Jkt Queens Yapoteza Ngao ya Jamii, Simba Queens Yaibuka Mabingwa

Global Publishers
October 3, 2026
0 views
0 Comments

Simba Queens leo Oktoba 3, 2026 wameanza msimu kwa kutwaa Ngao ya Jamii Wanawake 2026 baada ya kuifunga JKT Queens bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa KMC Complex.

Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Aisha Mnunka, ambaye ameipa Simba Queens ushindi na hatimaye kutwaa taji hilo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kuivua JKT Queens ubingwa wa Ngao ya Jamii na kuanza msimu kwa kumbukumbu nzuri baada ya kuondoka na ushindi katika mchezo huo wa fainali.