Vita Kali Serie A, LaLiga na EPL Kitawaka leo Jumapili, Juventus vs Milan, Arsenal vs Chelsea

Je unajua kuwa wikendi iliyopita kuna watu wameweza kubadili maisha yao kwa dau dogo kabisa la shilingi mia tano?. Huenda leo ikawa ni nafasi yako na wewe na unachotakiwa kufanya ni kutengeneza jamvi lako na ubeti sasa.

Kule SERIE A kuna mechi zitaendelea, lakini mechi kali ni hii ya Juventus vs AC Milan mchezo ambao tayari umebeba uzito mkubwa kwa sababu timu zote mbili zimeanza ligi kwa ushindi wa asilimia 100.

Juventus wamefungua msimu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Frosinone na 2-0 dhidi ya Parma, huku Milan wakiwashinda Torino 2-1 na Venezia 2-0. Hivyo, hii ni vita ya timu mbili ambazo bado hazijapoteza pointi.

Bibi Kizee wanaonekana kuwa na mwanzo wenye utulivu zaidi upande wa ulinzi. Katika mechi zao mbili za kwanza hawajaruhusu bao lolote, jambo linaloonyesha nidhamu ambayo kocha Luciano Spalletti ameanza kuijenga. Ushindi wa 2-0 dhidi ya Parma pia ulionyesha kwamba Juventus wanaweza kupata tofauti kupitia wachezaji wanaotokea benchi, baada ya Nico González na Teun Koopmeiners kuamua mchezo.

Wakati  AC Milan, wao mwanzo wao pia umeleta matumaini makubwa. Ushindi dhidi ya Torino na Venezia umeonyesha kwamba kikosi kinaweza kupata matokeo hata kama hakitawali kila dakika ya mchezo. Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba Milan wanaingia katika mchezo huu chini ya kocha Ruben Amorim, ambaye anaanza kujenga utambulisho mpya wa timu.

Kwahiyo yoyote ambaye atakuwa amejiandaa vyema anaweza akaondoka na ushindi kule Meridianbet ambapo pia kuna machaguo zaidi ya 1000 yakiwa yanakungoja siku ya leo. Jisajili hapa.

Tengeneza pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kule Hispania LALIGA pia itaendelea ambapo Valencia watawaleta kwao Barcelona ambao ni mabingwa watetezi wa ligi na wanahitaji kupata ushindi kuendelea kujikita kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Valencia wapo katika hali ngumu zaidi baada ya kukusanya pointi moja pekee katika mechi tatu, hivyo mechi hii wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki zao wanahitaji kuthibitisha kuwa wanaweza kupambana na timu kubwa.

Barcelona wameonyesha ubora mkubwa katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi tatu za mwanzo wamefunga mabao 12, huku wakiruhusu mawili pekee. Ushindi wa 5-2 dhidi ya Rayo Vallecano ulikuwa uthibitisho mwingine wa uwezo wao wa kutengeneza nafasi na kumaliza mashambulizi, huku Raphinha na Lamine Yamal wakifunga mabao mawili kila mmoja. Meridianbet wanakwambia beti mechi hii sasa.

Kule Uingereza EPL itakuwa ya moto haswa kwani Dunia nzima itakuwa ikisubiri mechi ya London Derby kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya kuvutia haswa kwani zinakutana timu mbili ambazo zote zinahitaji ushindi kwenye mechi hii ya leo.

Arsenal chini ya Arteta ndio mabingwa watetezi wa ligi, lakini pia wamenza vyema kabisa ligi kwa kushinda mechi zake mbili bila kuruhusu bao lolote kwani wamekuwa na ukuta bora kwenye ligi nzima baada ya kuruhusu magoli machache msimu uliopita.

Huku kwa upande wa Chelsea wao msimu uliopita ulikuwa wa kusua sua kwao wakishindwa kujipatia mpaka nafasi za kushiriki michuano mikubwa ya Ulaya kama vile Uefa, Europa na hata Conference na kufanya maamuzi ya kuachana na aliyekuwa kocha wao na kuajiri kocha mpya. Jisajili hapa.

The Blues wamefanya usajili msimu huu kwaajili ya kuimarisha kikosi ikiwemo kusajili golikipa Emiliano kutokana na makosa ambaypo Sanchez alikuwa nayo, hivyo mechi hii inaenda kuwa ya ushindani mkubwa wakiwa na kocha mpya Alonso.

Arsenal wameendelea kuwa wababe mbele ya vijana hao wa Darajani kwani mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa ni msimu wa 2021, hivyo ni muda mrefu sana hawajapata ushindi?. Je nani kuondoka na ushindi?. Beti hapa.

Tanzania Yaanza Kwa Kishindo CAF, Simba na Singida Zang’ara Ugenini

Global Publishers
September 6, 2026
36 views
0 Comments

Timu za Tanzania zimeanza kwa matokeo mazuri katika mashindano ya klabu Afrika, huku Simba SC na Singida Black Stars zikirejea nyumbani na ushindi katika mechi zao za kwanza za raundi ya kwanza ya kufuzu.

Simba leo Septemba 6, 2026 imeanza kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) 2026/27 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Bingu National Stadium nchini Malawi.

Bao pekee la Simba lilifungwa dakika ya 65 na Oura, huku kipa Djibril Kassim akihusishwa na assist ya bao hilo.

Kwa upande mwingine, Singida Black Stars imeichakaza Al-Ghazala SC Wau ya Sudan Kusini kwa mabao 7-1 ugenini katika raundi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).

Tegisi alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufunga hat-trick ndani ya kipindi cha kwanza, akifunga dakika za 20, 23 na 32.

Sheikhan aliongeza bao la nne dakika ya 41, kabla ya Sowah kufunga dakika ya 63. Henry alifunga bao la sita dakika ya 86, huku Sowah akifunga tena dakika ya 90 kukamilisha ushindi mkubwa wa Singida.

Matokeo hayo yamewapa Simba na Singida mwanzo mzuri katika safari zao za kuwania nafasi ya kufuzu hatua za juu za mashindano ya klabu Afrika.

DKT. MWIGULU ATOA WITO WA MAANDALIZI YA MAPEMA KUKABILI ATHARI ZA EL NIÑO

*_▪︎ Atoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya mafuriko_*

*_▪︎ Aagiza ndani ya Septemba kutangazwa zabuni ya ujenzi wa barabara km 11 za Igauri–Ilongero_*

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania na viongozi katika ngazi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño.

Dkt. Mwigulu ametoa rai hiyo leo, Jumapili, Septemba 06, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ilongero, Wilaya ya Singida, mkoani Singida, katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema maeneo yenye historia ya mafuriko yanapaswa kutambuliwa mapema na hatua za tahadhari kuchukuliwa, huku akiwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuzingatia taarifa na maelekezo ya mamlaka husika.

“Maeneo ambayo mnaona ni ya hatari sana Watanzania tunayajua. Tunayajua maeneo yenye historia ya mafuriko. Ni vyema tukaanza kuchukua tahadhari kwa sababu hicho ndicho tunachoweza kukifanya,” alisema.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuimarisha uwezo wa kukabiliana na athari za mvua, ikiwemo kuwa na magari ya kuchimba mabwawa katika kila ukanda, huku akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuepuka kujenga au kuishi katika maeneo yanayofahamika kuwa hatarishi kwa mafuriko.

Kuhusu barabara ya Igauri–Ilongero, Dkt. Mwigulu ametoa agizo la kuhakikisha ndani ya mwezi huu mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa kilomita 11 za awali unakamilika.

“Ndani ya mwezi huu huu, muwe mmeshatangaza kupata mkandarasi wa kuanza kujenga hizi kilomita 11 za awali ambazo zitaziba hili pengo kuanzia hapa mpaka kwenye lami na kupita kidogo mji wa Ilongero,” alisema.

Alisema fedha kwa ajili ya mradi huo zipo na kinachosubiriwa ni kumpata mkandarasi, akisisitiza kuwa ujenzi huo unapaswa kuanza haraka.

Dkt. Mwigulu pia amesisitiza umuhimu wa Serikali kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha zinazookolewa kwenye maeneo yenye kipaumbele, hususan elimu, afya, maji na miundombinu.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2028, hivyo Serikali inapaswa kuanza mapema maandalizi ya madarasa, maabara, maktaba na mahitaji mengine ya elimu.

“Ni fedha ya Serikali, ni fedha ya walipa kodi wa Tanzania, ni fedha ambayo inaweza kwenda kutatua hizi changamoto watoto wasikae chini,” alisema.

Kuhusu afya, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ambulensi zinapaswa kuwa tayari muda wote na kuwa na mafuta ili wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura na rufaa wasicheleweshwe.

“Ambulensi zetu ziwe standby. Tulishanunua magari, yawe na mafuta. Kila wakati yawe na mafuta. Tusichangishe wagonjwa kuweka mafuta kwenye gari ya Serikali kubeba mgonjwa ambaye yuko mautini,” alisema.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote, akisema mfumo huo ni suluhisho la kudumu la kupunguza utegemezi wa michango ya dharura wakati wananchi wanapokabiliwa na gharama za matibabu.

“Watanzania wote tuingie kwenye bima ya afya. Tutaepukana na matatizo mengi sana ambayo tumeyatafutia majawabu ya dharura, lakini yanahitaji yapate majawabu ya kudumu,” alisema.

Kuhusu maji, Dkt. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji na umwagiliaji kwa ushirikiano wa wizara zinazohusika, ili miradi hiyo iweze kunufaisha wananchi, mifugo na shughuli za uzalishaji.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia matumizi yenye tija ya rasilimali za umma na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha, ufanisi na mahitaji halisi ya wananchi.

Ajira Mpya 678 Zatangazwa Serikalini, Madaktari na Walimu Watajwa

Dodoma, Septemba 3, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya

Tangazo hilo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/56, limetolewa Septemba 3, 2026, likiwa na nafasi katika kada mbalimbali kuanzia madaktari, wauguzi, walimu, wataalamu wa mifugo hadi watumishi wa ofisi.

Nafasi zilizotangazwa

1. Daktari Daraja la II – Nafasi 115

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Udaktari kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, wawe wamekamilisha mafunzo ya Internship na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika.

Majukumu yanahusisha kutoa huduma za matibabu, elimu ya afya, kuzuia milipuko ya magonjwa, kutunza takwimu za afya, kusimamia watumishi na kushiriki katika kuboresha ubora wa huduma za afya.

Mshahara: TGHS E

2. Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II – Nafasi 128

Nafasi hizi ni kwa wenye Stashahada ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

Mshahara: TGHS B3. Afisa Mifugo Daraja la II – Nafasi 39

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Wanyama (Animal Science) au Shahada ya Sayansi ya Kilimo aliyebobea katika Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au sifa inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu yanahusisha kupanga na kusimamia uzalishaji wa mifugo, kutoa mafunzo kwa wafugaji, kuratibu miradi ya mifugo, kukusanya takwimu na kushiriki katika kudhibiti changamoto zinazohusiana na mifugo na mazingira.

Mshahara: TGS D

4. Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja la II – Nafasi 17

Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada ya Tabibu wa Meno (Diploma in Clinical Dentistry) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Baraza la Madaktari.

Mshahara: TGHS B

5. Mteknolojia Maabara Daraja la II – Nafasi 25

Nafasi hizi ni kwa wenye Stashahada katika Uteknolojia wa Maabara za Afya kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa amesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara.

Mshahara: TGHS B

6. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 74

Waombaji wanatakiwa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, pamoja na Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6).

Wanapaswa pia kuwa wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kasi ya maneno 100 kwa dakika moja na kuwa na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Mshahara: TGS C

7. Mwalimu Daraja la III C – Fizikia – Nafasi 55

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Elimu/Bachelor of Education yenye somo la Fizikia au shahada isiyo ya ualimu yenye Fizikia kama somo la kufundishia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE).

Mshahara: TGTS D

8. Mwalimu Daraja la III C – Hisabati – Nafasi 67

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Elimu/Bachelor of Education yenye Hisabati kama somo la kufundishia, au shahada isiyo ya ualimu yenye Hisabati pamoja na PGDE.

Mshahara: TGTS D

9. Mwalimu Daraja la III B – Fizikia – Nafasi 43

Nafasi hizi ni kwa wahitimu wenye Cheti cha Kidato cha Sita waliofaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na wenye Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili yenye Fizikia kama somo la kufundishia.

Mshahara: TGTS C

10. Mwalimu Daraja la III B – Hisabati – Nafasi 48

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Sita, wakiwa wamefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni, pamoja na Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili yenye Hisabati kama somo la kufundishia.

Mshahara: TGTS C

11. Afisa Misitu Msaidizi Daraja la II – Nafasi 28

Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada katika fani kama Forestry, Agroforestry, Forest Resources Assessment and Management, Forest Biology, Forest Economics, Forest Engineering au fani inayohusiana.

Majukumu ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mbegu na bustani za miti, kukusanya takwimu za misitu, kusimamia upandaji na utunzaji wa miti, kupima mazao ya misitu na kufanya doria.

Mshahara: TGS C

12. Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II – Nafasi 26

Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.

Majukumu yanahusisha kudhibiti milipuko ya magonjwa, kutoa elimu ya afya ya mazingira, kukagua usalama wa maeneo ya chakula, kusimamia sheria za afya ya mazingira na kuhamasisha jamii kuhusu usafi na afya.

Mshahara: TGHS B

13. Mwalimu Daraja la III C – Fasihi ya Kiingereza – Nafasi 13

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Elimu/Bachelor of Education yenye Fasihi ya Kiingereza kama somo la kufundishia, au shahada isiyo ya ualimu yenye somo hilo pamoja na PGDE.

Mshahara: TGTS D

Masharti muhimu ya maombi

Waombaji wote wanatakiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa maombi.

Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, pamoja na vyeti vya elimu na vyeti vya kitaaluma vinavyohitajika kwa nafasi husika.

Sekretarieti ya Ajira imesisitiza kuwa Testimonials, Provisional Results, Statement of Results pamoja na Result Slips za Kidato cha Nne na Kidato cha Sita hazitakubaliwa.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET, kulingana na sifa husika.

Aidha, waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ya nafasi hizi ni Septemba 17, 2026.

Maombi yote yanatakiwa kutumwa kwa njia ya kielektroniki kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira.

Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuambatishwa pamoja na vyeti vinavyohitajika na ielekezwe kwa:

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
S.L.P. 2320,
DODOMA.

Sekretarieti ya Ajira imeonya kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliowekwa hayatafikiriwa.

Aidha, waombaji wamekumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unapaswa kuzingatia misingi ya haki, usawa na uwazi.

Limetolewa na:
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Linah Aendelea Kung’ara na EP Yake Mpya ya Love Notes – Video


Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Linah, anaendelea kuwafikia mashabiki kupitia EP yake mpya ya LOVE NOTES, inayobeba nyimbo zinazozungumzia mapenzi, hisia na mahusiano.

EP hiyo imekusanya nyimbo zenye ladha ya Bongo Flava na ujumbe wa kimapenzi, huku Linah akitumia sauti yake kuelezea hisia mbalimbali zinazopatikana katika mahusiano.

Wimbo wa kwanza katika EP hiyo, “Raha”, unaelezea hisia za upendo na furaha inayopatikana unapompata mtu wa kipekee katika maisha. Wimbo huo umeambatana na video rasmi ya muziki inayomualika msikilizaji kuingia katika ulimwengu wa LOVE NOTES.

Akifuata ni “Huyu”, wimbo wa pili unaosisitiza mapenzi ya dhati, kujitoa na uhusiano wa karibu kati ya watu wawili. Kupitia wimbo huo, Linah anaeleza hisia za kumpenda mtu ambaye ana nafasi kubwa katika maisha yake.

Wimbo wa tatu, “Nipo”, unaendeleza simulizi hiyo ya mapenzi kwa kuzungumzia uaminifu, uwepo na kusimama pamoja na mtu unayempenda katika nyakati mbalimbali za maisha.

Kwa ujumla, LOVE NOTES ni mkusanyiko wa nyimbo unaomweka Linah katika safari ya kusimulia hadithi tofauti za mapenzi na mahusiano kupitia muziki.

EP hiyo tayari inapatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikiliza muziki, yakiwemo Spotify, Apple Music, Boomplay, Audiomack na YouTube Music.

Mashabiki wanaweza pia kutazama video rasmi za nyimbo hizo kupitia YouTube, kushiriki maoni yao na kusambaza nyimbo hizo kwa watu wao wa karibu.

Kwa LOVE NOTES, Linah anaendelea kuonyesha upande wake wa kimuziki unaogusa hisia, huku mapenzi yakiwa kiini cha safari hii mpya ya muziki.

Watuhumiwa 199 Wakamatwa Kwa Makosa Mbalimbali Rufiji

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limekamata jumla ya watuhumiwa 199 kwa makosa mbalimbali katika operesheni na misako iliyofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 31, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, watuhumiwa hao walikamatwa kwa makosa yakiwemo unyang’anyi, wizi, uvunjaji, kupatikana na nyara za Serikali, mali zinazodhaniwa kuwa za wizi, dawa za kulevya na pombe ya moshi (gongo).

Katika operesheni hiyo, Polisi imekamata pikipiki 24 za aina mbalimbali, baadhi zikiwa hazina namba za usajili na zikidaiwa kuwa mali ya wizi. Watu waliokutwa nazo walishindwa kutoa uthibitisho wa umiliki, huku uchunguzi ukiendelea kubaini wamiliki halali.

Aidha, Polisi imewakamata watuhumiwa saba kwa makosa ya uvunjaji, ambapo walikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi pamoja na vifaa vya kuvunjia. Kesi zao zinaendelea katika hatua mbalimbali za kisheria.

Katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, jumla ya kilo 22 na gramu 405 za bangi zilikamatwa pamoja na watuhumiwa 66. Polisi pia ilikamata lita 63 za pombe ya moshi (gongo) na kuwakamata watuhumiwa 11, akiwemo Fatuma Paulo Madebe (40), mkazi wa Mangwi, Wilaya ya Kibiti, aliyekutwa na mtambo wa kutengeneza gongo.

Kwa upande wa kesi zilizofikishwa mahakamani, Polisi Rufiji imesema watuhumiwa 19 wenye makosa mbalimbali, yakiwemo uvunjaji, wizi, ubakaji na kujeruhi, wamehukumiwa na kupewa adhabu mbalimbali, ikiwemo vifungo gerezani.

Katika kesi ya ukatili wa kijinsia, Maneno John Mboko (49), mkazi wa Tambani, Wilaya ya Mkuranga, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 12. Mahakama pia imemuamuru kulipa fidia ya Sh milioni 3 kwa mhanga.

Jeshi la Polisi pia limekamata madereva wanne kwa makosa ya usalama barabarani kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magari (VTS), huku baadhi wakifutiwa madaraja ya leseni na wengine kufikishwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kufichua uhalifu na wahalifu, huku akisisitiza kuwa operesheni za kupambana na uhalifu zinaendelea.

Ajira Mpya Dar: Supervisor – Mshahara Tsh 700,000 Tuma Maombi Yako Sasa!

Global Publishers
September 6, 2026
1,086 views
0 Comments

Location: Dar es Salaam, Tanzania
Salary: TSh 700,000 kwa mwezi

Kampuni inakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye uwezo, uwajibikaji na bidii kwa nafasi ya Supervisor. Mwombaji atakayefanikiwa atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za kila siku pamoja na kuhakikisha timu inafanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa.

Sifa za Mwombaji

  • Awe na kiwango cha chini cha elimu cha Diploma.
  • Awe anaishi Dar es Salaam kwa sasa.
  • Uzoefu wa kazi katika nafasi ya usimamizi au uongozi utakuwa ni faida.
  • Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano na kushirikiana na watu.
  • Awe na uwezo wa kusimamia na kuhamasisha timu.
  • Awe mwaminifu, mwenye nidhamu na anayewajibika.
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi chini ya presha na kufikia malengo.
  • Ujuzi wa msingi wa matumizi ya kompyuta utakuwa ni faida.

Majukumu Makuu

  • Kusimamia na kuratibu shughuli za kila siku.
  • Kusimamia na kufuatilia utendaji wa wafanyakazi.
  • Kuandaa ripoti za kila siku na kila wiki.
  • Kuhakikisha sera na taratibu za kampuni zinafuatwa.
  • Kushughulikia changamoto za wateja na wafanyakazi kwa weledi.
  • Kuhakikisha malengo na shughuli za kila siku zinafikiwa.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma CV zao kupitia barua pepe:

📧 [email protected]

Waombaji waliochaguliwa pekee ndio watakaowasiliana nao.

📌 Tuma maombi yako sasa!

Fahamu Maajabu Ya Israel Historia, Uchumi, Teknolojia Na Nguvu Za Kijeshi

Israel iko Mashariki ya Kati, kwenye mwambao wa Bahari ya Mediterania. Ni nchi yenye eneo dogo ukilinganisha na mataifa mengi duniani, lakini ina idadi kubwa ya watu mijini na uchumi unaotegemea kwa kiasi kikubwa huduma, teknolojia, biashara na ubunifu.

Israel ilianzishwa kama taifa la kisasa mwaka 1948, baada ya Azimio la Uhuru la Mei 14, 1948. Kuanzishwa kwake kulifuatia mchakato mrefu wa kisiasa na kihistoria uliokuwa umehusisha harakati ya Kizayuni, utawala wa Waingereza Palestina na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1947 wa kugawa eneo hilo.

Lakini tangu kuanzishwa kwake, Israel imekuwa katika mgogoro mkubwa na majirani zake wa Kiarabu pamoja na suala la Palestina. Vita vya 1948, 1967 na 1973 ni miongoni mwa matukio yaliyounda historia yake ya kisasa.

Jambo la kushangaza: nchi yenye mazingira magumu imekuwa nguvu ya kilimo

Sehemu kubwa ya kusini mwa Israel ina mazingira ya ukame na jangwa. Hata hivyo, nchi hiyo imekuwa maarufu duniani kwa kilimo cha kisasa kinachotumia maji kwa ufanisi mkubwa.

Moja ya teknolojia maarufu iliyotengenezwa na kutumiwa kwa kiwango kikubwa Israel ni drip irrigationumwagiliaji unaopeleka maji moja kwa moja karibu na mizizi ya mmea.

Mfumo huu umesaidia kupunguza upotevu wa maji na kuwezesha uzalishaji wa kilimo katika maeneo yenye ukame.

Kwa hiyo, badala ya kuiona changamoto ya maji kama tatizo pekee, Israel imeigeuza kuwa kichocheo cha ubunifu wa kiteknolojia. OECD inaeleza kuwa uhaba wa maji ni changamoto kubwa nchini humo na kwamba Israel imekuwa mstari wa mbele katika teknolojia zinazohusiana na maji.

Maajabu ya maji: kutoka uhaba hadi teknolojia ya desalination

Israel imewekeza sana katika desalination, yaani kuondoa chumvi kwenye maji ya bahari ili kuyafanya yaweze kutumika.

Hii ni muhimu kwa sababu nchi ina rasilimali chache za asili na sehemu zake zina mazingira ya jangwa.

Teknolojia za maji zimekuwa sehemu ya sekta yake ya biashara na pia zimeifanya Israel kuwa miongoni mwa nchi zinazotajwa sana duniani katika usimamizi wa maji.

Funzo kubwa: Israel haikungoja mazingira yabadilike; iliwekeza katika teknolojia ili kuendana na mazingira yake.

Israel imejenga uchumi wa teknolojia ya juu

Hapa ndipo moja ya “maajabu” makubwa ya Israel yalipo.

Israel imejenga mazingira makubwa ya startups, cybersecurity, artificial intelligence (AI), fintech, medical technology, software na defence technology.

OECD inaeleza kuwa sekta ya high-tech ni moja ya injini muhimu za ukuaji wa uchumi wa Israel, uzalishaji na mauzo ya nje. Pia inaeleza kuwa AI imekuwa sehemu kubwa ya shughuli mpya za high-tech nchini humo.

Nchi hiyo imekuwa maarufu kwa jina lisilo rasmi la:

“Startup Nation.”

Sababu ni mfumo unaounganisha:

  • vyuo vikuu,
  • utafiti wa kisayansi,
  • jeshi,
  • startups,
  • venture capital,
  • makampuni makubwa ya kimataifa,
  • na wafanyakazi wenye utaalamu wa teknolojia.

Kwa nini Israel ina startups nyingi?

Moja ya siri ni kuunganisha utafiti, elimu, jeshi na sekta binafsi.

Vijana wengi hupata uzoefu katika mazingira ya teknolojia na uhandisi kupitia huduma ya kijeshi. Baadhi yao baadaye huingia katika sekta binafsi na kuanzisha kampuni.

Mfumo huo umechangia kuibuka kwa makampuni katika maeneo kama:

Cybersecurity → AI → software → chips → medical technology → defence technology → telecommunications.

Hii haimaanishi kila startup inafanikiwa. Kinyume chake, startups nyingi hushindwa. Lakini mfumo wa uwekezaji na utafiti unaruhusu baadhi ya kampuni kukua kwa kasi sana.

Uchumi wake ukoje?

Israel ni mwanachama wa OECD tangu mwaka 2010.

Uchumi wake unategemea kwa kiasi kikubwa:

  • High-tech
  • Software
  • Cybersecurity
  • AI
  • Medical technology
  • Pharmaceuticals
  • Diamond trade
  • Defence industries
  • Tourism
  • Financial services
  • Natural gas
  • Agriculture

Ugunduzi wa gesi asilia baharini katika miaka ya 2000 pia uliathiri sana mfumo wa nishati wa Israel na kupunguza utegemezi wake wa baadhi ya mafuta kutoka nje.

OECD inaonyesha kuwa licha ya misukosuko ya vita, uchumi wa Israel umeonyesha uwezo mkubwa wa kustahimili mishtuko kutokana na mfumo wa fedha, sekta ya high-tech na misingi ya uchumi binafsi.

Sasa tuangalie nguvu zake za kijeshi

Israel ina moja ya majeshi yenye uwezo mkubwa zaidi Mashariki ya Kati.

Nguvu yake haitegemei idadi kubwa ya wanajeshi pekee, bali inategemea sana:

Teknolojia + ujasusi + ndege + makombora + mifumo ya ulinzi + cyber + drones + satelaiti + viwanda vya ndani vya silaha.

Mfumo maarufu zaidi kwa umma ni Iron Dome, ambao umeundwa kukabiliana na baadhi ya makombora yanayorushwa kuelekea maeneo yenye watu.

Lakini Iron Dome si mfumo pekee.

Israel ina mtandao wa mifumo ya ulinzi wa anga na makombora unaojumuisha mifumo kama:

  • Iron Dome
  • David’s Sling
  • Arrow

Pia ina uwezo mkubwa wa anga kupitia ndege za kivita za kisasa, pamoja na teknolojia za drones na mifumo ya ujasusi.

Israel hutumia pesa nyingi sana kwenye ulinzi

Kwa takwimu za karibuni za SIPRI, Israel ilitumia takribani dola bilioni 48.3 katika matumizi ya kijeshi mwaka 2025.

Hiyo ilikuwa karibu 7.8% ya GDP yake, kiwango cha juu sana kimataifa. Israel ilikuwa nchi ya 11 duniani kwa matumizi ya kijeshi kwa thamani ya dola mwaka huo.

Kwa kulinganisha, mwaka 2024 matumizi yake ya kijeshi yaliongezeka kwa asilimia 65 hadi takribani dola bilioni 46.5, kutokana na vita na migogoro ya kikanda.

Hivyo, sehemu kubwa ya nguvu ya Israel inatokana na uwekezaji wa muda mrefu katika teknolojia ya kijeshi, si idadi ya watu pekee.

Ujasusi ni sehemu muhimu sana

Israel pia inajulikana kwa uwezo wake wa kijasusi.

Mashirika yake ya ujasusi yanayojulikana zaidi ni:

  • Mossad – ujasusi wa nje.
  • Shin Bet – usalama wa ndani.
  • Aman – ujasusi wa kijeshi.

Uwezo wa kukusanya na kuchambua taarifa ni sehemu muhimu ya mfumo wake wa usalama.

Hapa ndipo teknolojia, cyber, drones, satelaiti na intelligence zinapoungana.

Israel na cybersecurity

Israel ni moja ya vituo muhimu duniani katika cybersecurity.

Kampuni nyingi zinazotengeneza bidhaa za usalama wa mtandao zimeanzishwa au zina shughuli kubwa nchini humo.

Sababu moja ni kwamba teknolojia za kijeshi na kijasusi zimekuwa chanzo cha utaalamu ambao baadaye unaweza kuhamia katika sekta binafsi.

Ndiyo maana Israel ina nafasi kubwa katika soko la:

Cyber defence, threat detection, identity security, cloud security na data protection.

11. Elimu na utafiti

Chuo kikuu na taasisi za utafiti zimekuwa sehemu muhimu ya maendeleo yake.

Vyuo kama Technion – Israel Institute of Technology, Hebrew University of Jerusalem na Weizmann Institute of Science vimekuwa muhimu katika sayansi, engineering na research.

Mfumo huu unasaidia kuzalisha wataalamu katika:

  • Engineering
  • Computer science
  • Medicine
  • Physics
  • Chemistry
  • Biotechnology
  • AI

Afya na teknolojia ya tiba

Israel pia imewekeza sana katika medical technology.

Teknolojia zinazohusiana na:

  • medical devices,
  • digital health,
  • pharmaceuticals,
  • diagnostics,
  • biotechnology,

ni sehemu ya sekta yake ya high-tech.

Hii ni sababu nyingine kwa nini nchi ndogo inaweza kuwa na ushawishi mkubwa kuliko ukubwa wake wa kijiografia.

Lakini kuna upande mwingine wa hadithi

Ni muhimu kutokuiangalia Israel kama simulizi la mafanikio pekee.

Maendeleo yake yameambatana na:

  • migogoro ya Israel na Palestina,
  • vita vya mara kwa mara,
  • matumizi makubwa ya kijeshi,
  • gharama za ulinzi,
  • mgawanyiko mkubwa wa kisiasa,
  • gharama kubwa za maisha,
  • na changamoto za kijamii na kiuchumi.

Siri kuu ya mafanikio ya Israel

Ukichanganua historia yake, unaweza kuona nguzo kadhaa:

🧠 1. Elimu

Imewekeza katika sayansi, mathematics, engineering na technology.

🔬 2. Utafiti

Utafiti wa vyuo na taasisi umeunganishwa na biashara.

💰 3. Mtaji

Venture capital imekuwa muhimu katika kukuza startups.

🪖 4. Ulinzi

Changamoto za kiusalama zimechochea uwekezaji mkubwa katika teknolojia.

💻 5. Teknolojia

Cybersecurity, AI, software na defence tech zimekuwa sekta muhimu.

💧 6. Uhaba wa maji

Changamoto ya maji imechochea desalination, recycling na irrigation.

🌵 7. Mazingira magumu

Sehemu za jangwa zimekuwa maabara ya kilimo na teknolojia.

🌍 8. Soko la kimataifa

Kwa kuwa soko la ndani ni dogo, kampuni nyingi hulenga masoko ya nje mapema.

Kwa kifupi

Maajabu ya Israel si kwamba ina rasilimali nyingi kuliko nchi nyingine. Kinyume chake, ina rasilimali chache katika maeneo mengi, lakini imejenga mfumo unaogeuza changamoto kuwa teknolojia.

Maji machache → desalination na water technology.
Jangwa → advanced agriculture.
Vitisho vya usalama → defence technology na cybersecurity.
Soko dogo → startups zinazolenga dunia nzima.
Rasilimali chache → uchumi unaotegemea maarifa na teknolojia.

Na upande wa kijeshi, Israel imejenga uwezo mkubwa kupitia mchanganyiko wa bajeti kubwa ya ulinzi, utafiti, teknolojia, ujasusi, sekta binafsi ya defence na ushirikiano wa kimataifa. SIPRI inaonyesha kwamba mzigo wake wa kijeshi ulikuwa 7.8% ya GDP mwaka 2025, ukiwa miongoni mwa viwango vya juu zaidi duniani.

Joheirry Mola Aibuka Mshindi wa Miss World 2026 nchini Vietnam

Global Publishers
September 6, 2026
66 views
0 Comments

Mshiriki kutoka Dominican Republic, Joheirry Mola, ametangazwa kuwa mshindi wa mashindano ya Miss World 2026, yaliyofanyika nchini Vietnam na kufikia kilele chake usiku wakuamkia leo Jumapili, Septemba 6, 2026.

Mshiriki kutoka Dominican Republic, Joheirry Mola.

Mola alitwaa taji hilo katika fainali ya 73 ya mashindano hayo ya kimataifa, akiwashinda washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani waliokusanyika Vietnam kuwania taji hilo.

Katika nafasi ya pili alimaliza Elisabeth Reynes wa Hispania, huku Taanusiya Chetty wa Malaysia akishika nafasi ya tatu.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na mshindi wa Miss World 2025, Suchata Chuangsri wa Thailand, ambaye alikabidhi taji hilo kwa Mola, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kukabidhi taji kwa mshindi mpya.