Global Publishers
September 28, 2026
0 views
0 Comments

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya pamoja na kufanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi za Kurugenzi zake.
Mabadiliko hayo yametangazwa leo, Septemba 28, 2026, kupitia kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam chini ya Rais wa TFF, Wallace Karia.
Katika uteuzi huo, Evans Mgeusa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa TFF, akichukua nafasi ya Oscar Mirambo, ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Kabla ya uteuzi huo, Mgeusa alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NIOREFA).
Kwa upande wake, Oscar Mirambo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, huku Mustapha Yusuph akiteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha.
Aidha, TFF imefanya mabadiliko katika Kurugenzi ya Sheria, Habari na Masoko, pamoja na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano.
Waliopewa majukumu ya kuongoza Kurugenzi hizo ni:
- Hassan Njama – Mkurugenzi wa Biashara na Masoko
- Boniface Wambura – Mkurugenzi wa Sheria
- Cliford Ndimbo – Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano
TFF imesema mabadiliko hayo yamefanyika kupitia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

