Global Publishers September 15, 2026 0 views 0 Comments
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara nchini Hispania na kutembelea klabu ya FC Barcelona, ambako amekutana na Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.
Katika ziara hiyo, Makonda amefanya mazungumzo na viongozi wa Barcelona kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka, kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi pamoja na maandalizi ya Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Mazungumzo hayo pia yameangazia namna uzoefu na mfumo wa soka wa Barcelona unavyoweza kusaidia katika kuimarisha maendeleo ya mchezo wa soka nchini Tanzania.
Aidha, Makonda amemkabidhi Rais wa Barcelona, Joan Laporta, salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, pamoja na kumkabidhi barua ya rambirambi kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.
Makonda pia anatarajiwa kushuhudia mchezo wa FC Barcelona dhidi ya Racing Santander, utakaochezwa Jumatano, Septemba 16, 2026, katika uwanja wa Spotify Camp Nou.
Kwa kifupi: Ziara hiyo inalenga zaidi katika kujenga ushirikiano wa kimichezo kati ya Tanzania na FC Barcelona, hususan katika maendeleo ya vipaji na soka la Tanzania kuelekea AFCON 2027.
Watu wengi hawajui adhabu zinazotolewa na mahakama. Baadhi yao hujua adhabu mbili tu, kufungwa aukunyongwa kulingana na kosa la mtu alilolitenda. Kwa taarifa yako elewa kwamba kuna adhabu saba ambazo mahakama huruhusiwa na sharia kuzitoa, fuatilia hapa:
1. ADHABU YA KIFO (DEATH PENALTY) Adhabu hii hutolewa kwa wenye makosa makubwa kama kuua kwa kukusudia (murder). Kifungu cha 26 Kanuni za Adhabu kinasema kuwa mtu atakapohukumiwa adhabu ya kifo basi adhabu hiyo itatekelezwa kwa kunyongwa kwa kitanzi mpaka mtu huyo atakapokufa.
Baadhi ya nchi adhabu ya kifo hutekelezwa kwa kupigwa risasi na nyingine kudungwa sindano ya sumu. Sisi kwetu ni kitanzi/kamba shingoni kwa kuningâinizwa mpaka roho itoke. Pamoja na hayo, adhabu hii inapingwa sana na mashirika ya haki za binadamu pamoja na wanaharakati wengine duniani kote.
2. ADHABU YA KIFUNGO (IMPRISONMENT) Adhabu ya kifungo hutolewa kwa muda tofauti kutegemea na aina ya kosa alilotenda mtu. Yapo makosa watu hufungwa miaka saba, mwaka mmoja, miezi, mpaka thelathini lakini pia kipo kifungo cha maisha. Kifungo kimegawanyika mara mbili.
Kipo kifungo cha ndani na kipo cha nje. Kifungo cha ndani ni kifungo ambacho mtu anakuwa ndani ya uzio maalum ambao haruhusiwi kutoka huku ukihudumiwa na askari magereza. Hii huitwa jela (jail). Hataruhusiwa kutoka humo mpaka muda maalum uliosemwa na mahakama utakapoisha.
Aidha, kifungu cha nje wakati mwingine huitwa kifungo cha masharti. Ni kifungo ambacho mtuhumiwa hazuiliwi katika jela isipokuwa atapewa masharti kadhaa atakayotakiwa kutekeleza akiwa nje ya jela.
Anaweza kuwa anaishi nyumbani kwake lakini kwa sharti la kuripoti sehemu fulani kila siku au vinginevyo, anaweza kuzuiwa kusafiri nje ya mkoa wilaya au vinginevyo, anaweza kupewa sharti la kutotenda kosa ndani ya mwaka, miaka au vinginevyo n.k. Kubwa hapa ni kuwa kifungo hiki mtu anakuwa nje lakini kwa masharti maalum kama vile kufanya kazi za kijamii kama mahakama itakavyoona.
3. ADHABU YA KUCHAPWA VIBOKO (CORPORAL PUNISHMENT) Hakimu au jaji anaweza, kwa mamlaka aliyonayo, kuamuru mtuhumiwa kuchapwa bakora. Adhabu hii inaweza kutolewa ikiwa kama adhabu inayojitegemea au kama nyongeza baada ya adhabu nyingine. Maana yake ni kuwa unaweza kuhukumiwa kifungo na viboko au viboko pekee na huchapwa na askari wa jeshi la magereza baada ya kupimwa na daktari kuthibitisha afya yake.
4. ADHABU YA FAINI (FINE) Hii nayo inaweza kuwa adhabu inayojitegemea au inayotumika kama adhabu ya nyongeza baada ya kuwa imetolewa adhabu nyingine. Faini huhusisha malipo ya fedha ambayo yatalipwa kwa utaratibu maalum utakaowekwa na Mahakama.
5. ADHABU YA KUNYANGâANYWA MALI (FORFEITURE) Mahakama inaweza kuamuru mali ya mtuhumiwa kunyangâanywa baada ya kupatikana na hatia. Mali kunyangâanywa ni sehemu ya adhabu. Mara nyingi mali zinazonyangâanywa ni zile zilizotumika katika uhalifu. Gari au pikipiki kutumika katika wizi ambao umethibitishwa inaweza kunyangâanywa. Hii ni pamoja na mali nyingine kama nyumba, meli, n.k. Mara nyingi adhabu hii hutolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya au kuzihifadhi majumbani.
6. ADHABU YA KULIPA FIDIA (COMPENSATION) Fidia ni tofauti na faini. Fidia ni kulipia kile ulichoharibu, kupoteza au hasara uliyosababisha. Fidia ni mpaka kiwepo kitu kilichosababisha hasara, upotevu, au uharibifu. Pesa inayolipwa kufidia hasara, uharibifu ndiyo inayoitwa fidia. Aidha, faini hulipwa bila kuhitaji kuwepo kitu kilichoharibika au kusababishiwa hasara.
7. ADHABU YA KUTUNZA AMANI NA KUWA NA TABIA NJEMA (PEACE KEEPING & BE OF GOOD BEHAVIOUR) Mara nyingi adhabu hii hutolewa kwa wenye makosa madogo madogo. Hatutarajii mtu aibe, aue au abake halafu adhabu yake iwe kuhakikisha anatunza amani na kuwa na tabia njema mtaani. Ifahamike kuwa adhabu hii hutekelezwa mtu akiwa nje. Ni sawa na kifungo cha nje kwa sharti la kutunza amani na kuwa mtu mwema mtaani. Endapo mtu huyu atatenda kosa jingine katika kipindi hiki cha uangalizi basi atapewa adhabu nyingine kubwa zaidi.
Matthew Rhys ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika tamthilia ya vichekesho.
LOS ANGELES â Tamasha la 78 la Tuzo za Emmy limefanyika Jumatatu, Septemba 14, 2026, katika ukumbi wa Peacock Theater mjini Los Angeles, huku vipindi vya televisheni âWidowâs Bayâ na âThe Pittâ vikiwa miongoni mwa vilivyoibuka na ushindi mkubwa.
Sherehe hizo ziliongozwa na mwigizaji Mariska Hargitay na kurushwa moja kwa moja kupitia NBC na Peacock, zikihudhuriwa na baadhi ya majina makubwa katika tasnia ya televisheni.
âWidowâs Bayâ ilitwaa tuzo ya Outstanding Comedy Series, huku Matthew Rhys akishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika tamthilia ya vichekesho. Stephen Root naye alishinda tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kiume, huku Kate OâFlynn akitwaa tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kike.
Kipindi hicho pia kilishinda tuzo za uandishi bora na uongozi bora (directing) katika kitengo cha comedy, na kukifanya kuwa miongoni mwa washindi wakubwa wa usiku huo.
Kwa upande mwingine, âThe Pittâ ilitwaa tuzo ya juu ya Outstanding Drama Series. Noah Wyle alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika drama kwa nafasi yake katika kipindi hicho.
âThe Pittâ pia ilipata uteuzi kadhaa katika vitengo vya waigizaji wasaidizi, huku ushindani mkubwa ukiwa miongoni mwa waigizaji wake.
Katika tuzo nyingine za drama, Rhea Seehorn alishinda Outstanding Lead Actress in a Drama Series kwa âPluribusâ, wakati Tom Pelphrey alitwaa tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kiume kwa âTaskâ. Allison Janney naye alishinda tuzo ya mwigizaji msaidizi bora wa kike kwa âThe Diplomatâ.
Rhea Seehorn ameshinda Outstanding Lead Actress in a Drama Series kwa âPluribus
Vince Gilligan alipewa tuzo ya uandishi bora wa drama kwa kipindi cha âPluribusâ, huku Saul Metzstein akishinda tuzo ya directing bora kwa âSlow Horsesâ.
Katika kitengo cha tamthilia maalum, âDTF St. Louisâ ilitwaa tuzo ya Outstanding Limited or Anthology Series. Matthew Rhys aliongeza ushindi mwingine kwa kutwaa tuzo ya mwigizaji bora wa kiume katika limited series au movie kwa âThe Beast in Meâ.
Sally Field naye alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike katika kitengo hicho kwa âRemarkably Bright Creaturesâ.
Kwa upande wa vipindi vya mashindano ya uhalisia, âThe Traitorsâ ilitwaa tuzo ya Outstanding Reality Competition Program, ikiwashinda âDancing with the Starsâ, âRuPaulâs Drag Raceâ, âSurvivorâ na âTop Chefâ.
Sally Field naye ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike katika kitengo hicho kwa âRemarkably Bright Creaturesâ.
Katika kitengo cha variety series, âThe Late Show with Stephen Colbertâ iliibuka mshindi, ikishinda programu zilizokuwa zikichuana nazo kama âThe Daily Showâ, âJimmy Kimmel Live!â, âLast Week Tonight with John Oliverâ na âSaturday Night Liveâ.
Tuzo hizo za Emmy za mwaka huu zilifuatia Creative Arts Emmys zilizotolewa Septemba 5 na 6, ambapo washindi wengine akiwemo Shailene Woodley, David Harbour, Linda Cardellini, Betty Gilpin na marehemu Rob Reiner walitambuliwa.
Mariska Hargitay, ambaye alikuwa mwenyeji wa sherehe kuu za mwaka huu, pia alikuwa miongoni mwa washindi baada ya kutwaa tuzo mbili za Emmy kwa filamu yake ya maandishi âMy Mom Jayneâ.
Kwa ujumla, usiku wa Emmy 2026 uliendelea kuonyesha ushindani mkubwa katika televisheni, huku âWidowâs Bayâ ikitawala upande wa comedy na âThe Pittâ ikifanya vizuri katika upande wa drama.
Outstanding Comedy Series
Abbott Elementary The Bear Hacks Margoâs Got Money Troubles Nobody Wants This Only Murders in the Building Shrinking Widowâs Bay â WINNER
Outstanding Lead Actor in a Comedy Series
Yahya Abdul-Mateen II â Wonder Man Steve Carell â Rooster Matthew Rhys â Widowâs Bay â WINNER Jason Segel â Shrinking Martin Short â Only Murders in the Building
Outstanding Lead Actress in a Comedy Series
Quinta Brunson â Abbott Elementary Ayo Edebiri â The Bear Elle Fanning â Margoâs Got Money Troubles Lisa Kudrow â The Comeback Jean Smart â Hacks â WINNER
Outstanding Supporting Actor in a Comedy Series
Colman Domingo â The Four Seasons Paul W. Downs â Hacks Harrison Ford â Shrinking Nick Offerman â Margoâs Got Money Troubles Stephen Root â Widowâs Bay â WINNER Michael Urie â Shrinking Tyler James Williams â Abbott Elementary
Outstanding Supporting Actress in a Comedy Series
Dale Dickey â Widowâs Bay Hannah Einbinder â Hacks Janelle James â Abbott Elementary Kate OâFlynn â Widowâs Bay â WINNER Michelle Pfeiffer â Margoâs Got Money Troubles Megan Stalter â Hacks Jessica Williams â Shrinking
Outstanding Writing for a Comedy Series
Abbott Elementary, âTeam Buildingâ â Quinta Brunson The Chair Company, âLife Goes by Too F**king Fast, It Really Doesâ â Tim Robinson, Zach Kanin The Comeback, âValerie Does It Allâ â Michael Patrick King, Lisa Kudrow Hacks, âHacks (Finale)â â Lucia Aniello, Paul W. Downs, Jen Statsky Jury Duty Presents: Company Retreat, âMergers and Acquisitionsâ â Anthony King Widowâs Bay, âWelcome to Widowâs Bay!â â Katie Dippold â WINNER
Outstanding Directing for a Comedy Series
Abbott Elementary, âBallgameâ â Randall Einhorn The Bear, âBearsâ â Christopher Storer The Chair Company, âLife Goes by Too F**king Fast, It Really Does.â â Andrew DeYoung Hacks, âHacks (Finale)â â Lucia Aniello The Ms. Pat Show, âGive It Arrestâ â Mary Lou Belli Widowâs Bay, âWelcome to Widowâs Bay!â â Hiro Murai â WINNER
Outstanding Lead Actor in a Drama Series
Sterling K. Brown â Paradise Gary Oldman â Slow Horses Mark Ruffalo â Task Rufus Sewell â The Diplomat Noah Wyle â The Pitt â WINNER
Outstanding Lead Actress in a Drama Series
Carrie Coon â The Gilded Age Chase Infiniti â The Testaments Keri Russell â The Diplomat Rhea Seehorn â Pluribus â WINNER Zendaya â Euphoria
Outstanding Supporting Actor in a Drama Series
Patrick Ball â The Pitt Billy Crudup â The Morning Show Shawn Hatosy â The Pitt Gerran Howell â The Pitt Jack Lowden â Slow Horses Tom Pelphrey â Task â WINNER Carlos-Manuel Vesga â Pluribus
Outstanding Supporting Actress in a Drama Series
Taylor Dearden â The Pitt Fiona Dourif â The Pitt Allison Janney â The Diplomat â WINNER Katherine LaNasa â The Pitt Sepideh Moafi â The Pitt Julianne Nicholson â Paradise Karolina Wydra â Pluribus
Outstanding Writing for a Drama Series
The Diplomat, âAmagansettâ â Peter Ackerman, Debora Cahn The Pitt, â1:00 P.M.â â Kirsten Pierre-Geyfman, R. Scott Gemmill The Pitt, â12:00 P.M.â â Valerie Chu Pluribus, âWe Is Usâ â Vince Gilligan â WINNER Slow Horses, âScarsâ â Will Smith Task, âA Still Small Voiceâ â Brad Ingelsby
Outstanding Directing for a Drama Series
The Gilded Age, âMy Mind Is Made Upâ â Salli Richardson Whitfield Paradise, âExodusâ â Hanelle M. Culpepper The Pitt, â12:00 P.M.â â Noah Wyle Pluribus, âWe Is Usâ â Vince Gilligan Slow Horses, âScarsâ â Saul Metzstein â WINNER Task, âOut Beyond Ideas of Wrongdoing and Rightdoing, There Is a River.â â Salli Richardson Whitfield
Outstanding Limited or Anthology Series
All Her Fault The Beast in Me Beef DTF St. Louis â WINNER Love Story: John F. Kennedy Jr. and Carolyn Bessette
Outstanding Lead Actor in a Limited or Anthology Series or Movie
Riz Ahmed â Bait Jason Bateman â Black Rabbit Charlie Hunnam â Monster: The Ed Gein Story Oscar Isaac â Beef Matthew Rhys â The Beast in Me â WINNER
Outstanding Lead Actress in a Limited or Anthology Series or Movie
Claire Danes â The Beast in Me Sally Field â Remarkably Bright Creatures â WINNER Carey Mulligan â Beef Sarah Pidgeon â Love Story: John F. Kennedy Jr. & Carolyn Bessette Sarah Snook â All Her Fault
Outstanding Reality Competition Program
Dancing with the Stars RuPaulâs Drag Race Survivor Top Chef The Traitors â WINNER
Outstanding Variety Series
The Daily Show Jimmy Kimmel Live! Last Week Tonight with John Oliver The Late Show with Stephen Colbert â WINNER Saturday Night Live
MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWAÂ
 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIAÂ
2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMÂ
3:TUZO YA AFYA
Â
4:TUZO YA MPIGA PICHAÂ
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .
MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWAÂ
 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)
1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIAÂ
2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMÂ
3:TUZO YA AFYA
Â
4:TUZO YA MPIGA PICHAÂ
AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .
Global Publishers September 15, 2026 36 views 0 Comments
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limethibitisha kifo cha mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35, baada ya kupigwa risasi alipokuwa akijaribu kutekeleza uhalifu katika Benki ya CRDB, Tawi la Rock City Mall, Wilaya ya Ilemela.
Tukio hilo lilitokea Septemba 13, 2026 majira ya saa 7:58 mchana, ambapo mwanaume huyo alifika benki akiwa amevalia kofia, shati la mikono mirefu, suruali ya jeans na viatu vya wazi.
Awali, alimuomba mhudumu fedha akidai anahitaji fedha za kula. Baada ya kukataliwa, aliingia katika eneo la kaunta na kuelekea kwenye sehemu ya kuhifadhi fedha, hali iliyosababisha taharuki kwa wafanyakazi na wateja.
Askari waliokuwa wakilinda benki walifika na kumtaka ajisalimishe, lakini alikaidi amri na kuanza kukabiliana na askari, akijaribu pia kuwanyangâanya silaha. Katika hatua hiyo, askari walimpiga risasi kwenye mguu wa kulia ili kumdhibiti.
Alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Sekou-Toure kwa matibabu, lakini alifariki akiwa hospitalini.
Mwili wake umehifadhiwa hospitalini kwa ajili ya utambuzi na hatua nyingine za uchunguzi. Polisi pia walimkuta na simu aina ya Samsung pamoja na Shilingi 500. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Moshi, Kilimanjaro â Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limeanzisha uchunguzi wa tukio la mauaji ya kijana Steven Karakira Kaaya (24), mkazi wa Mtaa wa Boma Mbuzi, Wilaya ya Moshi, ambaye alifariki baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa kitu cha plastiki.
Tukio hilo lilitokea Septemba 13, 2026, majira ya saa 11:00 jioni, katika eneo la Mtaa wa Spencorn, Kata ya Bomambuzi, Wilaya ya Moshi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, wakati wa tukio hilo kijana huyo alishambuliwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia kitu butu na watu ambao majina yao hayajajulikana. Alidaiwa kuhusishwa na tabia ya kuchunguza vitu vya watu mbalimbali kwa nia ya kuiba.
Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa mahojiano zaidi huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini na kuwakamata watu wengine waliohusika na tukio hilo.
Aidha, baada ya tukio la mauaji kutokea, baadhi ya wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa mali, ikiwemo kuchoma moto gari aina ya Mitsubishi Canta, yenye namba za usajili T.119 ATV, linalodaiwa kuwa la mmoja wa watu waliotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Vilevile, baadhi ya mali zilizokuwa ndani ya chumba cha duka linalomilikiwa na Thelesia Omary Nyambuleki Mwikoma ziliripotiwa kuharibiwa katika vurugu hizo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Jeshi hilo pia limeeleza kuwa chanzo na mazingira halisi ya tukio bado vinaendelea kuchunguzwa kwa kushirikiana na taasisi na mamlaka nyingine. Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na mauaji, vurugu na uharibifu wa mali.
Global Publishers September 15, 2026 6 views 0 Comments
Mfanyabiashara maarufu nchini, Jennifer Bilikwija, anayefahamika zaidi kwa jina la Niffer, amezungumzia suala la mahusiano na namna ambavyo mtu anaweza kukabiliana na hali ya kuchezewa na mwenza wake.
Niffer amesema kuwa kuchezewa katika mahusiano huku mtu akiwa anafahamu kinachoendelea kunaweza kuwa tofauti na pale ambapo anasalitiwa bila kutarajia.
âKuchezewa kwenye mahusiano huku unajua unachezewa hakuumi, ila ukichezewa bila kutarajia unaweza kufa,â amesema Niffer.
Katika kauli yake, Niffer amesisitiza umuhimu wa mtu kuwa makini na kutambua hali halisi ya uhusiano wake, badala ya kuishi bila kujua kinachoendelea nyuma yake.
âJifunze kujua mwenyewe kama unachezewa ili ujue namna ya kucheza,â ameongeza.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni mtazamo wa Niffer kuhusu namna watu wanavyopaswa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika mahusiano, huku akisisitiza umuhimu wa kutambua mapema mwenendo wa mwenza.
Ujumbe wake umeibua mjadala kuhusu uaminifu katika mahusiano na namna ambavyo mtu anavyoweza kuathirika pale anapogundua usaliti ambao hakutarajia.
Maji ya limao ni kinywaji rahisi kinachotengenezwa kwa kuchanganya maji na juisi ya limao mbichi. Kunywa maji ya limao kila siku kunaweza kusaidia kuboresha afya kwa ujumla kwa kutoa virutubisho muhimu, kuimarisha kinga ya mwili na kusaidia kazi mbalimbali za mwili.
Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Healthline, glasi ya juisi iliyokamuliwa kutoka gramu 48 za limao ina takribani kalori 10.6 na virutubisho vifuatavyo:
Vitamini C husaidia kuimarisha kinga ya mwili na kulinda mwili dhidi ya magonjwa.
Kuchanganya juisi ya limao na maji ni njia rahisi na yenye afya ya kudumisha unyevunyevu mwilini. Maji ya limao pia yana faida nyingi kiafya kutokana na virutubisho vyao.
1. Huongeza Kiasi cha Vitamini C
Limao lina vitamini C nyingi, antioxidant inayolinda seli dhidi ya free radicals zinazoweza kusababisha uvimbe na magonjwa mbalimbali. Vitamini C pia husaidia:
Uzalishaji wa collagen na L-carnitine
Metabolism ya protini
Urejeshaji wa antioxidants
Usogeaji wa chuma mwilini
Uzalishaji wa homoni
Kupunguza hatari ya baadhi ya saratani na magonjwa ya moyo
Ukikosa vitamini C mwilini unaweza kupata: kuongezeka kwa hatari ya maambukizi, ngozi kavu, macho kavu, kinywa kavu, uchovu, usingizi mdogo, na upotevu wa meno.
2. Husaidia Kupunguza Uzito
Kunywa maji ya limao kunasaidia kuongeza unywaji wa maji kwa ujumla, kuchochea hisia ya utoshelevu, na kuongeza kiwango cha metabolism. Maji ya limao ni yenye kalori chache, rahisi kutengeneza, na yanaweza kuchukua nafasi ya vinywaji vyenye kalori nyingi, hivyo kusaidia kudhibiti uzito.
3. Badilisha Vinywaji Vyenye Sukari
Maji ya limao ni mbadala wa asili na wenye afya kwa vinywaji vyenye sukari. Kunywa vinywaji vyenye sukari mara kwa mara husababisha kuongezeka kwa uzito, unene wa kupita kiasi, kisukari aina ya 2, magonjwa ya moyo, figo, ini, kuoza kwa meno, na gout.
4. Kuzuia Mawe ya Figo
Asidi ya citric iliyopo kwenye maji ya limao inaweza kusaidia kuzuia mawe ya figo kwa kuongeza kiwango cha mkojo na kuongeza pH, hali inayofanya mazingira ya figo kuwa yasiyofaa kwa uundaji wa mawe. Watu waliokuwa na mawe ya figo wanaweza kuchanganya ml 113 ya juisi ya limao na maji pamoja na dawa zao ili kuzuia kurudiwa kwa mawe. Citrate, sehemu ya asidi ya citric, inaweza kupunguza asidi ya mkojo na kusaidia kuvunja mawe madogo.
5. Kusaidia Utumbo na Usagaji Chakula
Kunywa maji ya limao kabla ya mlo kunaweza kuboresha usagaji chakula. Asidi ya citric inachochea uzalishaji wa asidi tumboni, ambayo husaidia kuvunja chakula. Watu wenye matatizo ya tumbo wanapaswa kuwa makini kunywa maji ya limao kwa tumbo tupu.
Jinsi ya Kutengeneza Maji ya Limao
Kamulia nusu limao ndani ya ml 230 ya maji ya moto au baridi.
Maji ya limao yanaweza kunywewa kama yalivyo au kuongeza: majani ya mint, kijiko kimoja cha syrup ya maple au asali safi, kipande cha tangawizi au tango, tone la mdalasini, au kiasi kidogo cha manjano (turmeric).
Anza asubuhi yako kwa glasi ya maji ya limao ya moto na weka chupa tayari kwenye friji ili kunywa kidogo kidogo siku nzima.
Kupunguza Madhara ya Maji ya Limao
Maji ya limao kwa kawaida ni salama, lakini asidi yake inaweza kuharibu enamel ya meno kwa muda. Ili kupunguza hatari:
Familia ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeibua mjadala mwingine katika kesi hiyo ya uhaini inayokabili baada ya wakili Nassoro Katuga kumuuliza shahidi John Heche kuhusu uraia wa baadhi ya wanafamilia wa Mwenyekiti huyo, huku Heche akisema hajui kama watoto na mke wa Lissu si raia wa Tanzania.
Katika mahojiano ya kuhojiwa na Nassoro Katuga, Heche alikiri kuwa hajui iwapo watoto wa Lissu, ambaye amekuwa akimtaja kama mzalendo, ni raia wa Tanzania, licha ya kukubali kuwa Tanzania haina uraia wa nchi mbili.
Katuga alimuuliza Heche kama anafahamu kuwa Mwenyekiti anayemtaja kuwa mzalendo ana watoto ambao si raia wa Tanzania, ambapo Heche alijibu kuwa jambo hilo halijui. Alipoulizwa kuhusu mke wa Mwenyekiti huyo, Heche pia alisema hajui kuhusu uraia wake, akisisitiza kuwa anachojua ni kwamba ni Mkurya.
Katika sehemu nyingine ya ushahidi wake, Heche alieleza kuhusu kifo cha mdogo wake, Suguta Heche, akisema yeye mwenyewe hakuwapo wakati mdogo wake alipokuwa akiteswa na kuchomwa kwa singe, bali taarifa hizo alizipata kutoka kwa RPC.
Katuga alitaka kufahamu iwapo Heche alishuhudia tukio hilo moja kwa moja, lakini Heche alisisitiza kuwa taarifa hizo zilitolewa na RPC. Vilevile, alipoulizwa sehemu ya mwili ambayo Suguta alichomwa kwa singe, Heche alisema hakueleza Mahakamani.
Heche pia alikiri kuwa hakuwapo eneo ambalo polisi walidaiwa kutaka kumtupa mdogo wake, akisema taarifa hiyo aliipata kutoka kwa RPC. Aidha, alikiri kuwa mtu anayemtuhumu kwa kumuua mdogo wake hakumtaja jina Mahakamani.
Katika mahojiano hayo, Katuga alitaka kujua kama mtu huyo aliwahi kumweleza Heche kwamba alimuua Suguta kwa lengo la kumtisha ili asiendelee na shughuli zake za kisiasa.
Heche alijibu kuwa mtuhumiwa huyo hakuwahi kumweleza hivyo. Hata hivyo, alirejea kauli ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli, kwamba mpaka mwaka 2020 upinzani ungekuwa umeisha.
Alipoulizwa kama sababu ya mauaji hayo ilikuwa ni kumkomoa yeye kisiasa, Heche alisema, âMimi najua ni mimi,â huku akikiri kuwa hakuwahi kuambiwa moja kwa moja na mtuhumiwa kwamba alimuua mdogo wake kwa sababu hiyo.