Bundesliga Kufunguliwa Rasmi Agosti 28, Bayern Munich Kuanza Kazi Nyumbani

BERLIN, Ujerumani — Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, inajiandaa kufungua msimu mpya wa 2026/27 Agosti 28, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona ushindani katika mbio za kuwania ubingwa, nafasi za michuano ya Ulaya pamoja na mapambano ya kuepuka kushuka daraja.

Msimu huo utafunguliwa rasmi Ijumaa, Agosti 28, kwa mabingwa watetezi Bayern Munich kuanza kampeni yao mbele ya mashabiki wao dhidi ya VfB Stuttgart.

Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Allianz Arena kuanzia saa 21:30, huku Bayern ikitarajiwa kuanza safari ya kutetea taji lake kwa kutafuta pointi tatu za mwanzo.

Mechi Sita Jumamosi

Jumamosi, Agosti 29, kutakuwa na michezo sita katika ratiba ya Bundesliga.

SV Elversberg itakuwa mwenyeji wa Bayer Leverkusen katika Uwanja wa Ursapharm-Arena an der Kaiserlinde, huku mchezo huo ukipangwa kuanza saa 16:30.

Wakati huo huo, FC Köln itakuwa nyumbani dhidi ya Hoffenheim katika Uwanja wa RheinEnergieSTADION kuanzia saa 16:30.

Mchezo mwingine utawakutanisha Mainz na Paderborn katika Uwanja wa MEWA ARENA, pia kuanzia saa 16:30.

RB Leipzig nayo itaanza msimu nyumbani dhidi ya Borussia Mönchengladbach katika Uwanja wa Red Bull Arena. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 16:30.

Katika mchezo mwingine wa muda huo, Union Berlin itakuwa mwenyeji wa Eintracht Frankfurt katika Uwanja wa Stadion An der Alten Försterei.

Dortmund Kuanzia Nyumbani

Mchezo wa mwisho wa Jumamosi utawakutanisha Borussia Dortmund na Hamburger SV katika Uwanja wa Signal Iduna Park.

Dortmund itakuwa mwenyeji katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 19:30, huku mashabiki wakisubiri kuona namna timu hiyo itakavyoanza msimu mpya.

Michezo Miwili Jumapili

Ratiba ya wiki ya kwanza itahitimishwa Jumapili, Agosti 30, kwa michezo miwili.

Freiburg itakuwa mwenyeji wa Werder Bremen katika Uwanja wa Europa-Park Stadion kuanzia saa 16:30.

Baadaye, Augsburg itakutana na Schalke katika Uwanja wa WWK ARENA kuanzia saa 18:30.

Msimu Mpya Waanza kwa Kishindo

Kwa ujumla, msimu mpya wa Bundesliga unatarajiwa kuanza kwa ushindani mkubwa huku kila timu ikiwa na malengo yake.

Macho mengi yataelekezwa kwa Bayern Munich, ambayo itaanza kampeni ya kutetea ubingwa mbele ya Stuttgart, lakini ushindani kutoka kwa Dortmund, Leipzig, Leverkusen na timu nyingine unatarajiwa kufanya mbio za msimu huu kuwa na mvuto mkubwa.

Mashabiki wa Bundesliga sasa wanasubiri Agosti 28 ifike ili kuona pazia la msimu mpya likifunguliwa rasmi.

Stori na Haika Urio | GPL – TUDACO

Mwenge wazindua madarasa Kagongwa – HabariLeo

SHINYANGA: Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, ameweka jiwe la msingi la jengo la vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kagongwa iliyopo Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Ujenzi wa jengo hilo ulianza kwa nguvu za wananchi waliotoa mchango wa shilingi milioni saba, huku ukamilishaji wake ukifadhiliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kupitia mapato ya ndani kwa kiasi cha Sh milioni 63.

Mwang’onda alisema hayo leo baada ya Mwenge wa Uhuru kupokelewa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kagongwa ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, alipokea mwenge huo.

Amesema amefurahishwa na hatua ya wananchi kushirikishwa katika ujenzi huo na amekubali kuweka jiwe la msingi kwa kuwa mradi huo umefikia hatua nzuri ya ukamilishaji. Aidha, aliwataka wazazi kusimamia maendeleo ya watoto wao na kuhakikisha wanapata elimu bora ili waweze kufaulu katika masomo yao.

Mwang’onda pia aliikabidhi shule hiyo cheti kwa ajili ya Klabu ya Wapinga Rushwa yenye wanafunzi 60, iliyoanzishwa mwaka 2023. Amesema klabu hiyo inaendelea kutoa elimu na kushiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa, jambo ambalo ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa salama.

“Nimezindua pia upandaji wa miti katika shule hiyo. Mazingira yanapaswa kutunzwa na kusimamiwa vizuri, na kila mwanafunzi anatakiwa awe na mti wake wa kuutunza. Hii itasaidia kuboresha mazingira ya kujisomea,” amesema Mwang’onda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amesema mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama.

Amesema mwenge huo utapita kwenye miradi 21 yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.4 na utakimbizwa umbali wa kilomita 361.4.

MAKAME AWAKALIA KOONI MA-DC, UTITIRI WA VITUO VYA UKAGUZI

 

Na Moses Ng’wat, Songwe.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Jabir Omari Makame, amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia kwa karibu utekelezaji wa agizo la kuondoa vituo vya ukaguzi barabarani visivyo na ulazima, akisema utitiri wa vituo hivyo katika umbali mfupi umekuwa kero kwa wafanyabiashara na wananchi.

Makame alitoa maelekezo hayo jana, Agosti 20, 2026, wakati akizungumza katika Jukwaa la Songwe Dira 2050 Forum lililofanyika kwa siku mbili mkoani Songwe, lililolenga kujadili ushirikishwaji wa wadau katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Alisema licha ya agizo la kuondoa vituo visivyo vya lazima kutolewa, baadhi yake bado vinaendelea kuwepo, hali inayolazimu Wakuu wa Wilaya kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na maeneo yao yanaondokana na vituo visivyo na msingi.

“Haiwezekani w

Wilaya moja inakuwa na vituo vingi vya ukaguzi kwa umbali mfupi, hii kero imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara, hivyo Wakuu wa Wilaya simamieni utekelezaji wa maelekezo haya,” alisema.

Katika hatua nyingine, Makame alilitaka Jeshi la Polisi kupunguza vituo vya ukaguzi visivyo vya lazima, akisema utitiri wa vituo hivyo unaongeza usumbufu na kuchelewesha safari.

Alisema kupunguza vituo hivyo hakumaanishi kuondoa ukaguzi barabarani, bali kuufanya kuwa wa ufanisi kwa kubaki na vituo vinavyohitajika kwa ajili ya usalama na udhibiti, bila kuweka vikwazo visivyo vya lazima kwa wasafirishaji.

Makame alisema kupunguza vikwazo vya aina hiyo ni muhimu katika kuboresha mazingira ya biashara, usafirishaji na uwekezaji, ambayo ni maeneo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Alisema Dira 2050 inahitaji mazingira yatakayowezesha wananchi na sekta binafsi kufanya shughuli za kiuchumi kwa ufanisi, hivyo Serikali katika ngazi zote inapaswa kutambua na kuondoa changamoto zinazoweza kuwa kikwazo kwa biashara na uwekezaji.

Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira 2050 unapaswa kuonekana kupitia hatua zinazoboresha mazingira ya biashara, usafirishaji na huduma kwa wananchi, badala ya kubaki katika mijadala na mipango pekee.

Awali ndani ya jukwaa hilo, wadau mbalimbali walilalamikia kuwepo usumbufu mkubwa kwenye ukaguzi hasa Malori katika barabara Kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam) na kusababisha usumbufu na malalamiko mengi.

Usipuuze! Haya Ndiyo Maajabu ya Komamanga Mwilini Wako, Wengi Hawajui!

Komamanga ni miongoni mwa matunda yenye virutubisho mbalimbali vinavyoweza kuwa sehemu ya lishe bora. Tunda hili, linalojulikana kwa jina la kisayansi Punica granatum, limekuwa likitumika katika maeneo mbalimbali duniani kutokana na ladha yake pamoja na matumizi yake katika chakula na vinywaji.

Komamanga hustawi vizuri katika maeneo yenye hali ya hewa ya joto na lina uwezo wa kustahimili vipindi vya ukame. Tunda hilo lina ganda gumu kwa nje na ndani yake kuna mbegu nyingi zenye ute wenye ladha tamu au chachu.

Virutubisho vinavyopatikana kwenye komamanga

Komamanga lina virutubisho mbalimbali muhimu, miongoni mwao vikiwa:

  • Vitamin C
  • Vitamin E
  • Vitamin K
  • Folate
  • Potassium
  • Nyuzi lishe (fiber)
  • Antioxidants, hasa polyphenols

Mbegu za komamanga pia zina kiasi cha mafuta yenye virutubisho, huku tunda zima likiwa na maji kwa kiwango kikubwa.

Komamanga lina faida gani mwilini?
1. Lina antioxidants nyingi
Komamanga lina kemikali za mimea zinazojulikana kama antioxidants. Antioxidants husaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na free radicals.

2. Husaidia afya ya moyo
Utafiti umeonyesha kuwa matumizi ya komamanga yanaweza kuwa na mchango katika afya ya moyo na mishipa ya damu. Hata hivyo, halipaswi kuchukuliwa kama dawa ya kutibu ugonjwa wa moyo au presha.

3. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo
Kwa kuwa mbegu zake zina fiber, komamanga linaweza kusaidia katika lishe inayochangia mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula na utendaji wa kawaida wa utumbo.

4. Huongeza virutubisho mwilini
Vitamin na madini yaliyomo kwenye komamanga yanaweza kusaidia kukamilisha mahitaji ya virutubisho katika lishe ya kila siku.

5. Linaweza kusaidia kupunguza madhara ya oxidation
Antioxidants zilizomo kwenye komamanga zimefanyiwa tafiti kuhusu nafasi yake katika kulinda mwili dhidi ya uharibifu wa seli. Hata hivyo, si sahihi kusema kwamba komamanga linatibu au kuzuia saratani moja kwa moja.

Kwa wanaume

Komamanga limekuwa likifanyiwa tafiti pia kuhusu afya ya wanaume, ikiwemo afya ya moyo na mishipa ya damu. Baadhi ya tafiti ndogo zimechunguza uhusiano wake na afya ya uzazi na utendaji wa tendo la ndoa, lakini ushahidi bado hautoshi kulichukulia tunda hili kama tiba ya tatizo lolote la nguvu za kiume.

Je, juisi ya komamanga ni bora kuliko tunda lenyewe?

Si lazima. Kula tunda lenyewe kunakupa fiber inayopatikana kwenye mbegu, wakati juisi inaweza kuwa rahisi kunywa lakini mara nyingi huwa na fiber kidogo.

Pia, si lazima kunywa nusu lita ya juisi ya komamanga kila siku ili kupata faida zake. Kiasi kinachofaa kinategemea mlo wa mtu kwa ujumla.

Komamanga ni sehemu nzuri ya lishe bora, lakini si dawa ya kutibu saratani, vidonda vya tumbo, presha, kisukari au magonjwa mengine. Watu wanaotumia dawa za kudhibiti presha au dawa nyingine za kudumu wanapaswa kushauriana na mtaalamu wa afya kabla ya kutumia juisi ya komamanga kwa kiasi kikubwa.

Kwa kifupi: Komamanga ni tunda lenye antioxidants, vitamins, madini na fiber na kulifanya sehemu ya mlo kamili kunaweza kuwa na manufaa kwa afya kwa ujumla.

iku ili kupata faida zake. Kiasi kinachofaa kinategemea mlo wa mtu kwa ujumla.

Muhimu

Komamanga ni sehemu nzuri ya lishe bora, lakini si dawa ya kutibu saratani, vidonda vya tumbo, presha, kisukari au magonjwa mengine. Watu wanaotumia dawa za kudhibiti presha au dawa nyingine za kudumu wanapaswa kushauriana na mtaalamu wa afya kabla ya kutumia juisi ya komamanga kwa kiasi kikubwa.

Kwa kifupi: Komamanga ni tunda lenye antioxidants, vitamins, madini na fiber—na kulifanya sehemu ya mlo kamili kunaweza kuwa na manufaa kwa afya kwa ujumla.

Mahakama Yasema Tundu Lissu Ana Kesi ya Kujibu

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Agosti 21, 2026 imemkuta na kesi ya kujibu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Uamuzi huo umetolewa na kusomwa na kiongozi wa jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji Dunstan Ndunguru, kwa niaba ya majaji wenzake.

Jaji Ndunguru amesema baada ya kupitia na kuzingatia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka pamoja na hoja za mshtakiwa, mahakama imejiridhisha kuwa Lissu ana kesi ya kujibu.

Lissu anashtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyorekebishwa mwaka 2023.

Kosa hilo linahusishwa na kauli alizotoa katika mkutano uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam, Aprili 3, 2025, kuhusu msimamo wa chama hicho wa kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na nia ya kuzuia uchaguzi huo.

Katika shtaka hilo, Lissu anadaiwa kuwa akiwa raia wa Tanzania, kwa nia ya uchochezi, alishawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa kutoa kauli na maandishi yaliyolenga kumshinikiza kiongozi mkuu wa Serikali ya Tanzania.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Ndunguru amesema katika hatua hii mahakama inapaswa kuangalia iwapo, kwa kuzingatia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, mshtakiwa anaweza kutiwa hatiani. Amesema mahakama haihitajiki katika hatua hiyo kuingia kwa undani katika kuchambua ushahidi au kutathmini kiwango cha kuaminika kwake.

Katika kufikia uamuzi huo, mahakama imezingatia viini vitatu vya kosa la uhaini ambavyo upande wa mashtaka ulipaswa kuvithibitisha.

Jaji Ndunguru amesema moja ya mambo yaliyozingatiwa ni utii wa mshtakiwa kwa Jamhuri. Kwa kuwa Lissu alikiri kuwa ni raia wa Tanzania, mahakama imeona kipengele hicho kimeungwa mkono na ushahidi uliowasilishwa.



Vikundi vya michezo kunufaika mikopo asilima 10 – HabariLeo

MOROGORO: MBUNGE wa Jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro, Sara Msafiri, amevitaka vikundi ambavyo vitashiriki kwenye tamasha la michezo kwenye jimbo hilo vitakuwa vya kijasiriamali na vitasaidiwa usajili ili vipate kunufaika na fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.

Msafiri amesema hayo wakati akizindua Tamasha la Sara Festival litakalohusisha mashindano ya mpira wa miguu ,ngoma za asili na riadha kwa kushirikisha vijiji vyote 130 vilivyopo katika kata 30 katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema lengo la tamasha hilo si tu kuibua vipaji vya vijana bali ni njia sahihi ya kuhimiza vijana kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa vijana ,wanawake na makundi maalumu.

“Kikundi cha ngoma , timu za mpira wa miguu pamoja na riadha za kutoka vijiji vyote 130 vilivyopo ndani ya wilaya yetu kitakachoshiriki pia kitageuzwa kuwa ni cha ujasiriamali na kitasaidiwa kusajiliwa na halmashauri kinufaike na asilimia 10,” amesema Msafiri.

Msafiri amewataka washiriki wa tamasha hilo kuhakikisha wanatumia fursa ya kujitangaza vizuri kwa sababu litakuwa jukwaa kubwa litakalofuatiliwa na watu wengi na hivyo kuwafungulia njia ya kushiriki matamasha ya kitaifa na kimataifa

Mbunge huyo ametolea mfano kuwa ngoma za kabila la Waluguru zimekuwa zikiwavutia watu wengi kutokana na kuendelea kudumisha mila zenye kusisitiza maadili, desturi na utamaduni wa Mwafrika

Naye, Mwenyekiti wa Chimbuko Band na Kikundi cha Ngoma ya Asili ya Mdundiko kutoka Kijiji cha Tangeni, John Mkude amesema kikundi hicho kinazaidi ya miaka 50 na kimekosa kuungwa mkono wa ufadhili kutoka kwa wadau na kujikuta wakibaki katika hali duni ya kiuchumi.

Mkude amesema kikundi hicho kina wanachama 37 na kinafanya shughuli za utumbuizaji kwenye halfa za kijadi asili na kuingiza kipato kwa ajili ya kugawana ili kukidhi mahitaji ya kifamilia pekee.

Kwa upande wake Msanii na Mweka hazina wa kikundi hicho, Benard Shaban amempongeza Mbunge kwa kuanzisha tamasha hilo ambalo litawasadia wasanii wa ngoma za asili kutangaza vipaji vyao na kwa makundi mengine.

‘Ugatuzi wa madaraka muhimu kufanikisha Dira 2050’ – HabariLeo

DODOMA: NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (anayeshughulikia afya), Jafar Seif, amesema ugatuzi wa madaraka ni miongoni mwa misingi muhimu ya kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuziimarisha Serikali za Mitaa ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akifungua mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa(TaOA) Dk Seif alisema kufikiwa kwa malengo ya Dira 2050 kutategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa Serikali za Mitaa kusimamia na kutekeleza mipango ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi katika maeneo yao.

Alisema Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya kiutendaji pamoja na usimamizi wa fedha za umma, ikiwemo utaratibu wa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo moja kwa moja katika taasisi za Serikali za ngazi za chini.

Taasisi zinazofikiwa na utaratibu huo ni pamoja na shule, zahanati, ofisi za kata na vijiji, hatua inayolenga kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Pia alisema Serikali za Mitaa zina nafasi muhimu katika kuhakikisha malengo ya maendeleo yanafikiwa kutokana na kuwa ndizo zilizo karibu zaidi na wananchi na zinaelewa kwa undani mahitaji na changamoto zinazowakabili.

“Fursa ya kufikia Dira ya Taifa 2050 inahitaji Serikali za Mitaa zenye uongozi bora na uwajibikaji, mipango madhubuti ya maendeleo na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma,” amesema.

Aidha, Dk Seif amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi na kuimarisha uwajibikaji katika ngazi mbalimbali za Serikali.

Alisema kuimarishwa kwa mifumo ya kiutendaji katika Serikali za Mitaa kutasaidia kuhakikisha rasilimali zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa tija na kuleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Kigoma yatarajia kuuza kilo milioni 15 za tumbaku – HabariLeo

KIGOMA: Zaidi ya kilo milioni 15 za tumbaku zinatarajiwa kuuzwa na wakulima kwa kampuni za ununuzi wa zao hilo mkoani Kigoma kwa msimu huu wa kilimo.

Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB), Elisha Chao, amesema hayo akiwasilisha taarifa ya bodi hiyo kwa wajumbe wa kikao cha wadau wa kahawa mkoa Kigoma kilichofanyika mjini Kigoma jana.

Chao amesema hadi sasa kilo milioni 15 zimenunuliwa na bado kuna tumbaku ipo sokoni na wanunuzi wanaendelea na taratibu za ununuzi kwenye masoko hayo.

Amesema mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji kutokana na soko lililokuwepo msimu uliopita na bei iliyokuwepo na kwamba TTB inasimamia kwa karibu kuhakikisha tumbaku iliyiozalishwa inaunuliwa yote.

Akizungumza katika mkutano huo Mkoa wa Kigoma Balozi ,Simon Sirro, ametaka wadau wa zao la tumbaku nchini kusimamia taratibu za kilimo na uuzaji wa zao hilo ili kuhakikisha mkulima ananufaika na kuwa na maendeleo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma amesema uzalishaji wa zao la tumbaku mkoani humo umeendelea kuongezeka, kutoka tani 4,452 mwaka 2021/2022 hadi tani 14,213 mwaka 2024/2025.

Amesema ongezeko hilo la uzalishaji limechochea pia kuongezeka kwa mapato ya Serikali, kutoka Sh bilioni 15.4 mwaka 2023/2024 hadi Sh bilioni 26.9 mwaka 2025/2026.

Wabuni vigae vya ukutani kwa kutumia chupa za plastiki – HabariLeo

TANGA; Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) kimeendelea kujipambanua kama kitovu cha tafiti na bunifu zinazotoa majibu ya moja kwa moja kwa changamoto zinazoikabili jamii, huku kikisisitiza mfumo wa vitendo kwa wanafunzi wake kabla ya kuhitimu.

Akizungumzia juhudi hizo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa, amesema chuo kimeimarisha mfumo ambapo kila muhula wanafunzi wanafanya miradi ya vitendo chini ya usimamizi wa wahadhiri na kuiteetea kama sehemu ya mitihani yao.

“Kila muhula wanafunzi wanasimamiwa na kufanya miradi chini ya usimamizi wa walimu, na wanazitetea kama sehemu ya mitihani yao,” anaeleza Profesa Liwa, akisisitiza kuwa mbinu hiyo inawafanya wahitimu kuwa na uelewa mpana katika kutatua changamoto za kiutendaji.

Katika kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira inayotokana na taka ngumu, Chuo Kikuu cha Ardhi kimeleta tija kupitia uvumbuzi mpya wa kutengeneza vigae vya ukutani (wall tiles) vinavyotokana na chupa za plastiki.

Mwanamapinduzi wa wazo hili ni Isabellah Edwin Sam, mwanafunzi wa mwaka wa nne chuoni hapo, ambaye alibaini kuwa chupa za plastiki za rangi zimekuwa zikitupwa kwa wingi kutokana na bei yake kuwa chini, hali inayochochea uchafuzi mkubwa wa mazingira.

Ili kupunguza kadhia hiyo, Isabellah alibuni mbinu ya kuchakata taka hizo na kuzigeuza kuwa vigae imara vinavyoweza kutumika katika ujenzi wa kuta, hususan katika maeneo ya bafu na vyoo.

Akizungumzia ubora wa uvumbuzi wake, Isabellah ameeleza kuwa bidhaa hiyo ni thabiti na inaendelea kuboreshwa zaidi.

Amesema hatua inayofuata ni kuwasilisha vigae hivyo katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya kupata uthibitisho rasmi kabla ya kuanza kutumika kwa wingi katika soko la ujenzi.