Kikao cha Katambi: Wasanii Wasamehewa, Anko T, Niffer Wakosa Msamaha – Video

Global Publishers
September 2, 2026
18 views
0 Comments

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema wasanii na watu maarufu walioitikia wito wa kufika kwenye kikao alichokiitisha leo Septemba 2, 2026, wamesamehewa makosa mbalimbali waliyokuwa nayo.

Katambi amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, akieleza kuwa Jennifer Jovin na Twalibu Bakari Anko T hawakusamehewa kutokana na kutofika kwenye kikao hicho.

Amesema baadhi ya wasanii waliohudhuria walikuwa na mashtaka mbalimbali, ambapo Wizara ilikaa pamoja na waliowashtaki na kuzungumza nao kuhusu uwezekano wa kuwasamehe.

Aidha, amesema kikao hicho kilitumika pia kuwapa wasanii na watu hao maarufu elimu kuhusu masuala ya sheria, hususan matumizi ya mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Katambi, baadhi yao walikiri kuwa walikuwa wakifanya makosa kupitia mitandao ya kijamii bila kufahamu kuwa vitendo hivyo vinaweza kuwa kinyume cha sheria.

Kuhusu Anko T na Noel, ambaye ni mwanamitindo anayehusishwa na msanii Diamond Platnumz, Katambi amesema wameeleza kuwa wako nje ya nchi, huku wakitakiwa kurejea nchini.