Global Publishers
September 28, 2026
0 views
0 Comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amewasili mkoani Arusha leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, kwa ajili ya kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum).
Makamu wa Rais amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Baada ya kuwasili Arusha, Ndejembi anatarajiwa kuelekea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo atafungua rasmi kikao hicho kinachowakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma.
C-CEOs Forum inalenga kuwa jukwaa la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji, utendaji na mchango wa Taasisi na Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa.


