Rais Samia Ampongeza Jihan Kwa Kutwaa Taji La Miss Grand International 2026

Global Publishers
October 10, 2026
12 views
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Jihan Dimack kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kutwaa taji la Miss Grand International 2026.

Rais Samia amesema ushindi huo ni fahari kwa Taifa na kielelezo cha uwezo wa Watanzania kufikia mafanikio makubwa wanapoungana na kushirikiana.

Aidha, amesema mafanikio hayo ni chachu kwa vijana, hususan wasichana, kujiamini, kuthubutu na kusimamia ndoto pamoja na vipaji vyao ili kufikia malengo makubwa.

“Ninakupongeza kwa dhati, mwanangu Jihan Dimack, kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kutwaa taji la Miss Grand International 2026. Ushindi huu ni fahari kwa Taifa letu na kielelezo cha uwezo wa Watanzania kufikia mafanikio makubwa tunapoungana na kushirikiana.

“Pia, ni chachu kwa vijana, hususan wasichana, kujiamini, kuthubutu na kusimamia ndoto na vipaji vyao.

“Hongera sana. Ninakutakia kila la kheri,” amesema Rais Samia.

Fupisha habari iwe na mtiririko mkaliBoresha sarufi na mtindo wa habari