Mgomo wa Madereva: Katambi Aweka Wazi Hatua za Serikali, Leseni Zarejeshwa, VTS Yachunguzwa – Video

DAR ES SALAAM: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametangaza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumaliza kero za madereva na mgomo uliodumu kwa siku mbili.

Akizungumza leo, Septemba 30, 2026, katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi jijini Dar es Salaam, Katambi amesema maagizo ya Rais yamepitishwa kwa Waziri Mkuu na kuanza kutekelezwa kwa haraka.

Miongoni mwa hatua hizo ni kurejeshwa kwa leseni za madereva, kuondolewa kwa vizuizi visivyo na sababu barabarani pamoja na kushughulikia miundombinu ya barabara, ikiwemo matengenezo ya maeneo yenye mashimo yanayoweza kusababisha ajali.

Kuhusu madereva ambao leseni zao zilikamatwa au kufungiwa kutokana na makosa madogomadogo, Katambi amesema wataweza kurejeshewa leseni zao kwa mujibu wa sheria kupitia Mamlaka ya Rufaa iliyo chini ya Waziri wa Mambo ya Ndani.

Amesema hatua hiyo haitawahusu madereva waliothibitika kuhusika na ajali mbaya zilizosababisha vifo na ambao kesi zao bado zinaendelea mahakamani.

Katambi pia amewataka madereva na wananchi kutafuta suluhisho la changamoto kupitia mazungumzo badala ya migogoro, akisisitiza umuhimu wa Serikali kusikiliza na kuwashirikisha wananchi katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.

Amesema amepewa mamlaka na Waziri Mkuu kushughulikia malalamiko ya madereva na kwamba changamoto zao sasa zitafanyiwa kazi.

Katika hatua nyingine, Katambi ametangaza kuwa wizara nne za Serikali zitakutana kuchambua na kutafuta suluhisho la changamoto zinazotokana na Mfumo wa Kufuatilia Magari (VTS).

Amesema mkutano huo utazihusisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi pamoja na Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano.

Hatua hiyo imekuja baada ya madereva kulalamikia tofauti za takwimu kati ya mfumo wa VTS na kamera za usalama barabarani.

Kwa mujibu wa Katambi, kuna maeneo ambayo kamera za usalama barabarani zinaweza kuonesha gari lilikuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 100 kwa saa, wakati mfumo wa VTS unaonesha kasi ya kilomita 130 kwa saa.

Amesema tofauti hizo zimekuwa zikisababisha madereva kupata adhabu na kuingia katika changamoto ambazo zinahitaji kufanyiwa tathmini.

Katambi amesema Serikali itakaa pamoja kuchambua changamoto hizo na kuweka utaratibu utakaokuwa na uwazi na haki zaidi kwa madereva.

Aidha, amesema mfumo wa VTS ni wa muda katika kipindi cha mpito, huku Serikali ikielekea kwenye mfumo wa kisasa wa kidijitali wa kudhibiti mwendo wa magari.

Kwa maelezo yake, mfumo huo mpya utakuwa na mfumo wa kamera huru zitakazorekodi makosa ya barabarani moja kwa moja bila kuhitaji udhibiti wa askari.

Katambi amefananisha mfumo huo na VAR inayotumika katika soka, akisema lengo ni kuhakikisha ushahidi wa kamera unatumika katika kuthibitisha makosa na kuongeza usawa katika utekelezaji wa sheria za usalama barabarani.

Mgomo wa Madereva: Katambi Aweka Wazi Hatua za Serikali, Leseni Zarejeshwa, VTS Yachungwa – Video

SAME WATAKIWA KUTUMIA MVUA ZA EL NINO KUPANDA MITI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Yusto Mapande, amewataka wananchi na watumishi wa umma kutumia mvua zinazotarajiwa kunyesha kutokana na hali ya El Niño kupanda miti kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Mapande ametoa wito huo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Same.

Amesema pamoja na tahadhari zinazotolewa kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo, wananchi wanapaswa pia kuzitazama kama fursa ya kupanda miti, kwani unyevu wa mvua utasaidia miche kustawi vizuri.

Amesema upandaji wa miti kwa wingi utasaidia kulinda mazingira, ikiwamo kupunguza mmomonyoko wa udongo, huku akiwataka wananchi kuanza zoezi hilo mapema kabla na wakati wa mvua.

“Pamoja na tahadhari tunazotoa kuhusu mvua hizi, tutumie pia fursa hii kupanda miti kwa wingi. Miti ikipata mvua kwa wakati itastawi vizuri na baadaye itasaidia katika kulinda mazingira na kupunguza mmomonyoko wa udongo,” amesema.

Aidha, amewataka madiwani kwenda kutoa elimu katika kata zao na mashuleni kuhusu umuhimu wa upandaji miti, akisisitiza kuwa wananchi wapande miti ya kawaida pamoja na miti ya matunda.

Amesema hatua hiyo itaunga mkono kampeni ya Mkuu wa Wilaya ya Same, Kaslida Mgeni, ya kuifanya Same kuwa wilaya ya kijani, hivyo amewataka wananchi kuanza utekelezaji wake mapema.

Katika hatua nyingine, Mapande amemtaka Mkuu wa Idara ya Kilimo kuanzisha hamasa ya kilimo cha mazao ya kimkakati, hususan zao la parachichi, ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.

Amesema baada ya kipindi cha El Niño, idara hiyo inapaswa kuandaa taarifa itakayoonyesha idadi ya miche ya parachichi iliyopandwa pamoja na kata ambazo zimefanikiwa katika kilimo hicho.

“Baada ya miaka mitatu tunahitaji kujua tumefikia wapi. Tuwe na kumbukumbu ya idadi ya miparachichi iliyopandwa, kata gani imefanya vizuri na ni matokeo gani tunayotarajia baada ya mvua hizi,” amesema.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Same Mamndolwa Gembe amesema wananchi hawapaswi kuzitazama mvua hizo kwa upande wa madhara pekee, bali wazitumie pia kama fursa ya kupanda miche ya mazao  

Dkt. Mwigulu Akutana na Viongozi wa Madereva, Mgomo Wasitishwa

Global Publishers
September 30, 2026
18 views
0 Comments

DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini, hatua iliyofuatia makubaliano ya kusitisha mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Septemba 30, 2026, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo, viongozi wa madereva wamekubali kusitisha mgomo huo, hivyo kuwezesha huduma za usafiri kuendelea kama kawaida nchini.

Serikali pia imeeleza utayari wake wa kusikiliza na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva, kwa lengo la kutafuta suluhisho la masuala yaliyosababisha mgomo huo.

Hatua hiyo inatarajiwa kurejesha huduma za usafiri huku Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiendelea na majadiliano kuhusu changamoto zinazowakabili madereva.

Makubaliano hayo yamekuja baada ya mgomo wa siku mbili ambao uliathiri huduma za usafiri katika maeneo mbalimbali nchini.

DKT. MWIGULU AKUTANA NA VIONGOZI WA MADEREVA, MGOMO WASITISHWA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubali kusitisha mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili, hatua inayowezesha huduma za usafiri kuendelea kama kawaida.

Aidha, Serikali imeeleza utayari wake wa kusikiliza na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva, kwa lengo la kupata suluhisho la masuala yaliyosababisha mgomo huo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha huduma za usafiri zinaendelea kutolewa huku majadiliano kuhusu changamoto za madereva yakiendelea kati ya Serikali na wadau husika.

VIVUTIO VYA UTALII KUTANGAZWA NCHINI INDIA

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India, imewapokea jumla ya mawakala wa utalii 13 kutoka India kwa ajili ya ziara maalum ya utangazaji utalii (Familiarization Trip) itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 28 Septemba 2026 hadi 04 Oktoba, 2026.

Lengo kuu la ziara hii ni kuwapa fursa mawakala hao kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yao na wadau wa utalii wa Tanzania.

Akizungumza kuwakaribisha nchini Mawakala hao, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega ambaye ameongozana na ujumbe huo, amesema Ubalozi utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii kutoka India katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kukuza sekta hiyo na kuchangia Uchumi wa nchi na kwamba ziara ya mawakala hao ni moja ya jitihada za Ubalozi huo katika kuhakikisha vivutio vya utalii vinatangazwa nchini India kupitia mawakala hao.

Kwa upande wake, kiongozi wa ujumbe wa Mawakala hao ambaye pia ni Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha shughuli za Utalii cha India, Bw. Himanshu Patil amesema kuwa lengo la ziara yao hapa nchini ni kujionea vivutio vya utalii na kuzungumza na wadau muhimu katika sekta hiyo ili hatimaye kuwawezesha kushirikiana na Tanzania katika kuwafikia watalii kutoka India kuja nchini.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo, mawakala hao walipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo ya kibiashara (B2B) na kundi la waendesha shughuli za utalii (Tour Operators) kutoka Tanzania. Mkutano huo ulilenga kujenga mahusiano ya kibiashara ya moja kwa moja na kufungua fursa mpya za kukuza idadi ya watalii kutoka soko la India.

Ziara hii ni sehemu ya mkakati endelevu wa Bodi ya Utalii Tanzania wa kukuza soko la India ambalo kwa sasa ni miongoni mwa masoko sita yanayoongoza kwa kuleta watalii nchini. 

Wakiwa nchini Mawakala hao watatembelea maeneo mbalimbali ya utalii yakiwemo Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Zanzibar.

Waajiri watakiwa kutatua changamoto za watumishi – HabariLeo

SIMANJIRO. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, amewataka waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhakikisha changamoto za kiutumishi zinashughulikiwa kwa wakati ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Qwaray ametoa agizo hilo wakati wa kikao kazi cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.

Amesema waajiri wanapaswa kuhakikisha stahiki za watumishi, ikiwemo kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao, zinashughulikiwa kwa wakati kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Aidha, amesisitiza kuwa madai ya watumishi yanapaswa kuhakikiwa na kuwasilishwa yakiwa yameambatanishwa na nyaraka muhimu ili kurahisisha utatuzi wa changamoto hizo.

Qwaray amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kusimamia haki na wajibu wa watumishi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, akisisitiza umuhimu wa kuacha utendaji wa mazoea.

Amesema mambo yaliyo ndani ya uwezo wa waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu yanapaswa kushughulikiwa katika ngazi hizo badala ya kuendelea kuwasilishwa Ofisi ya Rais.

Kuhusu maadili ya utumishi wa umma, Qwaray amewataka watumishi kuyafahamu na kuyatekeleza kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Watumishi wanaokiuka maadili au kutotekeleza majukumu yao ipasavyo wanapaswa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu kwa wakati,” amesema.

Aidha, amewataka waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kushirikiana na Tume ya Utumishi wa Umma katika ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi na kuhakikisha mapungufu yatakayobainika yanarekebishwa kwa wakati.

Qwaray atoa maagizo kero za wananchi – HabariLeo

Cheza, Panda Kwenye Msimamo na Ushinde Milioni 5

Global Publishers
September 30, 2026
48 views
0 Comments

Burudani mpya imefika kwa wapenzi wa Kasino Meridianbet. Ni Cash Storm Tournament kutoka Expanse, mashindano yanayokupa wiki mbili za burudani mfululizo za kasino kuanzia Septemba 26 hadi Oktoba 8, 2026. Sasa ni wakati wa kuchagua sloti yako inayoshiriki na kuanza safari ya kuwania nafasi nzuri kwenye msimamo.

Kuanza ni rahisi zaidi kuliko unavyofikiria. Kwa kiasi cha kuanzia Tsh. 500 kwa mzunguko, chagua mchezo unaoupenda na anza kucheza. Kila unaposhiriki, pointi zako zinaendelea kukusanywa na kukusaidia kufuatilia safari yako kwenye msimamo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Na safari hii ina zawadi kubwa mwisho wake. Jumla ya Tsh. 5,000,000 imetengwa kwa ajili ya wachezaji 20 bora. Hivyo, kila mchezaji ana nafasi ya kufuatilia nafasi yake wakati mashindano yakiendelea na kuona namna anavyosogea kwenye orodha ya washiriki.

Cash Storm imeleta sababu nyingine ya kufurahia sloti kupitia Meridianbet. Ni wiki mbili za mpambano wa kasino, ushindani wa msimamo na nafasi ya kuwania sehemu ya zawadi kubwa. Chagua mchezo wako, ingia kwenye mashindano na uendelee kufuatilia safari yako hadi siku ya mwisho.

Meridianbet ndiyo sehemu ya kuanzia safari ya Cash Storm. Anza kucheza kuanzia Tsh. 500, kusanya pointi zako na fuatilia msimamo hadi Oktoba 8, 2026. Tsh. 5,000,000 inasubiri wachezaji 20 bora, chagua sloti yako na uanze safari leo.