa sheria za nchi ya ajira

📋 UTARATIBU WA AJIRA

Waombaji watachaguliwa kulingana na mahitaji ya mwajiri na nafasi husika. Waombaji watakaokidhi vigezo watawasilishwa kwa mwajiri kwa ajili ya hatua zinazofuata za mchakato wa ajira.

📞 MAWASILIANO NA MAOMBI

BRAVO JOB CENTER AGENCY LIMITED

📞 0714 326005
📞 0781 634642
📞 0678 805452

📍 OFISI:
Rissa Tower, Lumumba na Amani, Dar es Salaam.

📢 WOTE MNKARIBISHWA!
🤝 Mwambie na mwenzako kuhusu fursa hii

Mchezo Mpya Wafika Meridianbet Ingia Kwenye Jungle Temple

Global Publishers
October 1, 2026
6 views
0 Comments

Msitu wa kale umefungua milango yake, na safari ya kutafuta hazina sasa imehamia Meridianbet. Wapenzi wa kasino mtandaoni wamepata burudani mpya kupitia Jungle Temple, mchezo wa Expanse unaopatikana rasmi Meridianbet. Hapa si safari ya kawaida, kwani kila mzunguko unakupeleka hatua moja zaidi ndani ya dunia iliyojaa siri, mahekalu yaliyofichika na hazina zinazokusubiri kugundua.

Jungle Temple imejengwa kwa mandhari inayochanganya historia na teknolojia ya kisasa. Unapoanza mchezo, unaingia moja kwa moja kwenye msitu wa kale wenye alama za ajabu na maeneo yaliyofichwa. Kila raundi inaleta tukio jipya, huku safari ikiendelea kuwa ya kuvutia kadri unavyofungua vipengele mbalimbali vya mchezo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Msisimko mkubwa unakuja kupitia vipengele vya bonasi vilivyowekwa ndani ya Jungle Temple. Kila mzunguko unaweza kuwa mwanzo wa tukio jipya, na kila hatua inakupa sababu nyingine ya kuendelea kuchunguza. Hii ndiyo ladha inayowafanya mashabiki wa sloti kufurahia safari huku wakisubiri kuona kitakachojitokeza kwenye raundi inayofuata.

Meridianbet imeendelea kuongeza michezo mipya kwenye kasino yake ili kuwapa wachezaji burudani yenye mandhari tofauti. Jungle Temple imewasili ikiwa na simulizi lake la kipekee la msitu, hekalu na hazina. Ni nyongeza inayokuja na mazingira mapya kwa yeyote anayependa kujaribu mchezo wenye ladha tofauti.

Safari ya hazina imeanza Meridianbet. Ingia kwenye Jungle Temple leo, chunguza siri zilizofichika na ufurahie kila mzunguko wa safari hii ya kipekee. Msitu una mengi ya kuficha, na kila raundi inaweza kufungua ukurasa mpya wa burudani yako. Jungle Temple inakusubiri, ingia Meridianbet na anza safari.

 

 

UEFA Nations League: Mechi za Moto Kutikisa Oktoba Denmark vs Ureno, Ugiriki vs Uholanzi

Mwezi Oktoba unaanza vyema kabisa ambapo tutashuhudia mitanange mbalimbali ya mechi za Kimataifa kuanzia Afrika Mpaka kule Ulaya. Pointi 3 zinagombaniwa haswa. Je nani kuondoka na ushindi?

Mapema kabisa Denmark atamenyana dhidi ya Ureno ya Cristiano Ronaldo ambao kwenye mechi mbili wameshinda zote hivyo wameanza vyema kabisa kwenye michuano hii.

Denmark inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na faida ya kucheza nyumbani, hivyo itahitaji kutumia nguvu na kasi ya wachezaji wake wa pembeni kuiwekea Ureno presha kwani wana wachezaji wengi wazuri wakiwemo Højlund na wengine.

Ureno ina ubora mkubwa katika eneo la kiungo kupitia Bruno Fernandes, Vitinha na Joao Felix, pamoja na uzoefu wa Cristiano Ronaldo katika safu ya ushambuliaji hivyo inawafanya kuwapa faidi zaidi.

Hata hivyo, kucheza ugenini dhidi ya Denmark kutahitaji umakini mkubwa katika ulinzi na matumizi mazuri ya nafasi. Kwa ujumla, tunatarajia mchezo wenye ushindani mkubwa ambao unaweza kuamuliwa na ubora wa timu katika dakika za mwisho. Nani kushinda leo?.

Mechi hizi za UEFA Nations League unaweza kuzipata pale Meridianbet, na zile za kufuzu Afcon pia.

Kivumbi kingine kipo mechi ya Ugiriki dhidi ya Uholanzi ambapo hawa wote wapo kwenye Kundi A na kila timu leo hii inahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huu ili iweze kujiweka kwenye nafasi nzuri kundini.

Ugiriki ni timu ambayo inaweza kuingia mchezoni kinidhamu zaidi, na kufanya mashambulizi ya kushtukiza pale inapopata nafasi. Ufanisi wao mbele ya lango utakuwa muhimu, kwa sababu huenda wasipate nafasi nyingi za kufunga kutokana na mpinzani ambaye wanaenda kukutana naye.

Kwa upande wa Uholanzi wao chini ya kocha mkuu Xavi Hernandez,  nguvu yao kubwa iko kwenye kasi ya kushambulia, ubunifu wa viungo na uwezo wa kutumia nafasi kwenye maeneo ya pembeni. Wanatarajiwa kujaribu kuutawala mchezo mapema na kuilazimisha Ugiriki kujilinda kwa muda mrefu.

Hata hivyo, wakishindwa kutumia nafasi zao, Ugiriki inaweza kuwaadhibu kupitia counter-attacks. Hivyo, mchezo huu unaweza kuamuliwa zaidi na umakini wa ulinzi na ubora wa kumalizia nafasi.

Tofauti yao mpaka sasa ni 2 pekee huku takwimu zikionesha kuwa mechi mbili mara ya mwisho kukutana Uholanzi ameondoka na ushindi meci zote mbili, hivyo huenda hii ndio mechi ya kisasi kwa Ugiriki.

Halikadhalika Ujerumani atakuwa nyumbani kumenyana vikali dhidi ya Serbia ambapo kwenye kundi lao wao ndio wapo nafasi ya mwisho huku tofauti yao ikiwa ni pointi 1.

Timu hiyo ya Ujerumani chini ya Klopp inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika kipindi cha mpito. Jürgen Klopp amechukua timu hiyo baada ya Kombe la Dunia la 2026 na anajaribu kujenga timu yenye nguvu zaidi kuelekea Euro 2028. Katika michezo yake ya mwanzo, Klopp amekuwa akitafuta namna bora ya kuchanganya wachezaji wenye uzoefu na vipaji vipya.

Kwa upande wa Serbia ni timu yenye nguvu kimwili na inaweza kuwa hatari kupitia mashambulizi ya kushtukiza. Wanahitaji kuwa na nidhamu katika ulinzi na kutumia vizuri mipira ya mwisho wanapopata nafasi. Kiungo kitakuwa eneo muhimu kwa sababu timu itakayolitawala eneo hilo inaweza kupata udhibiti mkubwa wa mchezo.

Kila timu inahitaji kupata ushindi siku ya leo, kwani pointi 3 ni muhimu sana kwa pande zote mbili. Je nani kushinda?.

Lakini pia kwa kumalizia Meridianbet wanakwambia kuwa unaweza ukaangalia takwimu, msimamo na hali za wachezaji mbalimbali kupitia App yao. Ingia na utazame sasa.

Miili ya Chivayo, Mkewe Yatolewa Kwenye Mabaki ya Ndege

Global Publishers
October 1, 2026
0 views
0 Comments

Miili ya mfanyabiashara maarufu nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo, mkewe Lucy Muteke na watu wengine watatu waliofariki katika ajali ya ndege, imeondolewa katika eneo la ajali baada ya zoezi la uokoaji na ukusanyaji wa mabaki kuchukua takribani saa 18.

Operesheni hiyo ya kurejesha miili ilikuwa imefanyika leo saa 4:00 asubuhi, huku maafisa wa uchunguzi wa kisayansi wa uhalifu pamoja na wahudumu wa kampuni ya mazishi ya Doves Funeral Services wakikusanya mabaki ya miili katika eneo la ajali.

Mabaki hayo yaliwekwa kwenye mifuko maalumu na kisha kubebwa kwa machela hadi kwenye magari yaliyokuwa yanasubiri eneo hilo.

Eneo la ajali lilikuwa limejaa mabaki ya ndege yaliyoharibika vibaya, huku harufu ya vitu vilivyoungua ikitanda katika eneo hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda, hali ilikuwa ngumu kiasi kwamba baadhi ya watu waliofika mapema walipata ugumu kuwatambua wahanga.

Mfanyakazi wa Kudenga Farm, David Yoramu, amesema waokoaji walikumbana na hali mbaya wakati wakijaribu kuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye eneo la ajali.

Amesema walilazimika kutafuta gari maalumu la kubeba maji (water bowser) ili kusaidia kuzima moto kutokana na ukubwa wa tukio hilo.

Baadhi ya ndugu wa Chivayo, akiwemo kaka yake Joachim, walifika eneo la ajali wakati zoezi la ukusanyaji wa mabaki ya miili likiendelea.

Miili hiyo inatarajiwa kufanyiwa taratibu rasmi za utambuzi pamoja na uchunguzi wa kitabibu (post-mortem) kabla ya kukabidhiwa kwa familia kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Ajali hiyo ilisababisha vifo vya Wicknell Chivayo, Lucy Muteke, marubani wawili na mlinzi, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka muda mfupi baada ya kuondoka katika makazi yao ya kijijini Gandami.

DKT. MWIGULU: TANZANIA NA QATAR BADO TUNA FURSA NYINGI ZA KIUCHUMI

_Apigia chapuo utekelezaji wa DIRA 2050_

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema bado kuna fursa nyingi za ushirikiano wa kiuchumi baina ya Taifa la Qatar na Tanzania ambazo zikitumiwa vizuri zitawanufaisha raia wa nchi zote mbili.

 

“Bado tuna fursa nyingi ambazo tunaweza tukanufaika nazo kama tutatekeleza baadhi ya shughuli za kiuzalishaji. Tanzania kama lango la Afrika Mashariki, Kusini na Kati na Qatar kama lango la Mashariki ya Kati na Umoja wa Nchi za Ghuba tulikubaliana kuwa tukichangamkia fursa zote zinazojitokeza, tutaongeza ushiriki wa wananchi wa nchi zote mbili,” alisema.

 

Alikuwa akizungumza na Rais na Mtendaji Mkuu wa Power International Holding (PIH), Bw. Ramez Al-Khayyat na baadhi ya viongozi wakuu wa taasisi hiyo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Lusail, jijini Doha.

 

Waziri Mkuu alimshukuru Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH kwa kuonesha nia ya dhati ya kuwekeza katika sekta ambazo DIRA 2050 imeyaainisha kama maeneo ya kipaumbele.

 

“Tunashukuru kwamba hii kampuni imeonesha nia ya kuwekeza kwenye maeneo yaliyotajwa katika DIRA 2050 ambayo na sisi tumeyawekea kipaumbele. Wameonesha nia ya kushiriki DIRA yetu kupitia utekelezaji wa fursa zilizopo. Tumekubaliana kwamba mawaziri waliopo wakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Kapinga wafuatilie kwa karibu ili utekelezaji uanze mara moja.”

 

Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH, Bw. Ramez Al-Khayyat alimweleza Waziri Mkuu kwamba Power International Holding ni kampuni kubwa ya kimataifa inayomilikiwa na watu binafsi ambayo inaendesha kampuni tanzu 400 zenye wafanyakazi 65,000 katika nchi 26.

 

Kati ya nchi 26, za Afrika ni Misri, Libya, Morocco, Algeria, Mauritania na Rwanda. Alisema wameshaingia makubaliano na Ethiopia (ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 400).

 

“Utendaji kazi wa taasisi yetu umegawanyika katika makundi makubwa saba ya kibiashara yanayoendeshwa kimataifa na yenye kampuni tanzu 400 na wafanyakazi 65,000. Kwa sehemu kubwa, shughuli zetu zinajihusisha na madini, ujenzi wa miundombinu mikubwa, ujenzi wa majengo ya makazi pamoja na hoteli, kilimo na viwanda, utalii na utoaji huduma za mawasiliano,” alisema

 

Mapema, akitoa taarifa kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Bw. Ephraim Mafuru alisema kwa muda mrefu Tanzania ilikuwa ikisafirisha nyama ya mbuzi na kondoo kwenda nchi za Ghuba lakini kwa sasa inaweza kufanya vizuri zaidi endapo itaongeza mazao ya kilimo na madini hasa ya dhahabu.

 

“Tunalo soko kubwa la dhahabu ambalo kimsingi halijatumiwa. Tunajua soko liko hapa katika Ghuba. Lakini pia kuna fursa kubwa kwenye mchele ambao unaweza kutuingizia dola bilioni 3.9. Mwaka jana, tulizalisha tani milioni 3.4 za mchele na tukatumia tani milioni 1.8 tu. Maana yake ni kwamba tuna zaidi ya tani milioni 1.6 ambazo tunaweza kuzisambaza kwa watu milioni 3.4 waishio nchini Qatar.”

 

Akielezea kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania, Bw. Mafuru aliyataja maeneo hayo kuwa ni nishati, LNG, utalii, mbogamboga na matunda, maua, uzalishaji wa malisho ya mifugo pamoja na mazao yanayotokana na uchumi wa bluu.

 

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Dodoma, Wabunge Esther Matiko na Subira Mgallu na watendaji wengine wa Serikali.

TANZANIA NA UTURUKI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA

SERIKALI ya Tanzania imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura ya Uturuki (AFAD), kwa lengo la kuimarisha uwezo wa nchi katika kuzuia na kupunguza athari za maafa, kujiandaa, kukabiliana na dharura na kurejesha hali baada ya maafa kutokea.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, wakati wa kikao cha pamoja kati ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na uongozi wa AFAD kilichofanyika katika ofisi za taasisi hiyo mjini Ankara, Uturuki ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo iliyolenga kuongeza ujuzi na maarifa ya kiufundi, kuimarisha uwezo wa kitaasisi, kujifunza uzoefu wa Uturuki katika kupunguza vihatarishi vya maafa, kujiandaa na kukabiliana na dharura, pamoja na kurejesha hali baada ya maafa kwa kutumia mbinu, mifumo na teknolojia za kisasa.

Dkt. Yonazi amesema Tanzania inathamini uzoefu na utaalamu wa AFAD katika usimamizi jumuishi wa maafa na kwamba Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano huo kwa manufaa ya Tanzania na Uturuki, hususan katika kuendeleza mifumo ya kisasa ya usimamizi wa maafa, teknolojia, mafunzo ya wataalam, utafutaji na uokoaji pamoja na uratibu wa hatua za mwitikio wakati wa dharura. 

“Tanzania itaendelea kujifunza na kushirikiana na taasisi mbalimbali zenye uzoefu katika usimamizi wa maafa, ikiwemo AFAD, ili kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kuzuia na kupunguza athari za maafa, kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali pindi yanapotokea,” amesema Dkt. Yonazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa AFAD nchini humo, Gavana Ali Hamza Pehlivan, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano na Uturuki katika eneo la usimamizi wa maafa na kueleza kuwa AFAD ipo tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya kitaalamu.

Gavana Pehlivan amesema maeneo hayo ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa maafa, mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ya vihatarishi na madhara ya maafa, maandalizi na mwitikio wa dharura, pamoja na uanzishaji, mafunzo na uendelevu wa timu maalumu za utafutaji na uokoaji na upatikanaji wa vifaa vinavyohitajika wakati wa maafa.

Ameeleza kuwa AFAD inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia dhana ya usimamizi jumuishi wa maafa, inayolenga kushughulikia hatua zote za mzingo wa usimamizi wa maafa, kuanzia katika kutambua na kutathmini vihatarishi, kuzuia na kupunguza uwezekano na athari za maafa, kujiandaa, kukabiliana na dharura hadi kurejesha hali pindi maafa yanapotokea. 

Vilevile, AFAD imejenga uwezo wa kuratibu timu za wataalam na vikosi vya utafutaji na uokoaji vinavyoshughulikia majanga mbalimbali, yakiwemo matetemeko ya ardhi, mafuriko na dharura nyingine, kwa lengo la kuokoa maisha na kulinda mali. Taasisi hiyo pia hushiriki katika uratibu wa utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa na kusaidia shughuli za kurejesha hali na makazi katika maeneo yaliyoathirika.

Katika eneo la kujenga uwezo wa rasilimali watu, AFAD inaendesha mafunzo na mazoezi ya vitendo kwa wataalam na timu za mwitikio wa maafa kupitia miundombinu yake ya mafunzo, ikiwemo Disaster and Emergency Training Centre (AFADEM). Mafunzo hayo yanalenga kuongeza ujuzi wa kitaalamu, uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na utayari wa kukabiliana na matukio ya dharura.

Gavana Pehlivan ameongeza kuwa AFAD pia hushiriki katika ushirikiano wa kimataifa wa usimamizi wa maafa kupitia Timu ya Kimataifa cha Utafutaji na Uokoaji (The International Search and Rescue Advisory Group – INSARAG) ambayo inasimamiwa na Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UN-OCHA) katika kupeleka timu maalumu za utafutaji na uokoaji na kutoa msaada wa kibinadamu katika nchi mbalimbali pale kunapojitokeza maafa makubwa.

Tanzania na Uturuki zimeendelea kuwa na fursa ya kubadilishana uzoefu na utaalamu katika eneo la usimamizi wa maafa, hususan katika teknolojia, mifumo ya taarifa na tahadhari za mapema, mafunzo, utafutaji na uokoaji, uratibu wa mwitikio wa kukabili na urejeshaji wa hali, kwa lengo la kujenga jamii na taasisi zenye uwezo mkubwa wa usimamizi wa maafa.

=MWISHO=

GST NA GTK ZAFUNGUA UKURASA MPYA UTAFITI WA MADINI

• *GST na GTK zasaini MoU*

• *Kufanya Utafiti wa Kina wa madini*

• *Kuimarisha upatikanaji wa taarifa za madini*

*Pori, Finland*

Tanzania na Finland zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika utafiti wa madini baada ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia ya Finland (GTK) kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) unaolenga kuimarisha utafiti wa jiolojia na upatikanaji wa taarifa sahihi za rasilimali za madini nchini.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa Septemba 30, 2026, yanahusisha utekelezaji wa Utafiti wa Kijiolojia kwa kutumia ndege ( _Airborne Geophysical Survey)_ pamoja na kuwajengea uwezo wataalam wa GST katika Uhakiki wa Ubora wa Takwimu na Udhibiti wa Ubora.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inathamini ushirikiano huo kwa kuwa una fursa ya kuimarisha uwezo wa Tanzania katika kutambua, kuchambua ili kutambua kiwango cha rasilimali madini zilizopo nchini.

Aliongeza kuwa, taarifa sahihi za kijiolojia ni msingi muhimu katika kufanya tafiti, kupanga matumizi ya rasilimali na kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Madini.

“ _Ushirikiano huu utaleta mabadiliko katika namna Tanzania inavyokusanya, kuchambua na kutumia taarifa za kijiolojia,”_ alisema Mbibo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa GTK, Dkt. Saku Vuori, alisema utekelezaji wa programu ya kuwajengea uwezo wataalam wa GST tayari imeanza, huku wataalam wa GTK wakiendelea kufanya tathmini ya hatua nyingine za utekelezaji.

Dkt. Vuori alisema kuwa, GTK pia iko tayari kuiwezesha GST katika kuimarisha uwezo wa Maabara mpya inayojengwa Dodoma, ikiwemo upatikanaji wa vifaa vya teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uchambuzi na upimaji wa sampuli za miamba na madini.

Hatua hiyo inalenga kuiwezesha Tanzania kupata taarifa za maabara zinazokidhi viwango vya kisasa, ambazo zinaweza kutumika katika utafiti, tathmini ya rasilimali madini na maamuzi ya uwekezaji.

Katika makubaliano hayo, Umoja wa Ulaya (EU) umeonesha nia ya kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa ushirikiano huo, hususan katika kuhakikisha taarifa na takwimu za kijiolojia zinazokusanywa zina ubora na sahihi kwa uwekezaji.

Pamoja na mambo mengine, ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kutembelea maabara ya kisasa ya GTK na kupata maelezo kuhusu matumizi ya teknolojia katika uchambuzi wa sampuli za miamba na madini pamoja na mifumo ya uhakiki na udhibiti wa ubora wa taarifa za kisayansi.

Ziara hiyo imehusisha wajumbe kutoka Wizara ya Madini, GST, Chemba ya Migodi Tanzania, kampuni za uchimbaji madini, Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden, Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Ubalozi wa Finland nchini Tanzania.

Ushirikiano wa Tanzania na Finland unatarajiwa kuongeza uwezo wa wataalam wa Tanzania na kuimarisha upatikanaji wa taarifa za kisayansi zitakazosaidia katika utafiti, uendelezaji na uongezaji thamani katika rasilimali madini nchini.

MUST Yatangaza Nafasi za Ajira kwa Wahitimu Wenye GPA 3.8

Global Publishers
October 1, 2026
930 views
0 Comments

Mbeya University of Science and Technology (MUST) imetangaza nafasi tano (5) za ajira kwa Watanzania wenye sifa, katika kada mbalimbali za Tutorial Assistant, ambapo nafasi zote zipo katika Kampasi Kuu ya Chuo.

Nafasi hizo ni:

  • Tutorial Assistant – Aquatic Science and Aquaculture Technology: Nafasi 1. Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi katika Aquatic Sciences and Aquaculture Technologies, Aquaculture, Aquatic Science, Fisheries au Marine Science, akiwa na GPA isiyopungua 3.8/5.
  • Tutorial Assistant – Health Information Science: Nafasi 1, kwa mwenye Shahada ya Sayansi katika Health Information Systems na GPA isiyopungua 3.8/5.
  • Tutorial Assistant – Interior Design: Nafasi 2, kwa mwenye Shahada katika Interior Design Technology, Bachelor of Science in Interior Design au Bachelor of Interior Architecture, akiwa na GPA isiyopungua 3.8/5.
  • Tutorial Assistant – Inclusive Education: Nafasi 1, kwa mwenye Shahada ya Education in Special Needs and Inclusive Education na GPA isiyopungua 3.8/5.

Waombaji wote wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45. Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba, huku watumishi walio katika utumishi wa umma wakielezwa kutoruhusiwa kuomba nafasi hizo.

Maombi yanapaswa kuwasilishwa kupitia Recruitment Portal ya Ajira, na waombaji wanatakiwa kuambatanisha vyeti vilivyoidhinishwa, transcripts, vyeti vya Form IV na Form VI, cheti cha kuzaliwa, picha ya passport na taarifa za wadhamini watatu.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 6 Oktoba 2026.

Soma zaidi bonyeza link chini

Wadau madini wasisitizwa kuzingatia viwango – HabariLeo

GEITA: SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara wa madini, wachimbaji na wasindikaji kuanzisha mifumo ya usimamizi wa ubora, mazingira, matumizi ya nishati pamoja na afya na usalama mahali pa kazi, ili kuhakikisha shughuli zao zinaendeshwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Magharibi, Joseph Makene, amesema hayo wakati akizungumza katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, ambapo TBS inatoa elimu kwa wadau kuhusu viwango, ubora na usalama wa bidhaa.

Makene amesema TBS imekuwa ikishiriki maonesho hayo tangu yalipoanza Septemba 23 mwaka huu, ikitumia fursa hiyo kuwafikia wajasiriamali na wadau mbalimbali wa sekta ya madini na sekta nyingine.

Amesema mifumo inayosisitizwa ni pamoja na Mfumo wa Usimamizi wa Ubora (Quality Management System), Mfumo wa Usimamizi wa Nishati (Energy Management System), Mfumo wa Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management System), pamoja na Mfumo wa Usimamizi wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi.

“Wadau hawa wakiwa na mifumo hii, hasa mifumo inayokidhi viwango vya kimataifa, wataweza kufanya shughuli zao katika mazingira yanayozingatia viwango vya kimataifa,” amesema.

Aidha, amesema TBS hutoa elimu kuhusu namna ya kuanzisha na kusimamia mifumo hiyo, pamoja na kufanya uhakiki na kutoa vyeti vya mifumo ya usimamizi (Management System Certification) kwa taasisi zinazokidhi matakwa ya viwango husika.

Makene pia amewataka wafanyabiashara wenye maabara zinazotumika katika upimaji wa madini kutumia huduma za maabara ya metrology ya TBS kwa ajili ya uhakiki na urekebishaji (calibration) wa vifaa vyao, ili kuhakikisha vipimo vinavyofanyika vinakuwa sahihi.

Kwa upande wa waingizaji wa bidhaa zinazotumika katika shughuli za uchimbaji madini, amewataka kuhakikisha bidhaa hizo zinakaguliwa na kuthibitishwa ubora kabla ya kuziingiza nchini.

Amesema TBS ina mawakala wa ukaguzi wa bidhaa katika nchi mbalimbali ambao hufanya ukaguzi wa bidhaa kabla hazijasafirishwa kuja Tanzania.

Katika hatua nyingine, Makene amewataka wafanyabiashara wa vipodozi katika Kanda ya Ziwa Magharibi kuhakikisha wanauza bidhaa zinazokidhi viwango na zisizo na viambata sumu.

Ametaja maeneo yanayolengwa katika ukaguzi kuwa ni Geita, Katoro, Runzewe, Kahama, Shinyanga na Bukoba, akisema TBS itaendelea kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa bidhaa hizo.

Amesema wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha vipodozi wanavyouza havina viambata vilivyopigwa marufuku, huku akiwataka kutumia taarifa zinazopatikana kupitia tovuti ya TBS kujua bidhaa ambazo haziruhusiwi.

“TBS Kanda ya Ziwa Magharibi imejipanga kufanya operesheni kubwa katika masoko ya maeneo ya Geita, Katoro, Kahama, Shinyanga na Bukoba, kuweza kuviondoa vipodozi vyote ambavyo vina viambata sumu na kuviteketeza kwa mujibu wa sheria,” amesema Makene.