Ngoma ya “Buku Jero” ya Mbosso Yawateka Mashabiki

Msanii wa muziki wa Tanzania, Mbosso, amezidi kuwateka mashabiki kupitia ngoma yake mpya “Buku Jero,” ambayo imeibuka kuwa miongoni mwa nyimbo zinazozungumziwa na kupokelewa kwa hamasa kutokana na ladha yake ya kipekee na ujumbe unaogusa maisha ya kila siku.

“Buku Jero” ni ngoma yenye mdundo wenye nguvu inayochota msukumo kutoka kwenye maisha halisi ya Watanzania, huku ikitumia lugha ya mtaani, vichekesho na misemo inayofahamika katika jamii.

Jina la ngoma hiyo limechochewa na kauli maarufu “buku jero,” inayohusishwa na kiasi cha Sh1,500, na Mbosso analitumia kama sehemu ya kuwasilisha simulizi kuhusu maisha, hustle, urafiki na namna watu wanavyokabiliana na changamoto za kila siku.

Kwa upande mwingine, ngoma hiyo inaonyesha namna watu wanavyoungana na kushirikiana katika safari ya maisha. Mbosso anagusa pia upande wa burudani na maisha ya usiku, ambapo marafiki hukutana, kufurahi na kusahau kwa muda presha za maisha.

Licha ya kuwa na ladha ya burudani na vionjo vya kuchezeka, “Buku Jero” imebeba ujumbe unaokwenda zaidi ya starehe. Inasisitiza umuhimu wa mtu kuwa makini na maisha yake, kujitegemea na kuendelea kumtegemea Mungu katika kila hatua ya safari yake.

Moja ya sehemu zinazogusa hisia zaidi ni ujumbe unaomhusu mama, ambapo badala ya kuomba utajiri, mama anaweka mkazo kwenye maisha, usalama na mustakabali wa mtoto wake.

Ujumbe huo unaonyesha kuwa katika maisha, upendo wa familia, imani na dua za wazazi vina thamani kubwa kuliko fedha.

Kwa kutumia lugha halisi ya mtaani, vionjo vya kitamaduni na kiitikio kinachoshika kwa urahisi, “Buku Jero” imejenga picha ya maisha ya Mtanzania wa kawaida kuanzia kwenye harakati za kutafuta maisha hadi muda wa kujiburudisha na marafiki.

Zaidi ya kuwa ngoma ya starehe, “Buku Jero” ni simulizi linalogusa urafiki, kujituma, uvumilivu, familia na imani, huku likisisitiza kuwa furaha ya kweli haipimwi kwa kiasi cha fedha kilichopo mfukoni, bali kwa watu wanaokuzunguka na namna unavyokabiliana na safari ya maisha.

Mbosso kupitia ngoma hiyo ameendelea kuonyesha uwezo wake wa kuchanganya burudani na simulizi za maisha halisi, jambo linalofanya muziki wake kuendelea kuwafikia mashabiki wa kizazi tofauti.

Mtangazaji TV Ahukumiwa Kunyongwa Pamoja na Washtakiwa Wengine 11

Global Publishers
September 7, 2026
72 views
0 Comments

CAIRO, Misri — Mtangazaji na mtayarishaji wa vipindi vya televisheni nchini Misri, Sarah Khalifa, mwenye umri wa miaka 39, amehukumiwa kifo kwa kunyongwa pamoja na washtakiwa wengine 11 katika kesi kubwa ya dawa za kulevya iliyofikishwa katika Mahakama ya Jinai ya Cairo.

Khalifa anafahamika zaidi kwa kuendesha kipindi cha televisheni “Mission Impossible”, kilichokuwa kikijikita katika masuala ya uhalifu na usalama.

Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, Khalifa na washtakiwa wenzake walipatikana na hatia ya kuunda mtandao wa uhalifu uliopangwa, uliodaiwa kujihusisha na uingizaji wa malighafi zilizotumika kutengeneza dawa za kulevya kwa ajili ya biashara.

Washtakiwa hao pia walikabiliwa na makosa mengine yanayohusiana na umiliki wa silaha na risasi bila leseni.

Mamlaka nchini humo ziliripoti kuwa wakati wa uchunguzi wa kesi hiyo, zilikamata zaidi ya kilo 750 za dawa za kulevya na malighafi, huku maeneo mawili yakidaiwa kutumika kama maabara za kutengeneza dawa hizo.

Kesi hiyo ilikuwa na washtakiwa 28 kwa jumla. Kati yao, watu 12 wamehukumiwa kifo, huku wengine tisa wakihukumiwa kifungo cha maisha na saba kuachiwa huru.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya mahakama kupata maoni ya Mufti Mkuu wa Misri, hatua inayohitajika katika kesi zinazoweza kupelekea hukumu ya kifo nchini humo.

Hata hivyo, hukumu hiyo bado inaweza kukatiwa rufaa kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Sarah Khalifa amekuwa akikanusha kuhusika na tuhuma hizo. Wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, mtangazaji huyo aliendelea kusisitiza kuwa hana hatia.

STORI NA TEREZA MUGA | GPL-TUDACO

Sababu 7 Zinazofanya Ndizi Mbivu Kuwa Tunda Bora kwa Afya

Global Publishers
September 7, 2026
3,752 views
0 Comments

Ndizi mbivu ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa urahisi na yanayopendwa na watu wengi kutokana na ladha yake tamu pamoja na virutubisho muhimu vinavyopatikana ndani yake. Mbali na kuwa chanzo kizuri cha nishati, ndizi mbivu zina faida mbalimbali za kiafya zinazoweza kusaidia kuboresha ustawi wa mwili.

1. Hutoa Nishati kwa Haraka
Ndizi mbivu zina kiwango kizuri cha wanga na sukari asilia ambazo mwili huzitumia kuzalisha nguvu. Hii ndiyo sababu ndizi hupendekezwa kwa watu wanaofanya mazoezi, wanafunzi na watu wenye shughuli nyingi za kila siku.

2. Husaidia Mfumo wa Mmeng’enyo wa Chakula
Ndizi zina nyuzinyuzi (fiber) zinazosaidia kuboresha usagaji wa chakula tumboni. Ulaji wa ndizi unaweza kusaidia kupunguza tatizo la kufunga choo na kusaidia mfumo wa mmeng’enyo kufanya kazi vizuri.

3. Huchangia Afya Bora ya Moyo
Madini ya potassium yaliyomo kwenye ndizi husaidia kudhibiti shinikizo la damu na kusaidia moyo kufanya kazi kwa ufanisi. Ulaji wa ndizi kwa kiasi unaweza kuwa sehemu ya lishe inayosaidia afya ya moyo.

4. Huimarisha Afya ya Misuli
Potassium pia ni muhimu katika utendaji wa misuli. Kula ndizi kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata maumivu ya misuli au kukakamaa hasa baada ya kufanya shughuli nzito za mwili.

5. Huboresha Hali ya Moyo na Hisia
Ndizi zina virutubisho vinavyosaidia mwili kuzalisha serotonin, kemikali inayohusishwa na hisia za furaha na utulivu. Hii inaweza kusaidia kuboresha hali ya moyo kwa baadhi ya watu.

6. Huimarisha Kinga ya Mwili
Ndizi zina vitamini na madini mbalimbali yanayosaidia mwili kupambana na magonjwa na kuimarisha mfumo wa kinga.

7. Husaidia Kudhibiti Hamu ya Kula
Kutokana na kuwa na nyuzinyuzi nyingi, ndizi husaidia mtu kushiba kwa muda mrefu zaidi, jambo ambalo linaweza kusaidia kudhibiti ulaji wa vyakula kupita kiasi.

Ndizi mbivu ni tunda lenye virutubisho vingi na faida mbalimbali kwa afya ya mwili. Zinasaidia kuongeza nguvu, kuboresha mmeng’enyo wa chakula, kuimarisha afya ya moyo na misuli pamoja na kusaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa. Kuingiza ndizi katika mlo wa kila siku kwa kiasi kinachofaa kunaweza kuwa hatua muhimu katika kuimarisha afya kwa ujumla.

Dereva wa Basi Akamatwa Mwanza kwa Tuhuma za Kuchati Akiwa Anaendesha – Video

Global Publishers
September 6, 2026
408 views
0 Comments

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Sabatho Malima Emmanuel, mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Buswelu, Wilaya ya Ilemela, ambaye ni dereva wa basi la Kampuni ya Obadia lenye namba za usajili T 870 DVW, aina ya Yutong.

Dereva huyo anakabiliwa na tuhuma za kuendesha gari kwa uzembe na kuhatarisha maisha ya abiria pamoja na watumiaji wengine wa barabara, baada ya kudaiwa kuwa alikuwa akichati kwa simu huku akiendesha gari.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo lilitokea Septemba 5, 2026, majira ya saa 6:40 mchana, katika eneo la Isangijo, Wilaya ya Magu, barabara ya Mwanza–Musoma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa dereva huyo alikuwa akiendesha basi hilo akitokea Nyamongo kuelekea Mwanza, huku akichati kwa simu kuanzia eneo la Lamadi, mkoani Simiyu.

Aidha, dereva huyo anadaiwa kutoa lugha chafu kwa watumiaji wengine wa barabara, kitendo ambacho Jeshi la Polisi limesema ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani na usafirishaji.

Polisi imesema kitendo hicho kilihatarisha maisha ya abiria waliokuwa ndani ya basi pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Wacky Panda Mania Yaingia Meridianbet na Kuleta Burudani Mpya

Global Publishers
September 6, 2026
48 views
0 Comments

Panda wameingia mjini na hawajaja kutafuta mianzi. Safari hii wamefika Meridianbet wakiwa na lengo moja, kuleta burudani mpya ya kasino kupitia Wacky Panda Mania, mchezo kutoka Games Global. Mchezo huu umebeba mchanganyiko wa furaha, raundi zenye msisimko na zawadi zinazoweza kufanya kila mzunguko kuwa wa kusubiriwa kwa hamu. Ni ujio mpya unaowaleta wapenzi wa kasino kwenye ulimwengu wa panda wenye njia za ushindi.

Kila raundi inapoanza kuzunguka, safari inaanza. Kila mzunguko unakuja na hali yake, huku alama zikijipanga na panda wakiendelea kutawala mazingira ya mchezo. Huwezi kujua kitakachotokea kabla mzunguko haujasimama, na hilo ndilo linaloongeza ladha ya kusisimua. Raundi moja inaweza kuwa tulivu, inayofuata ikaleta ushindi na kubadilisha kabisa mwendo wa mchezo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kupitia Meridianbet, unaweza kugundua burudani hii mpya kutoka Games Global na kuingia kwenye mchezo wa kipekee uliojaa zawadi za kila aina na fursa kubwa ya ushindi unaopatikana ndani ya Wacky Panda Mania. Mchezo umeundwa kwa mtindo unaolenga kuleta furaha na msisimko, huku panda wakiwa katikati ya kila kinachoendelea. Ni kama umefungua mlango wa ulimwengu ambao kila raundi inapochezwa, kuna jambo jipya la kutazamia.

Kwa hiyo, kama umekuwa ukisubiri mchezo mpya wa kuongeza ladha kwenye burudani yako ya kasino, Wacky Panda Mania imefika Meridianbet. Panda wamejiandaa, mchezo upo tayari na safari ya Mania inakusubiri wewe kuanza. Ingia Meridianbet, gundua siri za mchezo huu na uone ni kwa nini panda hawa wamekuja na vurugu ambazo huwezi kuzipuuza.

Valencia Yachapwa 5-0, Barcelona Yaendelea Kuwasha Moto La Liga

Global Publishers
September 6, 2026
30 views
0 Comments

BARCELONA, Hispania — FC Barcelona imeendelea na mwanzo wake bora wa msimu baada ya kuichapa Valencia CF mabao 5-0 katika mchezo wa La Liga uliochezwa kwenye Uwanja wa Mestalla.

Barcelona ilianza mchezo kwa kasi, huku Lamine Yamal akifungua akaunti ya mabao dakika ya 6 na kuiweka Barcelona mbele.

Fermín López aliongeza bao la pili dakika ya 22, kabla ya Raphinha kufunga la tatu dakika ya 50 na kuifanya Barcelona kuzidi kuutawala mchezo.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa cha Barcelona, ambapo Pedri alifunga bao la nne dakika ya 79. Yamal akakamilisha siku yake nzuri kwa kufunga bao lake la pili dakika ya 84, na kuipa Barcelona ushindi mnono wa 5-0.

Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi 12 kati ya 12 kwenye mechi nne za mwanzo za La Liga, ikiwa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya mabao.

Barcelona sasa imefunga mabao 17 na kuruhusu mawili pekee katika mechi hizo nne, ikionyesha uwezo mkubwa katika safu ya ushambuliaji na uimara wa ulinzi.

Chini ya kocha Hansi Flick, Barcelona imeendelea kuonyesha kiwango cha kuvutia, huku Lamine Yamal akiwa miongoni mwa wachezaji walioangaza zaidi katika ushindi huo baada ya kufunga mabao mawili.

Ushindi dhidi ya Valencia unaipa Barcelona mwendelezo mzuri wa kampeni yake ya La Liga, huku kikosi hicho kikionekana kuendelea kujiimarisha katika mbio za kutetea taji.

STORI NA DIDAS DIDAS| GPL – TUDACO

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 6, 2026
1,278 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

👉 Piga kura kupitia:
https://samiaawards.tz/mshiriki/260246

📌 Copy link hiyo kisha paste kwenye browser yako ili kumpigia kura.

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

#SamiaKalamuAwards #VoteForGodmuya #Godmuya #GlobalTVOnline #255GlobalRadio

Vita Kali Serie A, LaLiga na EPL Kitawaka leo Jumapili, Juventus vs Milan, Arsenal vs Chelsea

Je unajua kuwa wikendi iliyopita kuna watu wameweza kubadili maisha yao kwa dau dogo kabisa la shilingi mia tano?. Huenda leo ikawa ni nafasi yako na wewe na unachotakiwa kufanya ni kutengeneza jamvi lako na ubeti sasa.

Kule SERIE A kuna mechi zitaendelea, lakini mechi kali ni hii ya Juventus vs AC Milan mchezo ambao tayari umebeba uzito mkubwa kwa sababu timu zote mbili zimeanza ligi kwa ushindi wa asilimia 100.

Juventus wamefungua msimu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Frosinone na 2-0 dhidi ya Parma, huku Milan wakiwashinda Torino 2-1 na Venezia 2-0. Hivyo, hii ni vita ya timu mbili ambazo bado hazijapoteza pointi.

Bibi Kizee wanaonekana kuwa na mwanzo wenye utulivu zaidi upande wa ulinzi. Katika mechi zao mbili za kwanza hawajaruhusu bao lolote, jambo linaloonyesha nidhamu ambayo kocha Luciano Spalletti ameanza kuijenga. Ushindi wa 2-0 dhidi ya Parma pia ulionyesha kwamba Juventus wanaweza kupata tofauti kupitia wachezaji wanaotokea benchi, baada ya Nico González na Teun Koopmeiners kuamua mchezo.

Wakati  AC Milan, wao mwanzo wao pia umeleta matumaini makubwa. Ushindi dhidi ya Torino na Venezia umeonyesha kwamba kikosi kinaweza kupata matokeo hata kama hakitawali kila dakika ya mchezo. Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba Milan wanaingia katika mchezo huu chini ya kocha Ruben Amorim, ambaye anaanza kujenga utambulisho mpya wa timu.

Kwahiyo yoyote ambaye atakuwa amejiandaa vyema anaweza akaondoka na ushindi kule Meridianbet ambapo pia kuna machaguo zaidi ya 1000 yakiwa yanakungoja siku ya leo. Jisajili hapa.

Tengeneza pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kule Hispania LALIGA pia itaendelea ambapo Valencia watawaleta kwao Barcelona ambao ni mabingwa watetezi wa ligi na wanahitaji kupata ushindi kuendelea kujikita kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Valencia wapo katika hali ngumu zaidi baada ya kukusanya pointi moja pekee katika mechi tatu, hivyo mechi hii wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki zao wanahitaji kuthibitisha kuwa wanaweza kupambana na timu kubwa.

Barcelona wameonyesha ubora mkubwa katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi tatu za mwanzo wamefunga mabao 12, huku wakiruhusu mawili pekee. Ushindi wa 5-2 dhidi ya Rayo Vallecano ulikuwa uthibitisho mwingine wa uwezo wao wa kutengeneza nafasi na kumaliza mashambulizi, huku Raphinha na Lamine Yamal wakifunga mabao mawili kila mmoja. Meridianbet wanakwambia beti mechi hii sasa.

Kule Uingereza EPL itakuwa ya moto haswa kwani Dunia nzima itakuwa ikisubiri mechi ya London Derby kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya kuvutia haswa kwani zinakutana timu mbili ambazo zote zinahitaji ushindi kwenye mechi hii ya leo.

Arsenal chini ya Arteta ndio mabingwa watetezi wa ligi, lakini pia wamenza vyema kabisa ligi kwa kushinda mechi zake mbili bila kuruhusu bao lolote kwani wamekuwa na ukuta bora kwenye ligi nzima baada ya kuruhusu magoli machache msimu uliopita.

Huku kwa upande wa Chelsea wao msimu uliopita ulikuwa wa kusua sua kwao wakishindwa kujipatia mpaka nafasi za kushiriki michuano mikubwa ya Ulaya kama vile Uefa, Europa na hata Conference na kufanya maamuzi ya kuachana na aliyekuwa kocha wao na kuajiri kocha mpya. Jisajili hapa.

The Blues wamefanya usajili msimu huu kwaajili ya kuimarisha kikosi ikiwemo kusajili golikipa Emiliano kutokana na makosa ambaypo Sanchez alikuwa nayo, hivyo mechi hii inaenda kuwa ya ushindani mkubwa wakiwa na kocha mpya Alonso.

Arsenal wameendelea kuwa wababe mbele ya vijana hao wa Darajani kwani mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa ni msimu wa 2021, hivyo ni muda mrefu sana hawajapata ushindi?. Je nani kuondoka na ushindi?. Beti hapa.

Tanzania Yaanza Kwa Kishindo CAF, Simba na Singida Zang’ara Ugenini

Global Publishers
September 6, 2026
36 views
0 Comments

Timu za Tanzania zimeanza kwa matokeo mazuri katika mashindano ya klabu Afrika, huku Simba SC na Singida Black Stars zikirejea nyumbani na ushindi katika mechi zao za kwanza za raundi ya kwanza ya kufuzu.

Simba leo Septemba 6, 2026 imeanza kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) 2026/27 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Bingu National Stadium nchini Malawi.

Bao pekee la Simba lilifungwa dakika ya 65 na Oura, huku kipa Djibril Kassim akihusishwa na assist ya bao hilo.

Kwa upande mwingine, Singida Black Stars imeichakaza Al-Ghazala SC Wau ya Sudan Kusini kwa mabao 7-1 ugenini katika raundi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).

Tegisi alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufunga hat-trick ndani ya kipindi cha kwanza, akifunga dakika za 20, 23 na 32.

Sheikhan aliongeza bao la nne dakika ya 41, kabla ya Sowah kufunga dakika ya 63. Henry alifunga bao la sita dakika ya 86, huku Sowah akifunga tena dakika ya 90 kukamilisha ushindi mkubwa wa Singida.

Matokeo hayo yamewapa Simba na Singida mwanzo mzuri katika safari zao za kuwania nafasi ya kufuzu hatua za juu za mashindano ya klabu Afrika.

DKT. MWIGULU ATOA WITO WA MAANDALIZI YA MAPEMA KUKABILI ATHARI ZA EL NIÑO

*_▪︎ Atoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya mafuriko_*

*_▪︎ Aagiza ndani ya Septemba kutangazwa zabuni ya ujenzi wa barabara km 11 za Igauri–Ilongero_*

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania na viongozi katika ngazi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño.

Dkt. Mwigulu ametoa rai hiyo leo, Jumapili, Septemba 06, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ilongero, Wilaya ya Singida, mkoani Singida, katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema maeneo yenye historia ya mafuriko yanapaswa kutambuliwa mapema na hatua za tahadhari kuchukuliwa, huku akiwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuzingatia taarifa na maelekezo ya mamlaka husika.

“Maeneo ambayo mnaona ni ya hatari sana Watanzania tunayajua. Tunayajua maeneo yenye historia ya mafuriko. Ni vyema tukaanza kuchukua tahadhari kwa sababu hicho ndicho tunachoweza kukifanya,” alisema.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuimarisha uwezo wa kukabiliana na athari za mvua, ikiwemo kuwa na magari ya kuchimba mabwawa katika kila ukanda, huku akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuepuka kujenga au kuishi katika maeneo yanayofahamika kuwa hatarishi kwa mafuriko.

Kuhusu barabara ya Igauri–Ilongero, Dkt. Mwigulu ametoa agizo la kuhakikisha ndani ya mwezi huu mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa kilomita 11 za awali unakamilika.

“Ndani ya mwezi huu huu, muwe mmeshatangaza kupata mkandarasi wa kuanza kujenga hizi kilomita 11 za awali ambazo zitaziba hili pengo kuanzia hapa mpaka kwenye lami na kupita kidogo mji wa Ilongero,” alisema.

Alisema fedha kwa ajili ya mradi huo zipo na kinachosubiriwa ni kumpata mkandarasi, akisisitiza kuwa ujenzi huo unapaswa kuanza haraka.

Dkt. Mwigulu pia amesisitiza umuhimu wa Serikali kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha zinazookolewa kwenye maeneo yenye kipaumbele, hususan elimu, afya, maji na miundombinu.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2028, hivyo Serikali inapaswa kuanza mapema maandalizi ya madarasa, maabara, maktaba na mahitaji mengine ya elimu.

“Ni fedha ya Serikali, ni fedha ya walipa kodi wa Tanzania, ni fedha ambayo inaweza kwenda kutatua hizi changamoto watoto wasikae chini,” alisema.

Kuhusu afya, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ambulensi zinapaswa kuwa tayari muda wote na kuwa na mafuta ili wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura na rufaa wasicheleweshwe.

“Ambulensi zetu ziwe standby. Tulishanunua magari, yawe na mafuta. Kila wakati yawe na mafuta. Tusichangishe wagonjwa kuweka mafuta kwenye gari ya Serikali kubeba mgonjwa ambaye yuko mautini,” alisema.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote, akisema mfumo huo ni suluhisho la kudumu la kupunguza utegemezi wa michango ya dharura wakati wananchi wanapokabiliwa na gharama za matibabu.

“Watanzania wote tuingie kwenye bima ya afya. Tutaepukana na matatizo mengi sana ambayo tumeyatafutia majawabu ya dharura, lakini yanahitaji yapate majawabu ya kudumu,” alisema.

Kuhusu maji, Dkt. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji na umwagiliaji kwa ushirikiano wa wizara zinazohusika, ili miradi hiyo iweze kunufaisha wananchi, mifugo na shughuli za uzalishaji.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia matumizi yenye tija ya rasilimali za umma na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha, ufanisi na mahitaji halisi ya wananchi.