Global Publishers
October 8, 2026
18 views
0 Comments

Aliyekuwa mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, na mke wake, Lucy “Lulu” Muteke, wamezikwa leo, Alhamisi Oktoba 8, 2026, katika Makaburi ya Glen Forest Memorial Park jijini Harare, Zimbabwe.
Wanandoa hao walifariki dunia pamoja na watu wengine watatu katika ajali ya helikopta iliyotokea Septemba 30, 2026, katika eneo la Kudenga Farm, Marondera, takribani kilomita 70 mashariki mwa Harare.

Safari ya kuwasafirisha miili yao kuelekea eneo la mazishi ilivuta umati mkubwa wa watu katika mitaa ya Harare, huku polisi wakifunga baadhi ya barabara kuu kuwezesha msafara huo kupita.
Maelfu ya watu walijipanga kandokando ya barabara kushuhudia msafara huo, huku baadhi wakiwa wamevalia mavazi meupe na wengine wakirekodi kwa simu zao.
Mazishi hayo yamewakutanisha familia, ndugu, marafiki na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali kuaga wanandoa hao na kushiriki katika shughuli za mwisho za mazishi.



