WAFANYABIASHARA WA LIBRARY ZA VIDEO IRINGA WATISHIA KUTOFANYA KAZI NA UMOJA MOVIES

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

UMOJA wa wafanyabiashara wa filamu maarufu kama Library za Video mkoani Iringa umeazimia kusitisha kwa muda kufanya kazi na kampuni ya Umoja Movies, ili kutoa nafasi kwa viongozi na wawakilishi wa wadau kukutana na kampuni hiyo kujadili changamoto zinazodaiwa kujitokeza katika mfumo mpya wa usambazaji wa kazi za filamu.

Akizungumza na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Library Mkoa wa Iringa, Joshua Sanga  amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau kuhusu mfumo mpya uliowekwa na kampuni hiyo, hivyo kuna umuhimu wa pande zote kukutana na kutafuta suluhisho.

Sanga alisema moja ya hoja zinazohitaji ufafanuzi ni suala la usalama wa mfumo huo, hususan namna unavyolinda kazi pamoja na taarifa zilizohifadhiwa katika kompyuta za watumiaji.

Kwa mujibu wa Sanga  wafanyabiashara wanahitaji kupewa maelezo ya kutosha kuhusu mfumo huo na namna unavyofanya kazi kabla ya kuanza kuutumia kwa kiwango kikubwa.

Alisema ni muhimu kampuni kuwashirikisha wadau wanaotumia mfumo moja kwa moja kabla ya kuanzisha mabadiliko makubwa, ili kupata maoni yao na kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza kabla ya utekelezaji kamili.

Mwenyekiti huyo amesema wafanyabiashara wa filamu na kampuni wanapaswa kukaa pamoja na kujadiliana ili kubaini namna mfumo huo utakavyoweza kuwa na manufaa kwa pande zote.

“Umoja Movies inafanya biashara kwa lengo la kupata mapato, huku wadau nao wakitegemea kazi hizo kama chanzo cha kipato, hivyo ni muhimu kuwepo kwa usawa wa maslahi,” amesema.

Ameongeza kuwa wamependekeza utekelezaji wa mfumo huo usitishwe kwa muda ili kutoa nafasi kwa viongozi na wawakilishi wa wafanyabiashara kufanya mazungumzo na kampuni.

“Kuanzia sasa napendekeza kampuni kusitisha utekelezaji wa mfumo huo kwa muda ili kutoa nafasi kwa viongozi na wawakilishi wa wadau kukutana na kampuni na kujadili kwa kina changamoto zilizopo pamoja na namna bora ya kuendesha mfumo huo,” amesema.

Sanga alisema iwapo kampuni itaendelea na mfumo huo bila kufikiwa kwa makubaliano, umoja huo utaangalia njia nyingine zitakazowawezesha wanachama wake kuendelea kufanya kazi na kujipatia kipato.

Amefafanua kuwa hatua hiyo hailengi kuvunja ushirikiano uliopo, bali inalenga kuhakikisha maslahi ya wafanyabiashara na wadau wengine katika sekta hiyo yanazingatiwa.

Amesisitiza kuwa umoja huo una malengo ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa filamu pamoja na kuibua fursa kwa vijana wenye vipaji na wanaotegemea biashara hiyo kama chanzo cha ajira na kipato.

Amesema Mkoa wa Iringa una vijana wengi wenye uwezo na vipaji ambao wanahitaji mazingira rafiki ya kuendeleza shughuli zao na kujipatia kipato.

“Nawaomba wanachama tuendelee kushikamana na kuwa na sauti moja katika masuala yanayotuhusu, kwa sababu umoja ndio msingi wa kupata suluhisho la changamoto zetu. Kupitia ushirikiano huo tunaweza kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ya filamu na kuhakikisha sekta hiyo inanufaisha pande zote,” amesema.

Kwa upande wake, Katibu wa Wafanyabiashara wa Library za Video, Erick Mushi, amesema baadhi ya watumiaji wamedai kukumbana na changamoto za kiufundi katika matumizi ya mfumo huo, ikiwemo kutofanya kazi kwa ufanisi katika baadhi ya kompyuta zinazotumia matoleo tofauti ya mfumo wa Windows.

Mushi amesema changamoto hizo zimejitokeza baada ya mfumo kuanza kutumika, hivyo wameomba kupewa muda wa kutosha kuujifunza, kuufanyia majaribio na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kabla ya utekelezaji wake kwa kiwango kikubwa.

Amesema wanaamini mazungumzo kati ya kampuni na wafanyabiashara yanaweza kusaidia kupata suluhisho litakalolinda maslahi ya pande zote na kuwezesha biashara ya filamu kuendelea katika mazingira mazuri.TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Msiba Kibaha: Polisi Wawili Wapoteza Maisha Kwa Kugongwa na Gari, Waagwa Tumbi

Pwani. Jeshi la Polisi limewapoteza askari wake wawili katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Maili Moja, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, baada ya kugongwa na gari wakati wakiwa katika eneo la kivuko cha watembea kwa miguu.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Agosti 25, 2026, majira ya saa 1:40 katika barabara kuu ya Dar es Salaam–Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T.804 ERM, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mlandizi, liliwagonga watembea kwa miguu katika eneo la zebra.

Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Josia Isaya Arute, mwenye umri wa miaka 34, mkazi wa Mlandizi.

Inadaiwa kuwa wakati dereva huyo akifika katika eneo hilo, magari kadhaa yalikuwa yamesimama ili kuwawezesha watembea kwa miguu kuvuka. Hata hivyo, gari hilo lilipita upande wa magari hayo na kuwagonga waliokuwa wakivuka.

Miongoni mwa waliogongwa walikuwa askari wawili wa Polisi, Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa.

Izdory alifariki dunia kutokana na ajali hiyo, wakati Rehema alipata majeraha kichwani na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi kwa ajili ya matibabu.

Kwa bahati mbaya, Rehema alifariki dunia asubuhi ya Agosti 26, 2026, wakati akiendelea kupata matibabu.

Baada ya ajali, dereva wa gari hilo aliondoka katika eneo la tukio. Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanya msako na kulifanikiwa kulikamata gari hilo katika eneo la Kwa Mfipa, Kibaha, likiwa limefichwa.

Gari hilo limepelekwa Kituo cha Polisi Kibaha kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi za kisheria.

Askari hao wameagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi kabla ya kusafirishwa kwenda mikoani kwa ajili ya mazishi.

Ibada hiyo ya kuaga imeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, na kuhudhuriwa na askari wa vyeo mbalimbali pamoja na ndugu na waombolezaji.

Mwili wa Rehema Juma Magawa umepelekwa Korogwe, Tanga, huku mwili wa Izdory George Michael ukisafirishwa kwenda Sumbawanga Vijijini, Rukwa, ambako mazishi yao yatafanyika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeendelea kutoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuheshimu alama za barabarani, hususan maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu, ili kuepusha vifo na majeraha yanayotokana na ajali.

Msiba Kibaha: Polisi Wawili Wapoteza Maisha Kwa Kugongwa na Gari, Wameagwa Tumbi

Msiba Kibaha: Askari Wawili wa Polisi Wapoteza Maisha Kwa Ajali ya Gari

Miili ya askari yaagwa Tumbi

Leo, Agosti 26, miili ya askari hao imeagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi kabla ya kusafirishwa kwenda mikoani kwa ajili ya mazishi.

Ibada hiyo ya kuaga imeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, na kuhudhuriwa na askari wa vyeo mbalimbali pamoja na ndugu na waombolezaji.

Mwili wa Rehema Juma Magawa umepelekwa Korogwe, Tanga, huku mwili wa Izdory George Michael ukisafirishwa kwenda Sumbawanga Vijijini, Rukwa, ambako mazishi yao yatafanyika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeendelea kutoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuheshimu alama za barabarani, hususan maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu, ili kuepusha vifo na majeraha yanayotokana na ajali.

Meridianbet yawasha moto, TSh milioni 75 zawikwa kwenye Prize Drops

Meridianbet imewasha moto wa zawadi kupitia Rewards Burst Prize Drops, promosheni inayowapa wachezaji nafasi ya kunasa zawadi za papo hapo wakati wa kushiriki mchezo unaokidhi vigezo. Hapa, kila raundi inaweza kubeba sapraizi mpya, kuanzia zawadi za fedha taslimu hadi vizidishi vinavyoweza kufika mbali.

Kile kinachovutia zaidi ni nafasi ya kushinda hadi TSh 75,000,000 kama zawadi kuu. Kila mwezi, mchezaji mmoja anaweza kuchaguliwa kwa bahati na kutwaa zawadi hiyo kubwa. Lakini fursa hazipo kwa mshindi huyo pekee, maelfu ya zawadi hutolewa kila mwezi, huku wachezaji wakiwa na nafasi ya kupata vizidishi kila siku kuanzia x5 hadi x1,000.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa mfano, mchezaji anayecheza dau la TSh 600 na kupata kizidishi cha x500 anaweza kupata TSh 300,000. Hii inatokana na hesabu ya dau linalokidhi masharti wakati Prize Drop inapotolewa, na kiwango cha juu cha dau kinachozingatiwa ni TSh 3,000. Kwa hiyo, unapokutana na kizidishi kikubwa, dau linalostahili linaweza kuleta zawadi yenye tofauti kubwa.

Kuingia kwenye promosheni ni rahisi na hakuna safari ndefu. Ingia kwenye akaunti yako, weka dau linalostahili, chagua mchezo unaoshiriki na cheza. Kisha, bahati ndiyo itaamua kama Prize Drop itatua kwako. Kwa kuwa zawadi zinapatikana kila siku na maelfu ya zawadi zipo kila mwezi, kila raundi inayokidhi masharti inaweza kuwa mwanzo wa sapraizi nyingine.

Uko tayari kuona Burst ya zawadi? Basi usiache nafasi ipite. Rewards Burst Prize Drops inakupa nafasi ya kuwania zawadi kuu ya TSh 75 milioni, huku vizidishi vikifikia x1,000.

Real Madrid na Sociedad Kukutana, Macho yote Santiago Bernabéu

Je unajua kuwa siku ya leo unaweza ukaondoka na kitita cha mkwanja wa maana ukibashiri mechi zako sasa. Mechi nyingi kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huku wewe kwa dau dogo tuu unaibuka bingwa.

Tukianza na kule Hispania, LALIGA itaendelea kwa mchezo mmoja kati ya Real madrid dhidi ya Real Sociedad ambapo hii ni mechi ya pili wao kucheza toka ligi ianze na kule Meridianbet wanampa nafasi kubwa ya kushinda mwenyeji pale Bernabeu.

Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa Real Madrid kwa sababu ni moja ya mechi za mwanzo kabisa za José Mourinho katika kurejea kwake Santiago Bernabéu. Madrid wanaingia kwenye msimu huu wakiwa na dhamira kubwa ya kurejesha ubingwa wa La Liga baada ya kukosa mataji makubwa katika misimu miwili iliyopita.

Mourinho ameleta mtazamo tofauti nidhamu, mpangilio wa timu na uimara wa ulinzi. Mfumo wake unatarajiwa kuipa Madrid muundo bora zaidi bila mpira, jambo ambalo litakuwa muhimu hasa dhidi ya timu kama Sociedad inayopenda kuzungusha mpira na kushambulia kwa mipango.

Madrid pia wameanza msimu kwa kujiamini. Walishinda 2-1 dhidi ya Espanyol katika mchezo wao wa kwanza wa ligi, huku pre-season yao ikiwa na matokeo mazuri kwa ujumla.

Je vijana hawa wa Bernabeu wanaweza kuondoka na ushindi wakiwa nyumbani kwao?. Odds kubwa zipo kwenye mechi hii sasa.

Tengeneza pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini pia leo leo kutakuwa na mechi za kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) inaendelea huku macho yote yakiwa kwenye mechi ya Lyon dhidi ya Fenerbahçe ambapo kila timu inahitaji ushindi siku ya leo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano hii mikubwa Duniani.

Hii ni mechi ya marudiano na mechi ya maamuzi ya kuamua nani ataenda kucheza UEFA mechi ambazo zinatarajiwa kuanza mwezi ujao, ambapo mtanange wa kwanza walipokutana walitoka sare ya kufungana bao 1-1 huku sasa kila timu ikiwa imejipanga vyema kufanya vizuri. Jisajili hapa.

Lyon wao wameonyesha kwamba wana uwezo wa kubadilisha matokeo wanapocheza nyumbani. Katika raundi iliyopita dhidi ya Sparta Prague, walipoteza 2-1 ugenini lakini wakashinda 3-0 nyumbani, na hivyo kugeuza kabisa mwelekeo wa mchuano.

Kwa upande wa kiufundi, Corentin Tolisso ni mmoja wa wachezaji muhimu kwa Lyon katika eneo la kiungo. Uwezo wake wa kusoma mchezo, kupandisha mpira mbele na kuingia karibu na eneo la hatari unaweza kuwa muhimu sana. Katika mchezo wa kwanza Istanbul, pasi yake ilisaidia Lyon kupata bao lao. Beti hapa.

Nao Fenerbahçe wana kikosi chenye uzoefu mkubwa. Miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi chao ni N’Golo Kanté, Matteo Guendouzi, Talisca, Nathan Aké na Mason Greenwood. UEFA inaonyesha kwamba Talisca amefunga katika kila moja ya mechi nne za Fenerbahçe kwenye kampeni yao ya Champions League msimu huu, jambo linaloonyesha umuhimu wake katika safu ya mbele.

Rais Samia Akutana na Kamati Kuu ya CCM Katika Kikao Maalum Dar

Global Publishers
August 26, 2026
42 views
0 Comments

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar Es Salaam leo, Jumatano tarehe 26 Agosti 2026.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano, Agosti 26, 2026, ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho maalum kimefanyika jijini Dar es Salaam huku kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho ni sehemu ya shughuli za chama zinazofanywa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama.

Taarifa zaidi kuhusu ajenda na maazimio ya kikao hicho zitatolewa na CCM endapo kutakuwa na taarifa rasmi kuhusu yaliyofikiwa katika kikao hicho.

Kesi ya Uhaini: Lissu Akabiliana na Maswali ya Upande wa Jamhuri

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameanza kukabiliana na maswali ya upande wa Jamhuri baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake mkuu katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Dodoso hilo limeanza baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuahirisha mwenendo wa kesi kwa muda wa saa moja na nusu baada ya Lissu kukamilisha ushahidi wake wa msingi.

Mawakili wa upande wa Jamhuri, wakiongozwa katika hatua hiyo na Nassoro Katuga, wameanza kumuuliza Lissu maswali mbalimbali yanayohusu ushahidi alioutoa mbele ya jopo la majaji watatu.

Mwanzoni mwa dodoso hilo, Katuga alimpongeza Lissu kwa ushahidi mrefu alioutoa kabla ya kumtaka athibitishe kuwa anafahamu kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa kisheria.

Lissu alikubaliana na kauli hiyo, akisisitiza kuwa yeye ni wakili wa Mahakama Kuu na ana uelewa wa sheria.

Nassoro Katuga: Shahidi pole na ushahidi mrefu

Lissu: Ahsante sana

Katuga: Kama nimekusikia vyema ulisema utatuacha sisi ndugu zako tukuulize maswali.

Lissu: Sahihi.

Katuga: Waambie majaji hiki tunachokifanya ni kitu cha kisheria na hakina nasaba nyingine yeyote.

Katuga: Uliiambia mahakama wewe ni wakili wa mahakama kuu na una ujuzi wa kisheria.

Lissu: Ndio

Katuga: Hebu waambie majaji Tanzania ilipata uhuru mwaka gani.

Lissu: 9/12/1961

Katuga: Kwa majibu hayo Tanzania ni nchi huru.

Lissu: Ndio

Katuga: Chombo cha mwisho cha kufanya maamuzi ya mwisho kwa mujibu wa kisheria ni ni kipi?

Lissu: Mahakama

Katuga: Mahakama haitakiwi kuingiliwa na mtu yeyote inapotoa maamuzi na pia mahakama hailazimishwi wala haipingwi na mtu au chombo chochote toka nje au ndani.

Lissu: Sahihi haipangiwi walakulazimishwa.

Katuga: Umetuambia wewe ni Mwenyekiti wa Chadema, Je katika utetezi wako umeimbia mahakama hii kuwa mwenyekiti wa Chadema ana kinga?

Lissu; Hapana na sina kinga hiyo

Katuga: Ndugu shahidi kama nilikupata vyema ulieleza sifa nyingi kukuhusu wala sizikatai iambie mahakama hizi tuzo ulizopewa ziko kwenye form gani kama maandishi au katika hali gani.

Lissu: Ziko katika hali ya maandishi, na ile alama yenyewe

Katuga: Ka object flani hivi.

Lissu: Ndio

Katuga: Embu iambie haya matuzo yote haya umeyaleta mahakamani

Lissu: Hapana na sina sababu ya kuyaleta.

Katuga: Twende pole pole tutakuwa na siku saba hapa.

Lissu: Hakuna neno

Katuga: Wewe umeleta nini hapa

Lissu: Maneno

Katuga: Sasa wewe uliposema mashahidi wa jamuhuri wameleta meneno ulimaanisha nini?

Lissu: Siwajibiki kufanya hivyo mimi nimeleta maneno sababu sina kesi ya kuthibitisha

Katuga: Sheria inasemaje?

Lissu: Sheria inataka mtu alete ushahidi pamoja na vithibitisho

Katuga: Unajua usilete ujuaji

Lissu: Yes mimi mjuaji

Katuga: Principles gani zinakutaka ulete maneno bila vithibitisho?

Lissu: Mimi sina wajibu wa kuthibitisha lolote.

Katuga: Unajua kifungu cha sheria kinasema yule anasema ana wajihi fulani anapaswa kuthibitisha.

Lissu: Ndio ninathibitisha

Katuga: Ulisema mahakama ni chombo huru wale uliosema wameelekeza uachiwe na unakubali mahakama ni chombo huru ndani ya nchi huru ya Tanzania?

Lissu: Ndio, Kamati ya haki za binadamu ya Umpja wa Mataifa

Katuga: Shahidi kuna mahali popote kwenye ushahdi wako kuna umekanusha maneno haya ya tunakwenda kukinukisha kweli kweli?

Lissu: Nimesema hivi maneno hayo ukitaka kuyaelewa unabidi usikilize hotuba yote.

Katuga: Mimi siwezi kukuuliza una akili timamu wewe ni kaka yangu

Lissu: Niulize tu

Katuga: Siwezi swali langu kuna mahali umekanusha maneno haya

Lissu: Hapana

Katuga: Kwa maana hiyo maneno haya huyakatai

Lissu: Siyakatai wala hayana shida.

Katuga: Nilitaka tu hicho

Lissu: Nimesema mara kadhaa.

Harmonize Afichua Wasanii Walio kwenye Albamu Yake Mpya “31”

Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, ameweka wazi orodha ya nyimbo zitakazopatikana katika albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la “31”, ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameshirikisha mashabiki wake orodha ya nyimbo 14 zitakazounda albamu hiyo, huku akitangaza kuwa inatarajiwa rasmi kutoka Septemba 4, 2026.

Albamu hiyo imebeba ushirikiano mbalimbali kutoka kwa wasanii wakubwa ndani na nje ya Tanzania, akiwemo Marioo, Young Lunya, Jay Melody, Mayorkun, Darkoo, Yemi Alade, Rayvanny na Sofia Nzau, pamoja na wasanii wengine.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, Harmonize anatarajiwa kuendelea kuonyesha uwezo wake wa kuunganisha muziki wa Bongo Fleva na ladha mbalimbali za kimataifa kupitia nyimbo zitakazopatikana kwenye albamu hiyo.

Harmonize, ambaye ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa kujenga jina kubwa katika muziki wa Tanzania, tayari ameachia albamu kadhaa zilizofanya vizuri, zikiwemo “Afro East” iliyotoka mwaka 2020, “High School” mwaka 2021 na “Made For Us” mwaka 2022.

Kwa sasa, Harmonize anaendelea kufanya vizuri kupitia wimbo wake “Beautiful”, ambao pia umejumuishwa katika albamu mpya ya “31”.

Albamu hiyo inatarajiwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa ya Harmonize kwa mwaka huu, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona namna atakavyowasilisha kazi hizo mpya pamoja na ushirikiano wa wasanii mbalimbali.

Stori na Na Didas Didas | GPL