
MOROGORO; Wananchi wa Mkoa wa Morogoro wamejitokeza kwa wingi katika Usiku wa Nyama Choma, ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea mkoani humo.
Usiku huo uliofanyika Agosti 28, 2026 kuamkia Agosti 29, 2026 meleta burudani kwa wananchi na washiriki wa tamasha hilo, huku ukiwa pia fursa muhimu ya kukuza shughuli za kiuchumi kwa wananchi kupitia biashara, utamaduni na ubunifu, pamoja na kuwakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linatarajiwa kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano, kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia utajiri wake wa utamaduni, sanaa na utalii.

