Tanzania Kupokea Uwenyeji wa Miss World 2027 Nchini Vietnam Leo

Global Publishers
September 5, 2026
18 views
0 Comments

Tanzania leo, Septemba 5, 2026, inatarajiwa kukabidhiwa rasmi uwenyeji wa mashindano ya Miss World 2027, baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, kuwasili nchini Vietnam kushiriki Fainali za Miss World 2026.

Katika hafla hiyo inayofanyika Vietnam, Naibu Waziri Mwinjuma anatarajiwa kupokea bendera ya Miss World, ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa Tanzania jukumu la kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa ya urembo duniani mwaka 2027.

Tanzania katika fainali za Miss World 2026 inawakilishwa na Mlimbwende Latricia Ian Sawe, ambaye anashiriki katika mashindano hayo akiiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Uenyeji wa Miss World 2027 unatarajiwa kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa ya utalii, utamaduni na fursa za kiuchumi, huku ukitarajiwa kuvutia wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani.