Global Publishers
September 24, 2026
12 views
0 Comments

Mwandaaji wa shindano la Miss Grand Tanzania alitenda kosa la kuendesha shindano husika bila kuwa na KIBALI CHA TUKIO kutoka BASATA Kinyume na Kanuni na taratibu za uendeshaji wa matukio ya Sanaa hapa nchini. Alipewa Notisi ya kosa hilo tarehe 12/08/2026 na kutakiwa kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku 21 na hakutekeleza, Kwa mujibu wa Kanuni ya 45 ya Kanuni za Baraza, imeamuliwa:-
• Kulipa faini ya Shilingi Milioni Tatu (Tsh 3,000,000/=) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
• Kutokujishughulisha na kazi za Sanaa kuanzia tarehe ya uamuzi huu hadi atakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa.

