POLISI WADAIWA KUMUUA KWA RISASI MTUHUMIWA WA UHALIFU ALIYEWATEKA MWANAMKE NA MTOTO WAKE

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo akikagua nyumba ambayo mtuhumiwa alijificha baada ya kuwaona polisi

Baba wa mtuhumiwa aliyeuawa

Na Matukio Daima Media, Kilosa

TUKIO la kutekwa kwa mwanamke na mtoto wake katika Kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro limeishia kwa kifo cha Kokan State (30), baada ya mwanaume huyo kudhibitiwa kwa risasi na polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, Kokan alikuwa akitafutwa kwa tuhuma zinazohusisha mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia silaha.

Kantimbo akasema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na  polisi kwa muda mrefu ambapo baada ya kubaini alipo na kumfuata, alimshika mwanamke aliyekuwa alimhudumia kinywaji pamoja na mtoto wake mdogo na kujifungia nao katika chumba, akiwatumia kama kinga dhidi ya polisi.

Alisema Kokan alitishia kuwaua Mama na mtoto huyo kwa sime iwapo polisi wangejaribu kumkamata, hali iliyosababisha askari kutumia silaha na kumuua baada ya jitihada zote za kutaka ajisalimishe kushindikana.

Mwanamke na mtoto waliotumiwa kama Kinga na mtuhumiwa wa uhalifu

Mwanamke huyo aliyetekwa, mkazi wa Kijiji cha Parakuyo, Rehema Masuke, amesema tukio hilo liliwapa hali ya hofu wakiamini huenda wangeuawa kwa sime aliyokuwa nayo kijana huyo.

Kwa upande wake Baba mzazi wa Kokan amesema kwa muda mrefu alikuwa akimkanya mwanawe kuacha kujihusisha na Matukio ya ki uhalifu, lakini licha ya ushauri huo, alihusishwa mara kadhaa na matukio hayo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Parakuyo, Emmanuel Kibasisi, amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama na kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na uhalifu.

Polisi mkoani Morogoro wameendelea kutoa wito kwa vijana kujiepusha na uhalifu na kutafuta kipato kupitia shughuli halali.

Mwisho

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .