Global Publishers
September 25, 2026
12 views
0 Comments
ROME, ITALIA — Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametembelea Vatican City jijini Roma, Italia, katika ziara ya kando ya ushiriki wake kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo.
Mkutano huo ulifanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma.
Akiwa Vatican City Alhamisi, Septemba 24, Dkt. Mwigulu alikutana na Mkuu wa Itifaki wa Sekretarieti ya Nchi ya Vatican, Monsinyori Javier Domingo Fernández González, katika ziara iliyompa fursa ya kutembelea pia maeneo mbalimbali ya Vatican.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alitembelea maeneo ya kihistoria na kiutamaduni ya Vatican City, ambayo yana nafasi muhimu katika historia ya Kanisa Katoliki na urithi wa dunia.
Ziara hiyo imefanyika wakati Dkt. Mwigulu akiwa Roma kwa ajili ya kushiriki katika mjadala wa kimataifa unaohusu Afya Moja, chakula na mifumo ya kilimo, masuala yanayohusisha afya ya binadamu, wanyama na mazingira.
Vatican City ni makao makuu ya Kanisa Katoliki na ni eneo lenye taasisi mbalimbali za kihistoria na kidini.


