MILTON: MRITHI WA DR. TULIA IPU

Uchaguzi huo umefanyika leo Oktoba 9, 2026 katika kikao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Mhe. Dick ameshinda kwa asilimia 56  ya kura zote, huku akifuatiwa na Prof. Mhe. Sahiba Gafarova aliyepata asilimia 38 na Mhe. Robi Edwards amepata asilimia 6.

Mhe. Dick anachukua nafasi ya Dkt. Tulia Ackson wa Tanzania, ambaye anamaliza muhula wake wa miaka mitatu.

Mhe. Dick ni Mbunge wa Jimbo la Oxley, Queensland tangu mwaka 2016, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Spika mwaka 2022 na kuchaguliwa tena bila kupingwa mwaka 2025.

Baada ya kuchaguliwa Mhe. Dick amesisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano kwenye umoja huo.