
Katika kuendelea kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Tundu Lissu, shahidi John Heche amekabiliwa na maswali makali kutoka kwa Wakili Katuga kuhusu kauli mbalimbali alizowahi kutoa kuhusu mauaji ya Alphonce Mawazo, Akwilina Akwilina na Msafiri Mbwambo, pamoja na matukio mengine ya kisiasa nchini.
Katika mahojiano hayo, Katuga alimuuliza Heche iwapo ana imani na Mahakama, ambapo Heche alisema anaamini Mahakama, huku akieleza kuwa hawezi kusema kwa kiwango gani ana imani nayo kwa kuwa kesi bado haijaamuliwa.
Wakili Katuga pia alimuuliza Heche kuhusu kauli alizowahi kutoa hadharani kuhusu kesi hiyo, akimtaka kukumbuka baadhi ya hotuba na video zilizopo mtandaoni. Heche alipoonyeshwa baadhi ya video, alihoji matumizi ya teknolojia ya AI, huku akisema baadhi ya sauti alizozisikia zilifanana na yake.
Katika sehemu nyingine ya mahojiano, Katuga alimuuliza Heche kuhusu kifo cha Msafiri Mbwambo, ambaye shahidi alidai aliuawa kwa sababu za kisiasa na zinazohusiana na uchaguzi. Heche alieleza kuwa taarifa hizo alizipata kupitia mijadala mbalimbali, ikiwemo Bungeni na vyombo vya habari.
Heche pia aliulizwa kuhusu mauaji ya Alphonce Mawazo, ambapo alisema alifahamu kuwa kifo chake kilihusishwa na uchaguzi kwa sababu Mawazo alikuwa kwenye kampeni. Hata hivyo, alipoulizwa chanzo cha taarifa hizo, Heche alisema suala hilo lilijadiliwa katika maeneo mbalimbali na kuandikwa na vyombo vya habari.
Kuhusu mauaji ya Akwilina Akwilina mwaka 2018, Katuga alimuuliza Heche kuhusu tukio hilo lililotokea wakati wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni. Heche alithibitisha kuwa siku hiyo CHADEMA ilikuwa ikihitimisha kampeni.
Katuga pia alimuuliza iwapo baada ya mkutano kulikuwa na kundi la watu lililoelekea Magomeni na kutawanywa na polisi. Heche alikiri kuwa kulikuwa na kundi hilo na kwamba polisi waliwataka watawanyike.
Katika hatua nyingine, Katuga alimuuliza Heche kuhusu madai ya kuwepo kwa kesi dhidi ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA zinazohusiana na madai ya kutekwa kwa watu, akiwemo Bariki na Paul Mafie. Heche alisema hafahamu kuhusu suala hilo.
Mahojiano hayo yamejikita zaidi katika chanzo na msingi wa taarifa ambazo Heche amezitoa mahakamani, huku upande wa mashtaka ukitaka kubaini kama baadhi ya madai yake yanatokana na ushahidi aliouona mwenyewe au taarifa alizosoma na kusikia kutoka kwa vyanzo vingine.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mahakamani.
Katuga: Unajua ama hujui Tanzania ni nchi huru
Katuga Unajua hujui kwa mujibu wa Katiba ya 77 Mahakama ndio chombo kinachotoa haki
Katuga: Unajua Mahakama haitakiwi kuingiliwa
Katuga: Unaimani na hii Mahakama
Heche: Kesi haijaamulIwa siwezi sema nina imani
Katuga: Waambie Majaji unaiaminini huiamini
Katuga: Je ni sahihi kisheria mtu anayekuja kuwa shahidi akamapima dimina ya majaji
Katuga: Waambie majaji kama uko hapa baada ya Lissu kuonekakana na kesi ya kujibu
Katuga: Unajua kwamba ushahidi wa kielectromic ni sawa na document
Katuga: Waambie majaji kama hotuba zako nyingi ziko mtandaoni
Katuga: Waambie majaji kama uliwahi kuongelea kesi hii baada ya mshitakiwa kupatikana na kesi ya kujibu
Katuga: Waambie majaji kama ulisema dimina ya jaji haiko sawa hata ukimuangalia
Katuga: Uko tayari tukusikilizishe
Heche: Sikuamini kuna AI siku hizi
Katuga: Waheshimiwa Majaji naomba tumuoneshe fresh memory ili atusaidie kujibu baada ya maswali
Lissu: Huu utaratibu sijaelewa uko kwa sheria gani
Jaji: Utamfanyia re-examination
Heche: Siwezi kuamini kompyuta ni Katuga zama hizi za AI waheshimiwa majaji
Jaji: Wewe sikiliza kisha utafafanua
Katuga: Hii hotuba unaikumbuka
Heche: Kwa mbaali sauti kama ni yangu
Katuga: Unaikumbuka huiumbuki
Katuga: Unakumbuka ulisema shahidi wa 17 yeye ndio amepublish
Katuga: Je hilo swala shahidi ya 17 limezungumziwa hapo kwenye video
Heche: Hiyo video sio yangu
Katuga: Walau jibu kidogo hayo maneno P17 alisema ndiye alipublish yanafanana ya ushahdi wako hayafanani
Heche: Nimeyasikia yanafanana kwenye hiyo AI yako
Katuga: Kuthibitisha na ku-establish premafasheee kesi nini maana yake
Katuga: Waambie majaji kama uliridhika Mahakama Ilipoamua Lissu anakesi ya kujibu uliridhika au hukuridhika
Katuga: Uliwahi kuita press kuwasema mashahidi waongo hapo nje
Katuga: Tukikuonesha tena utakubali au utaita AI
Heche: Siwezi kukataa kama ni kitu cha kweli
Katuga: Lissu anachombo cha habari
Katuga: Lissu akitaka kupeleka ujumbe kwa uma anatumia njia gani
Katuga: Mh Lissu akitaka kupeleka ujumbe kwa watanzania wote anatumia vyombo vya habari
Heche: Anahutubia mikutano
Katuga: Kwenye ushahdi wako ulisema mapolisi walikuwa wanaingiza kura feki kwenye vibegi vyao embu waambie majaji kama uliwahi kumkamata
Heche: Niliwahi kuona askari shule ya Msingi Nyanungu
Katuga: Ulileta huo ushahidi hapa mahakamani
Katuga: Na unataka Mahakama ikuamini
Katuga: Unajua watu wanatuhuma za mauaji kwa sababu mbali mbali
Katuga: Katika ushahiri wako umeiambia Mahakama hii Msafiri Mbwambo alichinjwa kwa kulalamikia sheria za uchaguzi
Heche: Aliuawa sababu ya siasa
Katuga: Uliwaambia majaji ameuawa sababu ya moja mbili tatu
Heche: Nilisema sababu ya sababu za kisiasa
Katuga: Umeeleza ile sababu ya msingi, waambie majaji kama umeelezea sababu yake ya kuchinjwa
Heche: Nilieleza sababu za kiuchaguzi
Katuga: Unajua au hujui kuna kesi kwa viongozi wa CHADEMA iko Arusha ya kuteka mtu anaitwa Bariki na Paul Mafie na kuwapandisha mlimani kwa nia ya kuwatesa na kuwatishia unajua au hujui
Katuga: Unajua mtu yoyote anaweza kushitakiwa kwa jinai
Katuga: Unajua kusadikika ni hisia
Katuga: Ushahadi wako Katibu wenu aliuawa na watu wanaosadikika ni wa CCM
Heche: Nilisema sababu za kiuchaguzi
Katuga: Nani anafuatilia viapo vya mawakala Chadema
Heche: Kila eneo linafuatiliaji wake, mgombea, kiongozi wa chama kulingana na eneo husika
Katuga: Mwaka 2018 wakati wa kampeni za Jimbo la Kinondoni, alikuwa mgombea ni nani
Katuga: Ni kweli kwamba siku Akwilina ameuawa mlikuwa mnafunga kampeni
Katuga: Waambie majaji kama sio kweli jioni baada ya mkutano ilitoka hamasa ya kwenda kwa Mkurugenzi kwa maandamano
Katuga: Waambie majaji kama uliwaambia majaji mlikuwa watu wa ngapi mkifuata kwenda Magomeni
Katuga: Ni kweli kwamba mlikuwa Kundi, ikabidi polisi wa wawatawanye
Katuga: Wakati mnashitakiwa 2018 ulisema Mwenyekiti alikuwa ameshambuliwa
Heche: Nilisema Mwenyekiti wetu wa sasa
Katuga: Ulisema angekuwa ameshambuliwa kwa risasi tungekuwa naye huu ni ushahidi wa aina gani ni ku- assune, kuona au kusikikiii
Katuga: Ulijua muaji wa Alphonce Mawazo
Katuga: Waambie Mahakama kama ulijua sababu
Katuga: Sasa ulijuaje hizo sababu
Heche: Sababu ya uchaguzi alikuwa kwenye kampeni
Katuga: Mtu mwenye ugomvi na Mawazo anaruhusiwa kuua wakati wa uchaguzi
Heche: Sheria inakuzuia wakati wote
Katuga: Kwa hiyo huu ushahidi wa Mawazo ni wako au wa kusoma
Heche: NIlisoma na iljadiliwa Bungeni
Katuga: Unaawaambia Majaji ushahidi wako ni sababu za Bungeni
Heche: Ni ushahidi wangu ni sababu za uchaguzi
Katuga: Waambie majaji hizo sababu za hayo mauaji umetoa wapi
Heche: Ilijadiliwa kila mahali na hata kuandikwa kwenye vyombo vya habari
