Global Publishers
October 10, 2026
30 views
0 Comments

Mtanzania Jihan Dimack leo Oktoba 10, 2026 ametwaa taji la Miss Grand International 2026, na kuweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kushinda taji hilo tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Ushindi huo ni hatua kubwa kwa Tanzania katika jukwaa la kimataifa la urembo, ukiifanya nchi kujivunia mafanikio hayo na kuandika ukurasa mpya katika historia ya mashindano ya Miss Grand International.
Kupitia tangazo lililochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Miss Grand International, Jihan ametangazwa kuwa mshindi wa mwaka 2026, huku ujumbe wa ushindi ukisisitiza kuwa huu ni wakati wa Afrika na Tanzania.
Hongera Jihan Mohin Dimachk! Hongera Tanzania! πΉπΏππ
