Makamu wa Rais Ndejembi Awasili Arusha, Kufungua C-CEOs Forum

Global Publishers
September 28, 2026
0 views
0 Comments

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amewasili mkoani Arusha leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, kwa ajili ya kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum).

Makamu wa Rais amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Baada ya kuwasili Arusha, Ndejembi anatarajiwa kuelekea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo atafungua rasmi kikao hicho kinachowakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma.

C-CEOs Forum inalenga kuwa jukwaa la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji, utendaji na mchango wa Taasisi na Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa.

Sayari Ya Bahati Ya Planet Power Slots Yawasili Meridianbet

Global Publishers
September 28, 2026
0 views
0 Comments

Kuna wakati bahati haiji yenyewe mlangoni, bali inahitaji uamue kuifuata. Sasa safari hiyo inaweza kuanza kupitia Planet Power Slots, mchezo mpya unaopatikana Meridianbet kasino na kukusafirisha moja kwa moja kwenye anga za mbali. Ukiwa tayari kwa burudani yenye msisimko na raundi zinazoweza kubadilisha hali ya mchezo wakati wowote, Planet Power Slots inakupa mazingira ya kipekee ya kujaribu bahati yako huku ukifurahia mandhari ya kuvutia.

Kutoka Expanse Studios, mchezo huu umejengwa kwa picha zenye kuvutia ambazo zinakufanya uhisi kama umeingia kwenye misheni ya siri katikati ya sayari. Taa zinazong’aa, sayari zinazozunguka na mwonekano wa anga la mbali vinaunda mazingira yanayovutia macho kila sekunde. Kila raundi inakuwa kama hatua nyingine ya safari, huku matarajio yakibaki juu ya kile kinachoweza kujitokeza baada ya hapo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Msisimko unaongezeka zaidi pale vizidishi vinapoanza kuonekana, huku mchezo ukiwa na uwezo wa kufikisha kizidishi hadi x1000. Hapo ndipo raundi ya kawaida inaweza kugeuka kuwa tukio la kusisimua zaidi, kulingana na matokeo yatakayopatikana. Kwa kila mzunguko, macho yanabaki kwenye skrini huku ukisubiri kuona kama kizidishi kikubwa kitajitokeza na kuongeza thamani ya ushindi.

Planet Power Slots pia haijaja na raundi za kawaida pekee. Kuna bonasi zinazoweza kufungua fursa nyingine za kucheza na kushinda bila kuhitaji kuongeza dau jipya katika kila hatua. Hii huongeza ladha ya mchezo, kwa sababu kila bonasi inaweza kuleta sura tofauti ya safari yako. Kadri raundi zinavyosonga, ndivyo matarajio yanavyoongezeka.

Kisha inatokea sayari ya njano, na hapo ndipo mchezo unaweza kubadilika. Muonekano wake unaashiria kufunguka kwa bonasi huku jackpot ikianza kusogea karibu. Ukiwa tayari kwa safari yenye mandhari ya anga, vizidishi na bonasi, Planet Power Slots inakusubiri Meridianbet.

Ubelgiji, Ufaransa Kukipiga Kipute Kikali Nations League

Timu ya Taifa ya Ubelgiji itakuwa mwenyeji wa Ufaransa katika mchezo wa UEFA Nations League 2026/27 utakaochezwa Jumatatu, Septemba 28, katika Uwanja wa King Baudouin jijini Brussels. Mchezo huo wa Kundi A1 utaanza saa 21:45 usiku.

Mchezo huo unakuja katika siku ya pili ya hatua ya ligi, huku Ubelgiji na Ufaransa zikiwa katika Kundi A1 pamoja na Italia na Türkiye. Ubelgiji inaanza kampeni yake kwa kukutana na Italia Septemba 25, wakati Ufaransa itaanza dhidi ya Uturuki kabla ya kuelekea Brussels kukutana na Ubelgiji.

Kwa upande wa Ubelgiji, mchezo huo utakuwa pia mwanzo wa safari mpya chini ya kocha Mark van Bommel. Kocha huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi amechukua jukumu la kuiongoza Ubelgiji, huku akiwa na jukumu la kujenga kikosi kitakachokuwa na ushindani katika kundi lenye timu kubwa za Ulaya.

Ufaransa nayo inaingia katika mchezo huo ikiwa chini ya kocha mpya Zinedine Zidane, ambaye amerejea kwenye ukocha baada ya kuondoka Real Madrid zaidi ya miaka mitano iliyopita. Zidane amemteua Kylian Mbappé kuendelea kuwa nahodha wa Les Bleus, hivyo mchezo dhidi ya Ubelgiji utakuwa sehemu muhimu ya mwanzo wa kipindi chake kipya kwenye timu hiyo.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Historia ya hivi karibuni inaifanya mechi hii kuwa ya kuvutia zaidi, kwani Ufaransa imeshinda michezo mitano ya mwisho dhidi ya Ubelgiji. Pia, katika toleo lililopita la Nations League, Ufaransa ilishinda dhidi ya Ubelgiji kwa mabao 2-0 na 2-1. Hata hivyo, Ubelgiji itakuwa na nafasi ya kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kuvunja rekodi hiyo.

Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa miongoni mwa mikutano mikubwa ya siku hiyo katika Nations League, hasa kwa sababu timu zote mbili zinaingia katika mashindano hayo chini ya makocha wapya. Mashabiki watakuwa wakifuatilia pia namna Zidane na van Bommel watakavyopanga vikosi vyao katika mchezo huo wenye historia na ushindani mkubwa.

Lissu Aitaka Mahakama Kupuuza Ushahidi wa Mashahidi wa Kificho

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiomba Mahakama kutotegemea ushahidi uliotolewa na mashahidi wa kificho katika kesi inayomkabili, akidai kuwa baadhi ya ushahidi wao ulikuwa na uongo, mkanganyiko na maslahi.

Lissu ametoa ombi hilo leo, Jumatatu, Septemba 28, 2026, wakati akiendelea kuwasilisha hoja zake za mwisho mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.

Katika hoja zake, Lissu amewataja mashahidi hao kuwa ni PW5, PW7, PW8, PW10, PW11, PW13 na PW14, akidai kuwa ushahidi walioutoa mahakamani una mapungufu mbalimbali.

Lissu amesema ushahidi wa mashahidi hao haupaswi kupewa uzito kutokana na kile alichodai kuwa ni taarifa zisizo za kweli na zenye maslahi.

Kwa upande wa PW5, Lissu amedai kuwa shahidi huyo alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu dini yake, akieleza kuwa mahakamani alikula kiapo kama Mkristo, wakati katika maelezo yake yaliyowasilishwa kama kielelezo D4 alijieleza kuwa ni Muislamu.

Pia amedai kuwa PW5 alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu uanachama wake wa CHADEMA.

Akizungumzia PW7, Lissu amedai kuwa shahidi huyo alitoa taarifa za uongo kuhusu kupelekwa katika Kituo cha Polisi Songea pamoja na suala la uanachama wake wa CHADEMA.

Kuhusu PW8, Lissu amesema ushahidi wake ulikuwa na mikanganyiko na taarifa ambazo, kwa mtazamo wake, hazikuwa za kweli.

Aidha, akielezea ushahidi wa PW10, Lissu amedai shahidi huyo alitoa maelezo kwa polisi kwamba mshtakiwa alisema walikuwa wamejipanga kufanya fujo ili kuzuia uchaguzi. Lissu amekanusha kauli hiyo, akisema hakuwahi kutoa kauli kama hiyo.

Kwa upande wa PW11, Lissu amesema ushahidi wake pia ulikuwa na mikanganyiko na kwamba haukuwa wa kweli.

Kuhusu PW13, Lissu amedai shahidi huyo alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu uanachama wake wa CHADEMA, akisema katika maelezo yake alijitambulisha kama mwanachama wa chama hicho, jambo ambalo Lissu amepinga.

Lissu pia amepinga ushahidi wa PW14, akidai shahidi huyo alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu kazi yake. Kwa mujibu wa Lissu, katika maelezo ya polisi shahidi huyo alijitambulisha kama mkulima wa Kata ya Mwakibete, huku mahakamani akisema yeye ni fundi umeme wa Jiji la Mbeya.

Lissu pia amekanusha madai kwamba PW14 alimsikia akisema “lazima tukichafue,” akisema hakuwahi kutoa kauli hiyo.

Hoja hizo zimewasilishwa na Lissu katika hatua ya hoja za mwisho, huku Mahakama ikiendelea kusikiliza pande zinazohusika kabla ya hatua inayofuata ya kesi.

TFF Yafanya Mabadiliko Makubwa, Evans Mgeusa Ateuliwa Katibu Mkuu Mpya wa TFF

Global Publishers
September 28, 2026
60 views
0 Comments

Evans Mgeusa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa TFF.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya pamoja na kufanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi za Kurugenzi zake.

Mabadiliko hayo yametangazwa leo, Septemba 28, 2026, kupitia kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam chini ya Rais wa TFF, Wallace Karia.

Katika uteuzi huo, Evans Mgeusa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa TFF, akichukua nafasi ya Oscar Mirambo, ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Mgeusa alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NIOREFA).

Kwa upande wake, Oscar Mirambo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, huku Mustapha Yusuph akiteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha.

Aidha, TFF imefanya mabadiliko katika Kurugenzi ya Sheria, Habari na Masoko, pamoja na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano.

Waliopewa majukumu ya kuongoza Kurugenzi hizo ni:

  • Hassan Njama – Mkurugenzi wa Biashara na Masoko
  • Boniface Wambura – Mkurugenzi wa Sheria
  • Cliford Ndimbo – Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano

TFF imesema mabadiliko hayo yamefanyika kupitia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

TFF Yafanya Mabadiliko Makubwa, Evans Mgeusa Aingia Uenyekiti

Global Publishers
September 28, 2026
0 views
0 Comments

Evans Mgeusa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa TFF.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya pamoja na kufanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi za Kurugenzi zake.

Mabadiliko hayo yametangazwa leo, Septemba 28, 2026, kupitia kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam chini ya Rais wa TFF, Wallace Karia.

Katika uteuzi huo, Evans Mgeusa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa TFF, akichukua nafasi ya Oscar Mirambo, ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Mgeusa alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NIOREFA).

Kwa upande wake, Oscar Mirambo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, huku Mustapha Yusuph akiteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha.

Aidha, TFF imefanya mabadiliko katika Kurugenzi ya Sheria, Habari na Masoko, pamoja na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano.

Waliopewa majukumu ya kuongoza Kurugenzi hizo ni:

  • Hassan Njama – Mkurugenzi wa Biashara na Masoko
  • Boniface Wambura – Mkurugenzi wa Sheria
  • Cliford Ndimbo – Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano

TFF imesema mabadiliko hayo yamefanyika kupitia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Serikali yasisitiza tahadhari migodini kukabili El Nino – HabariLeo

KAHAMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametoa maagizo kwa wamiliki na mameneja wa migodi nchini kuhakikisha wanaboresha maeneo ya uchimbaji wa madini, hususan upande wa maduara, uwekaji wa mtingi na vyoo, ili kuhakikisha usalama kabla ya mvua za El Nino zinazotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuanza kunyesha.

Mhandisi Samamba ametoa maagizo hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya wachimbaji wadogo iliyolenga maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za El Nino katika maeneo ya uchimbaji wa madini.

Amesema maagizo hayo yanaendana na msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wa kuchukua tahadhari mapema na kuhakikisha miundombinu katika maeneo ya uchimbaji inakuwa salama.

Mhandisi Samamba amesema asilimia 70 ya ajali zote migodini zinatokana na udongo kulowana na kuwa mzito, huku mtingi ukiwa wa muda mrefu na wakati mwingine kuoza, hivyo jitihada za kuboresha miundombinu zinapaswa kuanza mapema ili kuepusha vifo na madhara kwa wachimbaji.

“Mojawapo ya majanga yanayosababisha vifo vya watu wengi ni ajali za migodini, lakini tukijitahidi kutengeneza miundombinu mizuri, mfano kuweka mifereji itakayosaidia kutiririsha maji, kubadilisha mtingi na kuweka wenye ubora pamoja na kujenga vyoo vizuri ili kuepuka magonjwa kama kipindupindu, tutapunguza madhara,” amesema Mhandisi Samamba.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Tanzania (FEMATA), ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kagusi, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wachimbaji kwa kuwa yanawawezesha kuelewa athari zinazoweza kusababishwa na mvua zinazotarajiwa.

Amesema wachimbaji watahakikisha wanazingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali ili kujilinda na madhara yanayoweza kutokea wakati wa mvua hizo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wakaguzi wa Migodi Tanzania (CHAWUMITA), Shija Musa, amesema wameanza kuchukua hatua za tahadhari kwa kufunga mtingi na kufukia mashimo ambayo hayatumiki.

Amesema chama hicho kitaendelea kuhakikisha maelekezo yote yanayotolewa na Serikali kuhusu usalama wa wachimbaji yanatekelezwa.

Netanyahu Atembelea Abu Dhabi, Akutana na Rais wa UAE

ABU DHABI – Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ametembelea Abu Dhabi na kukutana na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, siku ya Jumapili, Septemba 27, 2026, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Israel aliyezungumza na Reuters.

Taarifa kuhusu ziara hiyo haijaeleza kwa kina ajenda ya mazungumzo yao, huku ofisi ya Netanyahu na Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE zikiwa hazijatoa kauli ya haraka kuhusu mkutano huo.

Ziara hiyo inafanyika wakati ambapo uhusiano wa Israel na UAE unaendelea kuwa sehemu muhimu ya diplomasia ya Mashariki ya Kati, baada ya nchi hizo kuanzisha rasmi uhusiano wa kidiplomasia mwaka 2020 kupitia Abraham Accords.

Mkutano huo pia unakuja wakati Netanyahu akikabiliwa na mjadala mkali wa kisiasa nchini Israel kuhusu changamoto za kiusalama zilizotangulia shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023.

Mapema mwezi huu, gazeti la Haaretz liliripoti kuwa Sheikh Mohammed alikuwa amemwonya Netanyahu kabla ya shambulio hilo kwamba Hamas ilikuwa ikipanga operesheni kubwa dhidi ya Israel. Gazeti hilo lilidai kuwa taarifa hiyo haikufikishwa kwa vyombo vya ujasusi au jeshi la Israel.

Netanyahu amekanusha taarifa hiyo na ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Haaretz. UAE nayo haijatoa maoni kuhusu ripoti hiyo, ingawa imeeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na Israel, nchi hizo zimekuwa na njia za mawasiliano ya moja kwa moja na wazi.

Ziara ya Netanyahu pia inafuatia taarifa zilizowahi kutolewa kuhusu mikutano yake ya siri na viongozi wa UAE. Mapema mwaka huu, UAE ilikanusha kuwa Sheikh Mohammed alikutana na Netanyahu baada ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel kudai kuwa Netanyahu alikuwa ametembelea nchi hiyo kwa siri.

Kwa mujibu wa chanzo kilichofahamu kuhusu mkutano huo, Netanyahu na Sheikh Mohammed waliwahi kukutana Al Ain, mji wa oasis uliopo katika eneo la Abu Dhabi karibu na mpaka wa UAE na Oman, Machi 26.

UAE na Israel zimeendelea kudumisha uhusiano wao tangu Abraham Accords ya mwaka 2020, huku uhusiano huo ukiipa UAE njia ya kushirikiana na Israel pamoja na kuwa na mawasiliano muhimu na Marekani katika masuala ya kikanda.

MTV VMAs 2026: Taylor Swift, Madonna na BTS Waandika Historia

Global Publishers
September 28, 2026
12 views
0 Comments

Sherehe za MTV Video Music Awards (VMAs) 2026 zimefanyika Jumapili, Septemba 27, katika ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles, Marekani, huku Snoop Dogg akiwa mwenyeji wa hafla hiyo.

Katika tuzo hizo, Madonna aliongoza kwa kupata tuzo kadhaa, huku BTS, Taylor Swift, Ariana Grande, Bruno Mars, LISA na wasanii wengine wakitajwa miongoni mwa washindi.

Hii hapa ni orodha ya washindi kwa baadhi ya vipengele vikuu:

  • Best Group: BTS

  • Best Long Form Video: Madonna – Confessions II – The Film

  • Best Album: Madonna –Confessions II

  • Song of Summer: Ariana Grande – hate that i made you love me

  • Video of the Year: Taylor Swift –The Fate of Ophelia

  • Artist of the Year: Madonna

  • Song of the Year: BTS – Swim

  • Best New Artist: Sienna Spiro

  • Best Collaboration: Madonna & Sabrina Carpenter – Bring Your Love

  • Best Pop: LISA –Dream feat. Kentaro Sakaguchi

  • Best Hip-Hop: Cardi B ft. Kehlani – Safe

  • Best R&B: Bruno Mars –I Just Might

  • Best Alternative: Olivia Rodrigo – the cure

  • Best Dance: Madonna – Confessions II – The Film

  • Best Latin: Bad Bunny – NUEVAYoL

  • Best K-Pop: BTS –SWIM

  • Best Country: Ella Langley – Choosin’ Texas

  • Best Direction: Taylor Swift – Opalite

  • Best Art Direction: PinkPantheress –Stateside + Zara Larsson

  • Best Cinematography: Madonna – Confessions II – The Film

  • Best Editing: Sabrina Carpenter –House Tour

  • Best Choreography: Madonna –Confessions II – The Film

  • Best Visual Effects: Ariana Grande –hate that i made you love me

Mbali na tuzo hizo, Taylor Swift alitunukiwa tuzo mpya ya Artist Director Honors, huku kundi la Nirvana likipewa Video Vanguard Award.

Hafla hiyo pia ilihusisha maonyesho ya wasanii mbalimbali, wakiwemo Madonna, LISA, RAYE, Shaboozey, Gunna, Sienna Spiro, Gener8ion na Yung Lean. RAYE, Sombr na Teddy Swims walishiriki katika heshima maalum kwa George Michael, huku Kacey Musgraves akiongoza heshima kwa Dolly Parton.

Uchomaji moto misitu watia hofu wawekezaji Missenyi – HabariLeo

MISSENYI: Vitendo vya uchomaji moto misitu, mashamba na maeneo ya malisho vimeendelea kuleta hofu na simanzi kwa wawekezaji na wananchi katika Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera, huku wadau wakihimiza kuongezwa kwa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya uchomaji moto.

Mwekezaji wa shamba la kilimo cha kahawa na migomba la Bwikaranyange Investment Ltd, lililopo Kata ya Bugandika wilayani Missenyi, ameiomba Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Kitengo cha Majanga kuongeza kasi ya utoaji elimu kuhusu madhara ya uchomaji moto misitu na maeneo mengine.

Mwekezaji huyo, Justine Lambart, kupitia Meneja wa shamba hilo, Optat Rwebugisa, amesema uwekezaji huo una thamani ya Sh milioni 600, ambapo tayari uwekezaji umefanyika katika eneo lenye ukubwa wa ekari 374 kati ya ekari 570.

Amesema changamoto ya uchomaji moto imekuwa kikwazo kikubwa kinachozua taharuki katika maandalizi ya uwekezaji na mipango ya baadaye ya kujenga kiwanda katika eneo hilo.

Rwebugisa amesema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Kitengo cha Majanga inapaswa kubadili mbinu na mipango ya utoaji elimu kuhusu madhara ya kuchoma nyika, mashamba na maeneo ya malisho ya mifugo, akieleza kuwa katika msimu wa kiangazi maeneo makubwa yanayochomwa moto yanaweza kugeuka kuwa majanga makubwa.

Amesema hali hiyo pia inaweza kukatisha tamaa wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika Wilaya ya Missenyi.

“Tangu nimeanza kufanya uwekezaji, tishio la moto katika eneo letu limekuwa endelevu. Mara nyingi shughuli za uwekezaji zinasitishwa kwa ajili ya kuhangaika kuzima moto katika eneo letu na maeneo ya jirani, huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani,” amesema.

Amesema hivi karibuni moto ulichoma mashamba ya jirani na kuhatarisha nyumba pamoja na Shule ya Sekondari Bwabuki, huku shule hiyo ikinusurika.

Ameongeza kuwa kuna wakati moto ulichoma shamba la miti katika eneo lao, huku siku nyingine wafanyakazi na vibarua wakilazimika kusitisha shughuli zao kwa takribani saa tano ili kwenda kuzima moto katika mashamba ya jirani.

“Kama mnavyoona, shamba hili limetandazwa mabomba kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Kama moto utaunguza shamba, hasara inaweza kuwa kubwa. Mara nyingi wanasema wanaochoma mashamba ni wafugaji, lakini je, kweli elimu kuhusu kuchoma misitu au maeneo ya kufugia imetolewa?” amehoji Rwebugisa.

Amesema hali hiyo imeifanya tishio la moto kuwa jambo linalowafanya wawekezaji kuwa na hofu kuhusu usalama wa mali na uwekezaji wao.

Madai hayo yameibuka siku chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa kwamba vijana wa shamba la mwekezaji waliokuwa wakisafisha eneo kwa ajili ya kupanda migomba na mibuni walidaiwa kusahau kuzima moto na kusababisha mashamba ya majirani kuungua.

Hata hivyo, baada ya vyombo vya habari kufika katika shamba hilo, uongozi wa shamba ulisema mashamba ya miti yaliyoungua yalikuwa mbali na eneo la uwekezaji, yakiwa katika kata jirani, na kwamba Jumapili si siku ya kusafisha shamba bali ni siku ya shughuli za umwagiliaji.

Msimamizi wa Umwagiliaji katika shamba hilo, Majaliwa Patrick, amesema waliona moto ukiwaka katika mashamba ya Kata ya Kitobo, kata jirani, hivyo wafanyakazi na vibarua walitoa nguvu zao kwenda kuzima moto huo.

Amesema hakuna kipande cha shamba la Bwikaranyange Investment kilichoungua siku hiyo, huku akieleza kuwa Jumapili ambayo Jeshi la Polisi lilisema moto ulitokea, ilikuwa siku ya mapumziko katika eneo hilo la uwekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, mashamba 39 ya watu watano yenye thamani ya Sh milioni 36.9 katika Kijiji cha Kijunja, Kata ya Kitobo wilayani Missenyi, yaliungua baada ya vijana wanne kuwasha moto kwa ajili ya kusafisha shamba katika eneo la mwekezaji lililopo Kata ya Bugandika na kusahau kuuzima.

Hata hivyo, Chatanda alisema vijana hao hawakuwa wamefahamika majina hadi wakati huo, huku akiwataka wananchi kuacha vitendo vya kuchoma moto misitu na mashamba.

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Mstaafu Hamis Mahiga, amesema moto kwa wawekezaji katika wilaya hiyo ni tishio kubwa linaloendelea kuleta maumivu kwa wawekezaji na wananchi wa kawaida.

Amesema katika msimu wa kiangazi kila mwaka, maeneo ya nyika na misitu katika wilaya hiyo huchomwa kwa kiwango kikubwa, akieleza kuwa mwaka huu hata mashamba makubwa ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) yameungua.

Ameongeza kuwa mashamba ya wananchi, wawekezaji wa kilimo cha miwa, miundombinu na baadhi ya nyumba pia viliungua na kusababisha simanzi kwa wananchi.

Mahiga amesema uongozi unaendelea kuchunguza chanzo cha uchomaji moto huo, huku akieleza kuwa hata wafugaji wanaodaiwa kuchoma moto mara nyingi hawasikiki wakiacha ushahidi unaoweza kusaidia kuwabaini na kuwachukulia hatua.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kukabiliana na majanga ya moto, akisema uchomaji moto una madhara mbalimbali, ikiwemo kuharibu miundombinu ya umeme, shule na misitu, pamoja na kuchangia athari za mabadiliko ya tabianchi.