Makamu wa Rais Atembelea Hospitali ya Mount Meru, Arusha

Global Publishers
September 29, 2026
0 views
0 Comments

ARUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wagonjwa na watumishi.

Baada ya kuwasili hospitalini hapo, Makamu wa Rais alipokelewa na viongozi na watumishi wa hospitali hiyo, ambapo alipatiwa taarifa kuhusu maendeleo, utendaji na huduma zinazotolewa.

Baadaye alitembelea wodi mbalimbali na kuzungumza na wananchi wanaopata matibabu katika hospitali hiyo.

Akiwa hospitalini hapo, Ndejembi aliwapa pole wagonjwa kutokana na changamoto za kiafya zinazowakabili na kuwafikishia salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kuipa sekta ya afya kipaumbele kwa lengo la kuboresha huduma na kuhakikisha wananchi wanapata matibabu yenye ubora katika vituo vya afya nchini.

Katika Wodi ya Wazazi, Ndejembi alieleza kufurahishwa kuwaona akina mama waliojifungua salama pamoja na watoto wao wakiwa katika hali nzuri kiafya.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wanawake na watoto katika maeneo mbalimbali nchini.

Ziara hiyo pia ilimpa Makamu wa Rais fursa ya kuzungumza ana kwa ana na baadhi ya wagonjwa kuhusu huduma wanazopata na changamoto wanazokutana nazo.

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma za afya nchini.

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wagonjwa na watumishi wa hospitali hiyo.

 

Mara baada ya kuwasili hospitalini hapo, Makamu wa Rais amepokelewa na viongozi pamoja na watumishi wa hospitali, ambapo taarifa fupi ilitolewa kuhusu maendeleo, utendaji na huduma zinazotolewa, kabla ya kutembelea wodi mbalimbali na kuzungumza na wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo.

 

Akizungumza na wananchi waliolazwa hospitalini hapo, Mhe. Ndejembi aliwapa pole kutokana na maradhi yanayowakabili na kuwafikishia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuipa sekta ya afya kipaumbele na kuboresha huduma zinazotolewa katika vituo vya afya nchini.

 

Akiwa katika Wodi ya wazazi, Makamu wa Rais alieleza kufurahishwa kuwaona akina mama waliojifungua salama pamoja na watoto wao wakiwa na afya nzuri, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo vya watoto.

 

Alisema jitihada hizo zinaendana na dhamira ya Rais Samia ya kuhakikisha huduma bora na salama za afya ya uzazi zinawafikia wanawake na watoto katika maeneo mbalimbali nchini, sambamba na nafasi yake katika kusukuma mbele ajenda ya kupunguza vifo vya mama na mtoto barani Afrika.

 

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kuzungumza ana kwa ana na baadhi ya wagonjwa kuhusu huduma zinazotolewa hospitalini hapo.

 

Wagonjwa hao walieleza kuridhishwa na huduma wanazopatiwa, huku baadhi yao wakitaja kushindwa kulipa gharama za matibabu. Kufuatia changamoto hiyo, Makamu wa Rais aliwezesha kulipwa kwa gharama za matibabu za baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamekwama kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulipa, hatua iliyowapa unafuu wagonjwa hao pamoja na familia zao.

 

Ziara hiyo imempa Makamu wa Rais nafasi ya kujionea moja kwa moja huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Mount Meru, kusikiliza wananchi wanaozitumia na kufahamu changamoto zinazowakabili, huku akisisitiza kuendelea na hatua za kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma za afya nchini.

 

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais alitembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, kuwasalimu wananchi na kujionea hali ya mazingira mkoani humo.

 

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

29 Septemba 2026

Arusha

BREAKINGNEWS, AJALI YA FUSO YAUA WATANO KILOLO IRINGA

Wananchi  wakishuhudia  ajali ya  gari aina ya  fuso picha  hii ya Maktaba haihusiana na ajali ya  Kilolo

 NA  MATUKIO  DAIMA  MEDIA  KILOLO 

WATU  watano  wamefariki  dunia  papo hapo na  wawili  kujeruhiwa baada ya   gari aina ya  fuso  lililokuwa  limebeba  mbao  kufeli  Breck na  kuparamia  kibanda   cha  kutolea  huduma  za  Kifedha  katika kijiji  cha  Kidabaga  wilayani Kilolo mkoa wa Iringa .

Kwa  mujibu  wa mashuhuda  waliozungumza na Matukio  Daima  Media  kwa  njia ya  simu  walisema  kuwa fuso hiyo  ilifeli Breck na kuwagonga  wananchi hao  waliokuwa   nje ya kibanda hicho na  huduma ya  Kifedha  wakisubiri  usafiri .

Hata  hivyo  shuhuda  huyo  alisema  kabla ya  kugongwa na fuso hiyo  watu hao  walijaribu  kujiokoa kwa  kutaka  kukimbia  ila  hawakufanikiwa  kufika  mbali .

Matukio  Daima  tumemtafuta  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo ambae  pia  ni mwenyekiti wa kamati ya  ulinzi na usalama  wilaya hiyo  Stomen Kyando  ambae  amethibitisha  kutokea kwa  ajili  hiyo  na kuwa  ajali  hiyo  ilitokea majira ya  saa 9 Alasiri Septemba 29 mwaka  huu.

Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  jumla ya watu watano  ndio  waliofariki katika  ajali  hiyo  wakiwemo  wanawake  wanne wakiwemo  watu  wazima  watatu na mtoto  mmoja  mchanga wa  kike  aliyekuwa na mama yake  pamoja na  mwanaume  mmoja .

Alisema katika  ajali  hiyo majeruhi  mmoja amekimbizwa  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa  Iringa kwa matibabu  zaidi  huku  mhudumu wa  kibanda  cha  huduma  za  Kifedha akipata  majeraha  kiasi na  kuwa jitihada  za  kumtafuta  dereva  zinaendelea.

Hata  hivyo  mkuu  huyo wa wilaya  ametoa pole  nyingi kwa  familia  za  watu  waliopoteza maisha  katika  tukio  hilo na kuwa  serikali ya wilaya  itakuwa pamoja  nao wakati  wote  wa maombolezo.

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA
 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

POLISI WADAIWA KUMUUA KWA RISASI MTUHUMIWA WA UHALIFU ALIYEWATEKA MWANAMKE NA MTOTO WAKE

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo akikagua nyumba ambayo mtuhumiwa alijificha baada ya kuwaona polisi

Baba wa mtuhumiwa aliyeuawa

Na Matukio Daima Media, Kilosa

TUKIO la kutekwa kwa mwanamke na mtoto wake katika Kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro limeishia kwa kifo cha Kokan State (30), baada ya mwanaume huyo kudhibitiwa kwa risasi na polisi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, Kokan alikuwa akitafutwa kwa tuhuma zinazohusisha mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia silaha.

Kantimbo akasema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na  polisi kwa muda mrefu ambapo baada ya kubaini alipo na kumfuata, alimshika mwanamke aliyekuwa alimhudumia kinywaji pamoja na mtoto wake mdogo na kujifungia nao katika chumba, akiwatumia kama kinga dhidi ya polisi.

Alisema Kokan alitishia kuwaua Mama na mtoto huyo kwa sime iwapo polisi wangejaribu kumkamata, hali iliyosababisha askari kutumia silaha na kumuua baada ya jitihada zote za kutaka ajisalimishe kushindikana.

Mwanamke na mtoto waliotumiwa kama Kinga na mtuhumiwa wa uhalifu

Mwanamke huyo aliyetekwa, mkazi wa Kijiji cha Parakuyo, Rehema Masuke, amesema tukio hilo liliwapa hali ya hofu wakiamini huenda wangeuawa kwa sime aliyokuwa nayo kijana huyo.

Kwa upande wake Baba mzazi wa Kokan amesema kwa muda mrefu alikuwa akimkanya mwanawe kuacha kujihusisha na Matukio ya ki uhalifu, lakini licha ya ushauri huo, alihusishwa mara kadhaa na matukio hayo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Parakuyo, Emmanuel Kibasisi, amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama na kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na uhalifu.

Polisi mkoani Morogoro wameendelea kutoa wito kwa vijana kujiepusha na uhalifu na kutafuta kipato kupitia shughuli halali.

Mwisho

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

MOROGORO YAJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NINO

Na; Mwandishi Wetu – Morogoro.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu, Idara ya Usimamizi wa Maafa Dkt. Salim Manyata ametoa Salaam za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Kamati za Maafa za Mkoa wa Morogoro pamoja na Timu ya Mkoa ya Kukabiliana na Dharura wakati wa kikao kazi kitakachoambata na ziara ya kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa kwa Mikoa kuhusu kujiandaa na kukabiliana na athari za El Nino tarehe 28 Septemba 2026.

Mawasilisho mbalimbali yamewasilishwa katika kikao kazi hicho ikiwa ni pamoja na Taarifa ya Utayari kwa kila sekta na wadau ya kujiandaa na kukabiliana na athari za El Nino, ambapo sekta zilizohusika ni pamoja na TANROADS, TARURA, Sekta ya Afya,TANESCO, kilimo, Maji yaani maji safi na maji taka na Mamlaka zote za Bonde, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Shirika la Reli nchini (TRC), Maliasili, REDCROSS na SKAUTI.

Awali, akizungumza katika kikao hicho kilichohusisha pia kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa kabla ya kuanza Ziara Maalum Mkoani hapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Masauni (Mb), alisema ni muhimu kuchukua tahadhari na hatua mahsusi  kuhusiana na tishio la El Nino na kuweka nguvu zaidi katika kuzuia na kujiandaa  ili hata madhara yatakapotokea yasiwe makubwa zaidi. 

“Tutumie vizuri Rasilimali zilizopo ili kuweza kukabiliana na jambo hili, sambamba na kuzingatia suala zima la usafi wa mazingira katika maeneo yetu Alisisitiza Waziri Masauni.’

Imeelezwa kuwa Mkoa wa Morogoro ni Miongoni mwa Mikoa ambayo imekuwa akiathirika mara nyingi na mvua za misimu tofauti, hivyo ni vyema  kuangaliwa kwa namna ya kipekee hasa katika kipindi hiki cha Mvua za El Nino, zilizotabiriwa na Mamlaka ya hali ya hewa Nchini kunyesha mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2026

” Usimamizi wa Maafa ni jukumu la kila mtu, kila mmoja anatakiwa kushiriki sasa na kuchukua hatua katika eneo lake ili kuokoa  maisha, mali, miundombinu na mazingira.”

 

MSAMVU YASOTA, ABIRIA WASUBIRI HATMA YA SAFARI

 

Na Matukio Daima Media, Morogoro 

Hali ya usafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi Msamvu mkoani Morogoro leo ilikuwa tete, huku mabasi mengi yanayoanzia safari kituoni hapo yakishindwa kuanza safari na kusababisha abiria waliokuwa wakielekea mikoa mbalimbali nchini kusubiri kwa muda mrefu bila kujua hatma yao.

Baadhi ya abiria waliokuwa wamefika kituoni hapo tangu saa 12 kamili alfajiri waliendelea kusubiri, huku wengine wakilazimika kurejea nyumbani baada ya kukosa uhakika wa kuondoka. 

Miongoni mwa waliokumbwa na hali hiyo ni Harold Jackson, Anold Munuo na Hemedi Michael waliokuwa wakielekea Arusha na Moshi ambao walilalamikia muda walioupoteza kituoni hapo.

Mwenyekiti wa Wasafirishaji Kituo Kikuu cha Mabasi Msamvu, Aziz Kapilima, akaishauri Serikali kukutana na madereva na kusikiliza malalamiko yao ili kupata ufumbuzi wa haraka.

Kapilima  alisema kuendelea kwa mgomo huo kutaathiri abiria, wamiliki wa mabasi, madereva na Serikali kwa ujumla kiuchumi na kijamii.

Dereva mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema moja ya mambo yaliyowakwaza madereva ni kutoshirikishwa katika maamuzi yanayowahusu, huku akilalamikia faini, kufungiwa leseni na kupunguziwa pointi wanapokutwa na makosa barabarani.

 Alisema hali hiyo inaweza kuathiri ajira zao na maisha ya familia zinazowategemea hasa pale wanapokuwa hawana Leseni za kufanya kazi tofauti na madereva wa Serikali walioajiriwa ambao hata wakipata Ajali wakaumia na wasifanye kazi watalipwa.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, ametembelea maeneo mbalimbali ya usafirishaji, ikiwemo Mikumi na Kituo cha Mabasi Msamvu, na kutoa onyo kwa watu watakaowabughudhi madereva pamoja na vyombo vya usafiri vilivyoamua kuendelea kutoa huduma. 

Wakati huohuo, baadhi ya mabasi yalianza kutoa huduma  kwa uchache majira ya mchana tofauti na awali ambapo yale yaliyotokea safari za masafa marefu ndio  yaliyooendelea kupita kituoni hapo.

Mwisho

Waziri Katambi Awasili Stendi ya Mbezi Magufuli Kufuatia Mgomo wa Madereva – Live

Global Publishers
September 29, 2026
18 views
0 Comments


DAR ES SALAAM: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewasili katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mbezi Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia kusitishwa kwa safari za mabasi kunakodaiwa kusababishwa na mgomo wa madereva.

Katambi amefika stendi hiyo jioni hii kwa ajili ya kukutana na madereva pamoja na abiria waliokwama kutokana na kusitishwa kwa safari za mabasi.

Waziri huyo anatarajiwa kuzungumza na madereva na abiria mbele ya vyombo vya habari, huku akieleza hatua zitakazochukuliwa kuhusu hali hiyo.

Mgomo huo umeathiri huduma za usafiri katika baadhi ya vituo vya mabasi nchini, huku madereva wakieleza kuwa wanapinga masuala mbalimbali yanayohusiana na adhabu na faini za usalama barabarani.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya abiria kushindwa kuendelea na safari zao, huku mabasi yaliyokuwa yamepangwa kuondoka yakiwa hayajaanza safari.

Video: DCEA Yakamata Mirungi na Bangi Zikisafirishwa kwa Mabasi na Magari

Global Publishers
September 29, 2026
6 views
0 Comments

DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata watuhumiwa waliodaiwa kutumia vyombo vya usafiri kusafirisha dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa DCEA, watuhumiwa watatu walikamatwa wakisafirisha bunda 238 za mirungi zenye uzito wa kilogramu 125.33, kwa kutumia basi la kampuni ya RATCO lenye namba za usajili T 443 EMG, lililokuwa likifanya safari kati ya Tanga na Dar es Salaam.

Katika tukio jingine, DCEA imekamata kilogramu 21.95 za bangi katika Wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

Bangi hiyo ilidaiwa kuwa inasafirishwa kwa gari aina ya Tata lenye namba za usajili T 381 DW, lililokuwa likifanya safari kati ya Uyui mkoani Tabora na Kahama mkoani Shinyanga.

Katika tukio hilo, jumla ya watuhumiwa watano walikamatwa na wanatarajiwa kufikishwa katika hatua za kisheria kwa mujibu wa taratibu.

DCEA imeendelea kutoa tahadhari kuhusu matumizi ya vyombo vya usafiri katika kusafirisha dawa za kulevya, huku ikiimarisha operesheni za kudhibiti usafirishaji na biashara ya dawa hizo nchini.

Jamhuri Yafafanua Jinsi Kauli za Mshtakiwa Zinavyohusishwa na Shtaka la Uhaini

Dar es Salaam – Upande wa Jamhuri umeendelea kutoa hoja zake katika kesi ya uhaini, ukieleza mbele ya Mahakama Kuu kuwa ili mtu ashtakiwe kwa kosa hilo, ni lazima awe chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awe ndani au nje ya nchi, pamoja na kuwepo kwa nia inayodaiwa kuhusishwa na kosa hilo.

Katika mawasilisho yake, upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa hati ya mashtaka inahusisha madai kwamba mshtakiwa alikusudia kuchochea umma katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa lengo la kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jamhuri imeeleza kuwa katika kuandaa hati ya mashtaka, baadhi ya maneno yaliyopo kwenye kifungu cha sheria yalitafsiriwa na kuwekwa kwa namna inayolingana na ushahidi ambao upande huo ulitarajia kuutoa mahakamani.

“KUTAMKA MANENO NI KITENDO”

Upande huo umeieleza Mahakama kuwa neno manifestation katika tafsiri ya kisheria linaweza kujidhihirisha kwa njia mbalimbali, ikiwemo kusambaza maandishi au michoro, pamoja na kufanya overt act, yaani kitendo kinachoonekana.

Kwa mujibu wa Jamhuri, hati ya mashtaka inadai kuwa mshtakiwa alidhihirisha nia yake kwa kutamka maneno na kisha kuyasambaza.

Jamhuri imesisitiza kuwa kutamka maneno ni kitendo katika tafsiri ya kisheria, na hoja hiyo inapaswa kuangaliwa pamoja na vipengele vya kosa vinavyotajwa katika sheria.

Aidha, upande huo umeeleza kuwa kuchapisha au kusambaza taarifa kunahusisha kufanya taarifa hiyo ijulikane kwa umma.

NENO “PUBLIC” LAIBIWA

Katika hoja zake, Jamhuri pia imeeleza matumizi ya neno public katika hati ya mashtaka, ikisema mshtakiwa anatuhumiwa kuchochea umma na si kundi maalumu au mtu mmoja.

Kwa mujibu wa hoja hizo, dhana ya public inaweza kumaanisha kundi la watu bila kuwepo kwa idadi maalumu inayotakiwa ili kundi hilo litambuliwe kama umma.

Jamhuri imeeleza kuwa matumizi ya maneno hayo katika hati ya mashtaka yamekusudiwa kufanya maelezo ya shtaka yaendane na ushahidi uliowasilishwa.

“SERIKALI” NA LENGO LA KUITISHA

Katika sehemu nyingine ya mawasilisho, Jamhuri imeeleza kuhusu matumizi ya neno Serikali katika hati ya mashtaka.

Upande huo umesema katika muktadha wa shtaka hilo, neno Serikali limetumika kuhusisha mihimili ya utendaji, bunge na mahakama, huku ukieleza kuwa Kanuni ya Adhabu haina tafsiri mahususi ya maneno executive na judiciary katika kifungu hicho.

Jamhuri imeirejea pia sehemu ya ushahidi ambapo mshtakiwa alieleza kuwa “the executive is responsible” kwa ajili ya kutunza amani, huku jukumu la kulinda amani likihusishwa na polisi walio chini ya Serikali.

Kwa hoja ya Jamhuri, ushahidi huo unaonyesha kuwa jambo lililodaiwa kutishiwa ni Serikali katika jukumu lake la kudumisha amani na utulivu.

“SI LAZIMA KUTHIBITISHA SERIKALI ILITISHIKA”

Jamhuri imeendelea kusisitiza kuwa katika kuthibitisha shtaka, si lazima ionyeshe kwamba Serikali kweli ilitishwa au ilitikisika kutokana na maneno yanayodaiwa kutolewa na mshtakiwa.

Kwa mujibu wa hoja hizo, kinachotakiwa kuangaliwa ni iwapo kulikuwa na nia ya kuitisha Serikali kama inavyodaiwa katika hati ya mashtaka.

Upande wa Jamhuri pia umebainisha kuwa baadhi ya maneno yaliyotumika katika hati ya mashtaka yametokana na vifungu vya sheria, huku mengine yakichaguliwa ili kuendana na mazingira ya ushahidi uliowasilishwa.

Baada ya kukamilisha hoja zake kuhusu masuala hayo, Jamhuri imeendelea kuielekeza Mahakama kwenye vipengele viwili vinavyohusiana na iwapo mshtakiwa alikuwa na nia ya kuitisha Serikali na iwapo matendo yanayodaiwa yanaendana na masharti ya kosa la uhaini.

Kesi hiyo inaendelea mbele ya jopo la Majaji watatu la Mahakama Kuu.