Rais Mwinyi: Afrika Isibakie Kuwa Soko la Teknolojia, Ijenge Uwezo wa Kuizalisha

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Afrika haiwezi kuendelea kubaki kuwa soko la teknolojia zinazozalishwa na mataifa mengine, bali inapaswa kujenga uwezo wa kuzalisha teknolojia na bunifu zake, kukuza vipaji na kujipambanua kuwa kitovu cha ushindani katika ubunifu na uwekezaji.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, Septemba 29, 2026, wakati akifungua Maonesho ya Teknolojia na Akili Unde (Tech and AI Expo Zanzibar 2026) katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar, sambamba na uzinduzi wa Sera ya Kidijitali ya Zanzibar 2026 (Zanzibar Digital Policy 2026) inayolenga kutoa mwelekeo wa mageuzi ya mageuzi ya kidijitali Zanzibar.

Amesema mageuzi ya teknolojia yanatoa fursa kubwa kwa Afrika kukabiliana na changamoto za maendeleo, kuboresha huduma za umma, kupanua upatikanaji wa elimu na afya, kuongeza uzalishaji, kuimarisha biashara na kufungua fursa mpya za ajira.

Rais Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuweka mazingira na miundombinu yatakayowezesha wananchi, wafanyabiashara na taasisi kutumia teknolojia kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Amesema Serikali inalenga kuunganisha kaya 100,000 na huduma za intaneti za uhakika kupitia mfumo wa Fibre-to-the-Home (FTTH) ndani ya miaka mitatu, sambamba na kuimarisha mawasiliano kupitia nyaya za chini ya bahari (Submarine Cable) na kuendeleza miundombinu ya vituo vya kuhifadhi na kuchakata taarifa (Data Centers).

Akizungumzia Akili Unde (Artificial Intelligence – AI), Rais Mwinyi amesema teknolojia hiyo ina uwezo mkubwa wa kuongeza tija katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, elimu, utalii, huduma za Serikali na biashara.

Hata hivyo, amesema matumizi ya AI yanahitaji miundombinu imara, taarifa sahihi na za kuaminika, wataalamu wenye ujuzi, usimamizi wenye uwajibikaji pamoja na imani ya wananchi katika matumizi ya teknolojia hiyo.

Amesema Serikali inaandaa Mfumo Mkakati wa Akili Unde (AI Strategy Framework) utakaosaidia kuhakikisha matumizi ya teknolojia hiyo yanafanyika kwa usalama na kwa kuzingatia uwajibikaji katika uchumi na huduma za umma, huku ikilinda faragha, usalama na haki za msingi za wananchi.

Aidha, Rais Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuweka mfumo bora wa kisheria na kisera kwa kampuni changa, wabunifu na wawekezaji wa teknolojia, sambamba na kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi na uwajibikaji katika mazingira ya kidijitali.

Amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano katika miundombinu ya kidijitali, usalama wa mtandao, usimamizi wa taarifa, utafiti, ubunifu na uhamishaji wa teknolojia ili kuiwezesha Afrika kuwa na uwezo mkubwa wa kutatua changamoto zake.

Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga, amesema Serikali inalenga kujenga mazingira yatakayowawezesha vijana kutumia teknolojia na ubunifu kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali na kutengeneza bidhaa na huduma zenye uwezo wa kushindana katika masoko ya kimataifa.

Katika maonesho hayo, Rais Dkt. Mwinyi pia ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) baina ya Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar na Huawei Technologies Tanzania Limited, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya teknolojia.

Maonesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa teknolojia, wakiwemo wataalamu wa Akili Unde, wawekezaji, watafiti, kampuni changa, washirika wa maendeleo na vijana wabunifu kutoka ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kubadilishana maarifa, kuimarisha ushirikiano na kujadili nafasi ya teknolojia katika maendeleo ya Afrika.

Madereva wagoma, abiria wakwama Moshi – HabariLeo

MOSHI: Baadhi ya madereva wa mabasi katika Stendi Kuu ya Mabasi Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamegoma kutoa huduma za usafiri kwa saa kadhaa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni kwa makosa ya barabarani, wakidai kuwa utaratibu huo unawaongezea mzigo wa kiuchumi licha ya baadhi ya makosa hayo kutozwa faini.

Madereva hao pia wanaitaka Serikali kuweka wazi mgawanyo wa uwajibikaji kati yao na wamiliki wa magari, wakieleza kuwa baadhi ya makosa yanayosababisha kukatwa pointi yanahusiana na hali na vifaa vya magari ambavyo viko chini ya dhamana ya wamiliki.

Mgomo huo umesababisha baadhi ya safari kusitishwa na abiria waliokuwa tayari wamekata tiketi kukosa usafiri, hali iliyolazimu uongozi wa kituo kushirikiana na wadau wengine kutafuta usafiri mbadala.

Akizungumza kuhusu sababu za mgomo huo, dereva wa mabasi, Emmanuel Singine, amesema mfumo wa faini na kukatwa pointi unawaweka madereva katika mazingira magumu kiuchumi, hasa wale wenye majukumu ya kifamilia.

Singine amesema dereva anapokosea na kutozwa faini ya Sh30,000, bado hukatwa pointi, hali ambayo amesema inaongeza gharama kwa dereva ambaye tayari ana majukumu ya kugharamia familia na elimu ya watoto.

“Nina mke na watoto na nasomesha. Nakosea unanipa fine ya 30 elfu, halafu bado unanikata pointi. Nikikatwa pointi zikifika 15, natakiwa kurudi tena shule na kulipa ada. Kwa mtindo huu nitaweza kulipa pointi, fine na kulipa ada ikiwemo kusomesha watoto?” amehoji Singine.

Amesema madereva wanahitaji maelezo ya wazi kuhusu namna mfumo wa pointi unavyotekelezwa, huku akitaka uwajibikaji ugawanywe kati ya dereva na mmiliki wa gari kulingana na aina ya kosa.

Ametoa mfano wa makosa yanayohusu vifaa vya gari, kama matairi na vioo, akisema yanapaswa kuwajibishwa zaidi kwa mwenye gari, wakati makosa yanayotokana moja kwa moja na mwenendo wa dereva, kama kuzidisha abiria, yawajibishwe kwa dereva.

“Kama watatukata pointi kulingana na makosa tushirikiane. Kama ni vifaa kama matairi, kioo na kadhalika, alipishwe mwenye gari, lakini kama ni kuhusu kuzidisha abiria basi mimi kama dereva niwajibishwe,” amesema.

Kwa upande wake, Shadrack Kaaya, dereva wa kampuni ya Masalu, amesema malalamiko yao yanahusu namna sheria zinavyotekelezwa dhidi ya madereva, akidai kuwa baadhi ya makosa, yakiwemo ya kupita magari mengine (overtaking), yanaweza kusababisha kukatwa pointi.

Kaaya amesema hali hiyo inazidishwa na ukweli kwamba madereva wengi hawana mikataba ya ajira inayowalinda ipasavyo, hivyo ameiomba Serikali kuangalia upya mfumo huo na kuhakikisha majukumu yanagawanywa kwa kuzingatia aina ya kosa.

“Madereva wengi hawana mikataba. Serikali itusaidie kwa sababu hizi sheria zinambana dereva peke yake wakati mengine yanamhusu mwenye gari. Asilimia 99 dereva ndiye anabanwa na hizi sheria,” amesema Kaaya.

Akizungumzia athari za mgomo huo, Samuel Mlay, msimamizi wa Kituo cha Mabasi Moshi, amesema baadhi ya mabasi yaliyokuwa tayari yameuza tiketi yalishindwa kuondoka kutokana na kukosekana kwa madereva.

Mlay amesema uongozi wa kituo ulihusika kutafuta usafiri mbadala kwa abiria waliokwama ili kuwawezesha kuendelea na safari zao na kupunguza usumbufu uliotokana na hali hiyo.

Wakati huo huo, Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyelo, alikuwa katika kituo hicho na kushirikiana na uongozi wa stendi kuhakikisha abiria waliokosa usafiri wanapata usafiri mbadala na kuendelea na safari zao.

Hata hivyo, Nyelo hakutaka kuzungumzia zaidi sababu za mgomo huo wala kutoa maelezo kuhusu hatua zinazochukuliwa na mamlaka kukabiliana na malalamiko ya madereva.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO), Nassoro Sisiwaya, ambaye pia alikuwepo katika kituo hicho, hakutoa maelezo kuhusu mgomo huo na hatua zinazochukuliwa.

Hadi wakati wa taarifa hii, baadhi ya mabasi yalikuwa yakiendelea na safari, huku mengine yakiwa yamesitisha huduma kutokana na mgomo huo.

Madereva hao wanataka mamlaka husika kuangalia upya utekelezaji wa mfumo wa faini na pointi za leseni, pamoja na kuweka utaratibu unaotambua wajibu wa dereva na mmiliki wa gari kulingana na aina ya kosa.

 

Chalamila apiga marufuku utupaji taka Tabata Liwiti – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameziagiza kampuni zinazokusanya na kusafirisha taka katika eneo la Tabata Liwiti, Mtaa wa Mfaume, Wilaya ya Ilala, kuacha mara moja utupaji wa taka ovyo na kuzitaka kuzipeleka katika dampo lililotengwa, ikiwemo Pugu.

Chalamila amesema wananchi wanalipia huduma ya ukusanyaji na usafirishaji wa taka, hivyo kampuni yanayotekeleza jukumu hilo yanapaswa kuzingatia makubaliano na kuhakikisha taka zinapelekwa katika maeneo rasmi yaliyotengwa.

Amesema mkandarasi yeyote atakayebainika kumwaga taka katika eneo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kufutiwa mkataba na kampuni yake kuondolewa katika utekelezaji wa huduma hiyo.

Amesema utupaji taka ovyo unaweza kuhatarisha afya za wananchi, kuchangia milipuko ya magonjwa kama kipindupindu na kuharibu mazingira, huku akibainisha kuwa eneo hilo lipo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Aidha, amewataka wakurugenzi wa halmashauri wanaosimamia wakandarasi wa usafi kuhakikisha wanawajibika ipasavyo na kuchukua hatua dhidi ya kampuni zinazokiuka masharti ya kazi.

Amewataka viongozi wa serikali za mitaa, wenyeviti na watendaji kuhakikisha maeneo yao yanalindwa dhidi ya utupaji taka ovyo, akisisitiza kuwa jukumu la usafi haliwezi kuachwa kwa viongozi wa mkoa na wilaya pekee.

Katika hatua nyingine, Chalamila ameelekeza wananchi watakaokamatwa wakitupa taka ovyo wapewe adhabu ya kufanya usafi katika maeneo machafu kwa muda utakaopangwa, badala ya kufungwa pekee, ili kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kutunza mazingira.

Amesema Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha Bonde la Mto Msimbazi, hivyo hakuna sababu ya kuendelea kutupa taka katika maeneo hayo.

Kutokana na hali hiyo, amezitaka wataalamu kutoka Bonde la Msimbazi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kukutana na kuweka mkakati wa pamoja wa kudhibiti tatizo hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema changamoto hiyo inachangiwa na baadhi ya viongozi na wakazi wanaoshinikiza makampuni kutupa taka katika eneo hilo.

Ameongeza kuwa tatizo jingine ni baadhi ya watu wanaojihusisha na masuala ya mazingira pamoja na kamati zao kutoa vibali vya uchimbaji mchanga kiholela katika eneo hilo.

Tanzania Yaingia Hatua ya Pili Miss Grand International 2026

Dar es Salaam – Tanzania, kupitia mrembo wake Jihan Dimack, Miss Grand Tanzania 2026, imefanikiwa kuingia katika hatua ya pili ya kipengele cha Country’s Power of the Year kwenye mashindano ya Miss Grand International 2026.

Baada ya kukamilika kwa Round 1, jumla ya washiriki 40 bora wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya pili, ambapo wamegawanywa kwa bahati nasibu katika makundi manne yenye washiriki 10 kila moja.

Tanzania kupitia Jihan Dimack imepangwa katika Group A, pamoja na washiriki wengine tisa kutoka mataifa tofauti.

Katika hatua hii, washiriki wawili bora kutoka kila kundi ndio watakaofuzu kwenda hatua inayofuata.

Hii ina maana kwamba kati ya washiriki 40 waliopo Round 2, ni jumla ya washiriki wanane pekee watakaosonga mbele.

KURA ZA SAA 48

Kwa mujibu wa taarifa ya Miss Grand International, upigaji kura wa Round 2 umeanza Septemba 28, 2026 saa 5:00 jioni kwa saa za GMT+7, na utafikia mwisho Septemba 30, 2026 saa 5:00 jioni kwa saa za GMT+7.

Hivyo, zoezi hilo litadumu kwa muda wa saa 48 pekee.

JINSI YA KUMPIA KURA JIHAN

Kura zinapigwa kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Miss Grand International.

Ili kushiriki katika kura, shabiki anatakiwa kwanza kuifuatilia akaunti rasmi ya Miss Grand International, kisha kushiriki katika chapisho maalum la kundi la Round 2 lililotengwa kwa ajili ya upigaji kura.

Kwa Tanzania, Watanzania wanatakiwa kufuatilia akaunti rasmi ya mashindano na kushiriki kwenye chapisho linalomhusu Jihan Dimack ili kumuongezea nafasi ya kusonga mbele.

MFUMO WA UPATIKANAJI WA POINTI

Katika Round 2, mfumo wa alama umeweka uzito mkubwa kwenye New Followers, ambao unachangia asilimia 95 ya alama zote.

  • 95% – New Followers: Alama zitazingatia idadi ya wafuasi wapya wanaohusishwa na chapisho la kura la kila mshiriki katika kipindi rasmi cha upigaji kura.

  • 5% – Engagement: Ushiriki wa mashabiki kupitia Like, Repost na Comment pia utachangia katika matokeo.

Kwa upande wa engagement, mfumo umeainisha:

  • ❤️ Like = Pointi 1

  • 🔄 Repost = Pointi 2

  • 💬 Comment = Pointi 1

Alama za New Followers na Engagement zitahesabiwa kwa uwiano ili kupata alama ya mwisho ya kila mshiriki.

DATA YA INSTAGRAM NDIYO ITAKAYOTUMIKA

Waandaaji wameeleza kuwa matokeo yatategemea Instagram Insights kutoka kwenye akaunti rasmi ya Miss Grand International.

Data itakayohesabiwa ni ile iliyorekodiwa ndani ya muda rasmi wa upigaji kura pekee.

Endapo washiriki wawili watakuwa na alama zinazolingana, mshiriki mwenye alama nyingi zaidi kutoka kwa New Followers ndiye atakayepewa nafasi ya kusonga mbele.

Kwa ufupi, mfumo wa Round 2 ni:

Washiriki 40 → Makundi 4 → Washiriki 10 kila kundi → Washiriki 2 bora kutoka kila kundi → Washiriki 8 wanafuzu.

Kwa Jihan Dimack na Tanzania, kipindi cha saa 48 ni muhimu huku Watanzania wakihamasishwa kujitokeza kwa wingi kwenye Instagram ya Miss Grand International, kumfuatilia Jihan na kushiriki katika chapisho lake la kura.

Katuga Aweka Wazi Kifungu Kilichotumika Kumfungulia Mshtakiwa Shtaka la Uhaini

Dar es Salaam – Wakili wa Serikali, Peter Katuga, ameiambia Mahakama Kuu kuwa kauli zilizotolewa na mshtakiwa ndizo zilizotumiwa na Jamhuri kama msingi wa shtaka la uhaini linalomkabili.

Akitoa hoja za mwisho za upande wa Jamhuri mahakamani, Katuga amesema mshtakiwa anakabiliwa na shtaka hilo chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya mwaka 2022.

Kwa mujibu wa Katuga, hati ya mashtaka inadai kuwa Aprili 3, 2025, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikusudia kuchochea umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katuga amesema Jamhuri inadai kuwa nia hiyo ilidhihirishwa kupitia maneno yaliyotolewa na kusambazwa na mshtakiwa.

Amesema kauli hizo ndizo zilizochukuliwa na upande wa Jamhuri kuwa kiini cha mashtaka yanayomkabili mshtakiwa.

Akifafanua msingi wa kisheria wa shtaka hilo, Katuga amesema Kifungu cha 39(2)(d) kinaweka masharti yanayohusiana na kosa la uhaini kwa mtu aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwe yuko ndani au nje ya nchi.

Amesema kifungu hicho kinahusisha mtu anayetengeneza au kuendeleza nia ya kutenda vitendo vinavyotafsiriwa kuwa vya uhaini.

Katuga pia amerejea Kifungu cha 135 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Marejeo ya mwaka 2025, akieleza kuwa hati ya mashtaka inapaswa kubainisha kosa analodaiwa kutenda mshtakiwa pamoja na namna kosa hilo linavyodaiwa kufanyika.

Kwa mujibu wa wakili huyo, matakwa hayo yanalenga kuhakikisha mshtakiwa anafahamu kwa uwazi tuhuma zinazomkabili na namna anavyodaiwa kutenda kosa hilo.

Katuga amesema pia Kifungu cha 138(3)(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinataka lugha inayotumika katika hati ya mashtaka iwe ya kawaida, wazi na isiyoleta mkanganyiko.

Amesema sharti hilo ni muhimu ili mshtakiwa aweze kuelewa kwa usahihi tuhuma zinazomkabili na kujiandaa kujibu mashtaka hayo.

Aidha, Katuga amesisitiza kuwa moja ya masharti muhimu ya Kifungu cha 39(2)(d) ni kwamba mtu anayeshtakiwa chini ya kifungu hicho lazima awe chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwe yuko ndani au nje ya mipaka ya nchi.

Akiendelea na hoja zake, Katuga amesema Jamhuri ilifungua shtaka la uhaini kwa madai kwamba mshtakiwa alikuwa mtu aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kifungu hicho kinavyotaka.

Hoja hizo ni sehemu ya mawasilisho ya upande wa Jamhuri katika kesi hiyo, huku Mahakama ikiendelea kusikiliza hoja za kisheria za pande zinazohusika kabla ya hatua inayofuata katika kesi hiyo.

Aliyejifanya Ametekwa, Aliomba Milioni 5 Akamatwa na Polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemkamata kijana aitwaye Gatami Maduhu Martine (20), mkazi wa Kijiji cha Mwauchumu, Wilaya ya Bariadi, akidaiwa kuhusika katika tukio la kuteka mtu na kuomba Sh milioni 5 kwa ajili ya kumwachia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, tukio hilo lilianza baada ya Polisi kupokea taarifa kutoka kwa Gatami Maduhu Maltine (64), Msukuma na mkazi wa Mwauchumu, aliyesema mtoto wake aitwaye Gatami Maduhu Martine alikuwa ameondoka nyumbani tangu Septemba 19, 2026, na kuelekea Mgodini Mwabasabi Kata ya Gibeshi.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa mnamo Septemba 23, 2026, majira ya saa 4:00 usiku, Gatami Maduhu Martine alimpigia simu mdogo wake aitwaye Sayi Maduhu, akitumia namba 0613 035 688, na kumweleza kuwa yupo sehemu asiyoijua.

Aidha, alidai kuwa amefungwa na watu ambao walikuwa wakimtaka Sh milioni 5 ili wamwachie.

Baada ya taarifa hiyo kupokelewa, Polisi Bariadi ilianza uchunguzi na kufuatilia mawasiliano ya simu, hatua iliyowezesha kubaini kuwa kijana huyo alikuwa Kata ya Bwanga, Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita.

Polisi ilisema mtuhumiwa alikamatwa akiwa mzima wa afya na bila tatizo lolote.

Uchunguzi wa Polisi umebaini kuwa tukio hilo lilikuwa njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo mtuhumiwa alijifanya kuwa ametekwa na kuomba fedha kutoka kwa ndugu zake.

Jeshi la Polisi limeonya wananchi kuacha tabia ya kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu, likisisitiza kuwa vitendo vya aina hiyo vinahatarisha amani na usalama wa jamii.

Polisi pia limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapobaini vitendo vya uhalifu, huku likisisitiza kuwa mtu yeyote atakayekiuka sheria atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Sekretarieti ya Ajira Yatangaza Nafasi ya Afisa Sheria Mwandamizi

Global Publishers
September 29, 2026
0 views
0 Comments

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi moja (1) ya kuhamia ya Afisa Sheria Mwandamizi, kwa Watanzania ambao ni watumishi wa Umma wenye sifa na uwezo.

Majukumu ya nafasi hiyo ni pamoja na kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa Sekretarieti ya Ajira, kutoa mapendekezo ya maboresho katika uandaaji wa miswada ya sheria na sheria ndogo, kufuatilia mashauri yaliyopo mahakamani, pamoja na kusimamia uandaaji na mapitio ya nyaraka mbalimbali za kisheria.

Sifa za mwombaji:
Mwombaji anatakiwa kuwa mtumishi wa Umma mwenye Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) kutoka taasisi inayotambuliwa na Serikali, akiwa na uzoefu wa kazi usiopungua miaka saba katika eneo husika. Pia anatakiwa kuwa amehudhuria na kufaulu mafunzo ya uanasheria kwa vitendo au Shule ya Sheria Tanzania, pamoja na kusajiliwa kama wakili wa Mahakama Kuu.

Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa mtumishi wa Umma aliyefanya kazi kwa mwajiri wake wa sasa kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu na awe tayari kugharamia gharama za uhamisho.

Waombaji wanapaswa kuambatisha CV yenye maelezo ya kina, vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa, cheti cha kuzaliwa, pamoja na majina ya wadhamini watatu. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Oktoba 2026. Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Ajira.

FIFA Yashutumu UEFA Kwa Kampeni ya Upotoshaji Dhidi ya Infantino

FIFA imeishutumu UEFA kwa kuendesha kile ilichokiita “kampeni ya upotoshaji” pamoja na kujaribu kuathiri uchaguzi wa urais wa FIFA, huku ikiomba Mahakama ya Marekani ikatae ombi la UEFA la kupata nyaraka na ushahidi kutoka kwa taasisi hiyo.

UEFA mwezi uliopita iliwasilisha ombi katika Mahakama ya Shirikisho nchini Marekani ikitaka ruhusa ya kupata ushahidi na nyaraka zitakazotumika katika malalamiko ya jinai yanayopangwa kuwasilishwa nchini Uswisi dhidi ya Rais wa FIFA, Gianni Infantino.

Malalamiko hayo yanahusishwa na mpango uliokuwa umepewa jina la FIFA Forward Enterprise (FFE), ambao ulikuwa na lengo la kuhamisha baadhi ya haki za kibiashara za Kombe la Dunia kwenda katika kampuni hiyo. Mpango huo ulisitishwa mwezi Julai baada ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa mashirikisho mbalimbali, yakiwemo UEFA, CONCACAF na Shirikisho la Soka la Asia.

Katika majibu yake yaliyowasilishwa Jumatatu, FIFA ilidai kuwa nyaraka za UEFA zina “taarifa nyingi za uongo au zinazopotosha” kuhusu FIFA na Infantino.

FIFA pia imekanusha madai kwamba Infantino alikusudia kujinufaisha binafsi kupitia mpango wa FFE, ikisema mpango huo ulipaswa kupata idhini kutoka kwa vyama wanachama wa FIFA pamoja na Baraza la FIFA.

Mzozo Kuhusu Thamani ya FFE

UEFA ilidai kuwa wawekezaji walikuwa tayari kulipa dola bilioni 4.2 kwa hisa katika FIFA Forward Enterprise, jambo ambalo lingeifanya kampuni hiyo kuwa na thamani ya takribani dola bilioni 20.

UEFA ilisema thamani hiyo ilidharau kwa kiasi kikubwa haki za kibiashara za FIFA na kwamba mchakato huo haukuhusisha zabuni ya wazi wala tathmini huru.

Hata hivyo, FIFA imekanusha hoja hiyo, ikisema UEFA imechanganya “equity value” na “enterprise value.”

Kwa mujibu wa FIFA, thamani ya hisa ya FFE ilikuwa dola bilioni 20, huku thamani ya jumla ya biashara ikiwa zaidi ya dola bilioni 30.

Mzozo Wafikia Uchaguzi wa Urais FIFA

FIFA pia imedai kuwa hatua za kisheria zinazochukuliwa na UEFA zinaweza kuwa na uhusiano na uchaguzi wa urais wa FIFA unaotarajiwa kufanyika Machi 2027, ambapo Infantino anawania kuchaguliwa tena.

Wiki iliyopita, Infantino aliwaandikia vyama vyote 211 wanachama wa FIFA akipendekeza kufanyika kwa mapitio huru ya mifumo ya maamuzi na utawala wa taasisi hiyo.

FIFA imesema hatua ya UEFA ya kuwasilisha nyaraka hizo mahakamani wakati uchaguzi huo ukikaribia ni jaribio la kuathiri uchaguzi huo.

UEFA haikuwa imetoa majibu mara moja kwa ombi la Reuters la kutoa maoni kuhusu tuhuma hizo.

Miaka 17 ya Manchester City Yafika Kwenye Kivumbi cha Mashtaka 115

Historia ya mafanikio ya Manchester City katika zaidi ya muongo mmoja imeambatana na mjadala mkubwa kuhusu namna klabu hiyo ilivyofadhili ukuaji wake tangu iliponunuliwa na Abu Dhabi United Group mwaka 2008.

Sasa, klabu hiyo inakabiliwa na kesi kubwa zaidi ya kinidhamu katika historia ya Premier League, baada ya kushutumiwa kwa jumla ya makosa 115 ya kanuni za kifedha yanayohusishwa na kipindi cha mwaka 2009 hadi 2018.

Kesi hiyo imechukua miaka kadhaa, huku Manchester City ikikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa ushahidi wake utaonyesha kuwa haikukiuka kanuni hizo.

Mwanzo wa enzi mpya

Mabadiliko makubwa Manchester City yalianza Septemba 2008, wakati Abu Dhabi United Group iliponunua klabu hiyo kutoka kwa Thaksin Shinawatra.

Usajili wa Mbrazil Robinho kwa ada iliyokuwa rekodi nchini England siku hiyo ulikuwa ishara ya kwanza ya uwezo mkubwa wa kifedha wa wamiliki wapya.

Msimu uliofuata City iliendelea kutumia fedha nyingi katika usajili, ikiwemo kumsajili Carlos Tevez kutoka Manchester United, Emmanuel Adebayor kutoka Arsenal na wachezaji wengine.

Wakati huo huo, UEFA ilikuwa inaanzisha mfumo wa Financial Fair Play (FFP) uliolenga kuhakikisha klabu hazitumii fedha zaidi ya mapato zinazozalisha.

Mafanikio yakaanza kuja

Chini ya Roberto Mancini, Manchester City ilianza kubadilisha nguvu yake ya kifedha kuwa mafanikio uwanjani.

Mwaka 2011, City ilishinda FA Cup, ikiwa ni taji lake kubwa la kwanza baada ya miaka 35.

Mwaka mmoja baadaye, ilikuja moja ya siku maarufu zaidi katika historia ya Premier League.

City ilihitaji ushindi dhidi ya Queens Park Rangers ili kutwaa ubingwa, lakini ilikuwa nyuma hadi dakika za nyongeza. Edin Dzeko na Sergio Aguero walifunga katika dakika za mwisho na kuipa City ushindi wa 3-2 na ubingwa wake wa kwanza wa England tangu mwaka 1968.

Maswali kuhusu fedha

Kadiri mafanikio yalivyoongezeka, ndivyo maswali kuhusu matumizi na vyanzo vya fedha yalivyozidi.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni mikataba ya udhamini iliyohusisha kampuni kutoka Abu Dhabi, ikiwemo Etihad Airways.

Baadaye, nyaraka zilizochapishwa na Der Spiegel kupitia Football Leaks ziliibua madai kuhusu namna baadhi ya mikataba hiyo ilivyofadhiliwa.

Manchester City ilikanusha madai hayo, ikisema taarifa zilizotolewa zilitokana na udukuzi wa barua pepe na uchapishaji wa nyaraka nje ya muktadha.

UEFA nayo ikaingia

Mwaka 2014, UEFA iliichukulia City hatua kwa kukiuka kanuni za Financial Fair Play, baada ya klabu hiyo kuripoti hasara kubwa.

City ilifungiwa baadhi ya matumizi na kutozwa faini, huku idadi ya wachezaji wake katika mashindano ya Champions League ikipunguzwa.

Mwaka 2020, UEFA ilichukua hatua kubwa zaidi baada ya kuamua kuifungia City kushiriki mashindano ya Ulaya kwa miaka miwili.

Hata hivyo, Manchester City ilikata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), ambayo iliondoa adhabu ya kufungiwa na kupunguza faini.

Guardiola na enzi ya mafanikio makubwa

Kufikia kipindi hicho, City ilikuwa tayari imekuwa moja ya timu kubwa zaidi England.

Kuwasili kwa Pep Guardiola mwaka 2016 kuliongeza kasi ya mafanikio.

City ilitwaa mataji mengi ya Premier League, FA Cup na League Cup, huku mwaka 2023 ikifikia kilele kwa kushinda UEFA Champions League na kukamilisha treble baada ya kutwaa pia Premier League na FA Cup.

Erling Haaland naye aliingia katika historia kwa kuvunja rekodi nyingi za ufungaji tangu alipowasili mwaka 2022.

Mashtaka 115

Mnamo Februari 2023, Premier League iliishtaki Manchester City kwa madai ya kukiuka kanuni za kifedha mara 115 katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2018.

Mashtaka hayo yalihusisha madai mbalimbali kuhusu taarifa za kifedha, mapato ya udhamini, malipo ya mameneja na wachezaji pamoja na wajibu wa klabu kushirikiana na uchunguzi.

City ilikanusha mashtaka hayo na kusema ilikuwa na imani kuwa ushahidi wake ungeonyesha kuwa madai hayo hayakuwa na msingi.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwaka 2024 mbele ya jopo huru.

Uamuzi wa jopo

Mnamo Septemba 25, 2026, iliripotiwa kuwa jopo huru lililokuwa likisikiliza kesi hiyo limefikia uamuzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, Manchester City imepatikana na hatia katika idadi kubwa ya mashtaka hayo 115, ingawa maelezo kamili kuhusu ni mashtaka gani yamekubaliwa na yapi yamekataliwa bado hayajawekwa wazi.

City haijatoa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo, huku mchakato wa kisheria ukiendelea na klabu ikiwa na uwezekano wa kukata rufaa.

Adhabu bado haijajulikana

Kwa sasa, hatua inayofuata ni kusubiri mchakato wa kuamua adhabu.

Miongoni mwa adhabu zinazoweza kujadiliwa ni faini, kupunguzwa pointi au hatua nyingine kali zaidi kwa mujibu wa kanuni husika. Pia kumekuwa na mjadala kuhusu uwezekano wa mataji kuathiriwa iwapo ukiukaji uliothibitishwa utahusishwa na misimu husika.

Hata hivyo, hakuna adhabu ya mwisho iliyotangazwa bado, na mchakato wa rufaa unaweza kubadilisha matokeo ya sasa.

Kesi yenye athari kubwa

Kesi hii imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu kwa sababu inaweza kuwa na athari kubwa kwa Manchester City na historia ya Premier League.

Kwa zaidi ya miaka 17, City imebadilika kutoka klabu iliyokuwa ikipambana kupata mafanikio hadi kuwa moja ya timu zilizotawala soka la England na Ulaya.

Lakini sasa mafanikio hayo yameingia katika kipindi cha kusubiri majibu ya mwisho ya mchakato wa kisheria.

Kinachobaki ni kujua ni mashtaka gani hasa yamebaki, adhabu itakayowekwa na kama Manchester City itaweza kubadilisha matokeo hayo kupitia rufaa.

Hivyo, baada ya miaka mingi ya uchunguzi, kesi ya “Manchester City 115” bado haijafikia mwisho wake.

Cheetah Wild Yafungua Safari ya Porini Ndani ya Meridianbet

Global Publishers
September 29, 2026
0 views
0 Comments

Meridianbet inakuletea mchezo unaokupa ladha halisi ya porini. Cheetah Wild kutoka Pragmatic Play inakualika kwenye safari yenye wanyama, mizunguko ya bure na alama za pesa. Kila mzunguko unaongeza msisimko na kukufanya ufuatilie hatua inayofuata.

Kupata alama za Scatter ndiyo njia ya kufungua mizunguko ya bure. Scatter tatu zinakupa mizunguko ya bure 8, nne zinakupa 15, na tano zinakupa 20. Ukifika kwenye mizunguko ya bure, safari inaendelea kupitia mfumo wa Level Up.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Alama ya LEVEL UP inakusaidia kupanda kutoka Level 1 hadi Level 5. Kila Level ina mabadiliko yake. Tembo, Kifaru, Pundamilia na Swala wanaweza kubadilika kuwa alama za pesa kadiri unavyopanda. Hii inafanya kila hatua ya mizunguko ya bure kuwa na kitu kipya cha kusubiri.

Cheetah Wild pia inakupa Ante Bet na Buy Feature kwa chaguo zaidi na burudani kubwa. Na kwa wale wanaofuatilia ushindi mkubwa, mchezo una kiwango kikubwa sana cha malipo cha hadi mara 5,000 ya dau lako. Safari inaweza kuanza kwa raundi moja na kuendelea hadi hatua za juu.

Usikae nje wakati pori limefunguka ndani ya kasino ya Meridianbet. Cheetah Wild iko tayari kwa safari yako ya ushindi. Ingia Meridianbet, zungusha reels mara nyingi uwezavyo, fungua mizunguko ya bure na uone kama unaweza kufika Level 5.