Takwimu Hizi Zinamuweka Lamine Yamal Kwenye Mbio za Ballon d’Or

Mchezaji huyo Raia wa Hispania amezidi kugonga kwenye vichwa vya habari kutokana na kiwango bora anachozidi kuonesha kwenye michuano yote. Je ana nafasi ipi ya kubeba Ballon d’Or?

Akiwa na miaka 19 tu, tayari ana historia ya mataji ya La Liga, Copa del Rey, Super Cup, Euro 2024 na World Cup 2026. Barcelona yenyewe inaeleza kuwa msimu wa 2025/26 alifunga mabao 24 na akachaguliwa kuwa mchezaji bora wa La Liga.

Lamine Yamal ameendelea kuonesha umuhimu wake kwenye klabu yake ya Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania chini ya kocha mkuu Luis de la Fuente amekuwa ni mchezaji wa muhimu sana na ambaye anazidi kumarika kila siku.

Zipo sababu nyingi zinazomfanya Lamine kuwa mchezaji wa kipekee kutokana na namna anavyoweza kubadilisha mchezo akiwa na mpira mguuni. Ana uwezo wa kumkabili beki mmoja dhidi ya mmoja, kuingia ndani kutoka upande wa kulia, kutumia mguu wa kushoto kutengeneza nafasi kwa wenzake pia.

Hiyo ndiyo moja ya sababu takwimu zake zinaonekana zaidi kama za mchezaji anayekamilika kuanzia kule La Liga msimu wa 2026/27 pekee tayari ana mabao 7 na assists 4 katika mechi 7.

Piga pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Vilevile kijana huyo ameonesha uthubutu wake kwenye mechi kubwa ambapo haoneshi kuhitaji muda mrefu kuingia kwenye mchezo. Ikumbukwe kuwa mwezi Septemba alikuwa na mwezi wa ajabu kwani alipachika nyavuni mabao 9 na assists 7 kwa Barcelona na Hispania.

Pia alihusika moja kwa moja kwenye mabao 16 ndani ya mwezi mmoja. Kwa Hispania, alifunga dhidi ya Uingereza, akaifunga Croatia mara mbili, kisha akafunga tena dhidi ya Czechia. Jisajili hapa.

Kutokana na jina lake kuimbwa na mashabiki wengi na kumfanya kuwa ni moja ya wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu, Lamine sasa anajikuta kwenye mazingira ya kutakiwa kufanya vyema kwenye kila mechi ambayo anacheza. Akicheza vizuri, watu wanataka zaidi akicheza kawaida, wanaanza kusema ameshuka kiwango. Hii ni presha ambayo wachezaji wengi huanza kuipitia wakiwa na miaka 23–25, lakini Yamal anakutana nayo akiwa bado kijana sana.

Kwa upande wa Ballon d’Or, si ajabu kabisa kwamba Yamal ametajwa miongoni mwa majina makubwa yanayowania tuzo ya 2026 pamoja na Kylian Mbappé na Harry Kane.

Mchezaji huyo ni tunu kwa timu ya Hans Flick na Luis de la Fuente huku wengi wakijiuliza kama ataendelea kuonesha kiwango hicho hicho miaka yote.