Baraza la Wazazi CCM Launga Mkono Nchimbi Kuvuliwa Uanachama – Video

Global Publishers
August 30, 2026
24 views
0 Comments

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Wazazi la CCM Taifa, Ally Salum Hapi

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Wazazi la CCM Taifa, Ally Salum Hapi, amesoma azimio la Jumuiya hiyo la kuunga mkono uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wa kumvua uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Azimio hilo limesomwa Agosti 29, 2026, katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yaliyofanyika jijini Mwanza.

Akisoma azimio hilo, Hapi amesema uamuzi huo umezingatia tamko na maamuzi yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, pamoja na jukumu la Jumuiya ya Wazazi la kusimamia maadili katika jamii.

Amesema Jumuiya hiyo imeona umuhimu wa kuunga mkono uamuzi huo kutokana na wajibu wake wa kuhimiza na kusimamia maadili ndani ya jamii na chama.

Hapi amesema azimio hilo limepitishwa kwa kauli moja na wajumbe wote, baada ya Jumuiya ya Wazazi kufanya kikao chake Agosti 28, 2026.

Hatua hiyo imekuja katika kipindi ambacho uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuhusu uanachama wa Dkt. Nchimbi umeendelea kuzua mjadala ndani na nje ya chama.