Global Publishers
September 27, 2026
12 views
0 Comments

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya kiutendaji katika ngazi ya Makatibu wa CCM wa mikoa, kwa kuteua Kaimu Makatibu 32 wa mikoa yake yote ya kichama, ambao wanaanza kazi mara moja.
Taarifa hiyo imetolewa Septemba 27, 2026, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Labani Kihongosi. Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa mabadiliko hayo yanafuatia uteuzi wa viongozi wapya watakaosimamia shughuli za chama katika mikoa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, ameandaa semina elekezi ya siku mbili kwa Kaimu Makatibu hao, itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 29 hadi 30, 2026.
Semina hiyo inalenga kuwaandaa viongozi hao kwa majukumu yao ya kiutendaji, huku orodha kamili ya walioteuliwa ikiwa kwenye kurasa zinazofuata za taarifa hiyo.
CCM pia imewapongeza na kuwashukuru Makatibu wa Mikoa waliomaliza muda wao kwa utumishi na mchango wao ndani ya chama, ikieleza kuwa itaendelea kutumia uzoefu na uwezo wao kama sehemu ya hazina ya viongozi na watendaji wake.
Orodha ya Kaimu Makatibu wa CCM wa Mikoa
- Arusha — Pilly John Jackson
- Dar es Salaam — Stanley Wilson Mkandawire
- Dodoma — Pili Augustine Mbanga
- Geita — Ramadhani Kapeto
- Iringa — James Dan Mgego
- Kagera — Rukia Said Mkindu
- Kaskazini Pemba — Salum Khamis Haji
- Kaskazini Unguja — Haji Machano Juma
- Katavi — Hawa Siri Makonyola
- Kigoma — Halid Said Mwinyi
- Kilimanjaro — Julius Nansongelya Peter
- Kusini Pemba — Bilal Hussein Maulid
- Kusini Unguja — Himid Lussan Tweve
- Lindi — Zuwena Suleiman Mohamed
- Mkoa wa Magharibi — Alawi Haidar Foum
- Mkoa wa Mjini — Yusuph Mabena
- Manyara — Eva Michael Degeleki
- Mara — Godfrey R. Kavenga
- Mbeya — Ramadhani Samwel Mahanyu
- Morogoro — Joseph Robert Mwega
- Mtwara — Ahmada Shaha Vuai
- Mwanza — Mwanamasudi Msafiri Pazi
- Njombe — Waridi Josephat Mgumi
- Pwani — Abdul-Rahim Hamad (Dogo)
- Rukwa — Rehema Nzunye Ndele
- Ruvuma — Mohammed Ali Khalfan
- Shinyanga — Sophia Abdallah Kibaba
- Simiyu — Kajoro Peter Vyohoroka
- Singida — Jonathan Mabihya
- Songwe — Aziza Juma Isimbula
- Tabora — Salum Suleiman Tate
- Tanga — Twalib K. Berege

