Global Publishers
October 1, 2026
930 views
0 Comments
Jihan Dimack ameendelea kufanya vizuri katika kipengele cha Country’s Power of the Year cha Miss Grand International 2026, baada ya Tanzania kufanikiwa kuingia Top 8.
Kutoka Group A, Tanzania imeingia Top 8 pamoja na Chile. Nchi nyingine zilizofuzu ni Ecuador, Pakistan, Philippines, Guatemala, Vietnam na Paraguay.
Hatua inayofuata imeanza leo, Septemba 30, 2026, na kura zitapigwa kwa muda wa saa 24 hadi Oktoba 1, 2026. Katika hatua hii, washiriki wanne pekee kati ya Top 8 wataendelea kwenda hatua inayofuata.

Kura zinapigwa kupitia tovuti rasmi ya Miss Grand International, ambapo kura moja ni 2,800. Kura za hatua hii pia zitaongezwa kwenye jumla ya alama za Miss Popular Vote.
Watanzania, safari bado inaendelea!
Nguvu iwe kwa Jihan Dimack. Kura yako inaweza kusaidia Tanzania kusonga mbele!
Twende Jihan! Twende Tanzania!

