CCM Yampendekeza Ndejembi Kuwa Makamu wa Rais

Global Publishers
August 27, 2026
36 views
0 Comments

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, ametangaza kuwa vikao vya Chama hicho vilivyokutana jana na leo jijini Dar es Salaam vimempitisha kwa kauli moja Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Migiro amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya vikao husika vya CCM kujadili na kuridhia jina la Mhe. Ndejembi, ambaye ni mwanachama wa chama hicho, kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo iliyo wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Amesema baada ya taratibu za ndani ya chama kukamilika, jina la Mhe. Ndejembi litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

ALIYEKUWA MKUU WA WALINZI WA RAIS KAGAME AFARIKI GEREZANI

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

Aliyekuwa mkuu wa walinzi wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Tom Byabagamba, amefariki dunia akiwa gerezani nchini Rwanda, ambako alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 15. Alikuwa na umri wa miaka 59.

Byabagamba, ambaye pia aliwahi kuwa mlinzi binafsi wa Rais Kagame, alikamatwa mwaka 2014 pamoja na shemeji yake, Brigedia Jenerali mstaafu Frank Rusagara.

Mwaka 2016, Mahakama Kuu ya Kijeshi nchini Rwanda ilimhukumu Byabagamba kifungo cha miaka 21 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa yaliyohusisha kuchochea uasi na kuchafua taswira ya Serikali. Hata hivyo, mwaka 2019 Mahakama ya Rufaa ilipunguza adhabu hiyo hadi miaka 15. Byabagamba alikuwa amekanusha mashtaka dhidi yake.

Kifo chake kimethibitishwa na kaka yake, David Himbara, ambaye amesema familia bado haijafahamu chanzo cha kifo hicho. Kwa mujibu wa Himbara, familia haikuruhusiwa kumuona Byabagamba katika kipindi cha miaka aliyokuwa gerezani.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliwahi kukosoa mwenendo wa kesi ya Byabagamba na Rusagara, yakidai kulikuwa na dosari katika mchakato wa kesi pamoja na madai ya mateso na kuingiliwa kwa mashahidi.

Rusagara, ambaye alihukumiwa katika kesi hiyo hiyo, naye alifariki akiwa gerezani Machi 2025.

Byabagamba ameacha mke na watoto wawili wa kiume. Hadi taarifa za awali zilipotolewa, mamlaka za Rwanda hazikuwa zimetoa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha kifo chake.

TRA United yaanza maandalizi kuivaa Dodoma Jiji FC – HabariLeo

ARUSHA: TIMU ya TRA United imezindua Wiki ya Shamra Shamra yenye matukio mbalimbali ya kijamii na uhamasishaji kuelekea mechi yake ya kwanza ya nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji itakayochezwa Jumamosi, Agosti 29, 2026.

Mchezo huo pia utatumika kutambulisha wachezaji wao wa msimu huu wa 2026/2027.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Deogratius Shuma, amesema klabu hiyo inatumia soka kama njia ya kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu faida za kulipa kodi na kudai risiti.

Alisema TRA ilianzisha timu hiyo kutokana na umuhimu wa soka kama mchezo unaopendwa na watu wengi, hivyo kuwezesha mamlaka hiyo kufikisha kwa urahisi ujumbe wa ulipaji kodi kwa wananchi.

“Mbali na kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari, timu pia imeanzishwa kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana na kuonyesha faida zinazotokana na mapato ya kodi,” amesema.

Amesema kupitia TRA United, mamlaka hiyo pia itaendelea kutoa elimu kuhusu mifumo mbalimbali inayotumika katika kurahisisha ulipaji na usimamizi wa kodi.

Ofisa Habari wa TRA United, Christina Mwagala, amesema Wiki ya ‘Shamra Shamra’ itajumuisha matukio mbalimbali, yakiwemo uhamasishaji mitaani na shughuli za kurudisha kwa jamii.

Amesema kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa, timu hiyo itafanya hamasa katika maeneo mbalimbali jijini Arusha, sambamba na kutembelea taasisi za soka na pia kutoa msaada kwa watoto yatima.

“Tumekuwa tukifanya shughuli za kurudisha kwa jamii, lakini mara nyingi tunafanya bila kwenda na vyombo vya habari kwa sababu tunaamini ni sehemu ya sadaka yetu kwa jamii,”

Mwagala amesema timu hiyo imeanza msimu kwa kucheza michezo mitatu ya ugenini, ikipata pointi mbili baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania, kufungwa mabao 2-1 na Azam FC na kutoka sare dhidi ya Coastal Union mjini Tanga.

Ameeleza pamoja na matokeo hayo kutokuwa katika malengo yaliyowekwa na klabu, bado ni mwanzo wa msimu na timu ina matumaini ya kufanya vizuri katika mechi za nyumbani.

Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, TRA United itakuwa na mchezo mwingine wa nyumbani dhidi ya Mbeya City Septemba 4.

Wanafunzi 1,700 Bagaza wafaidika msaada wa mahindi, sukari – HabariLeo

GEITA: TAASISI ya Mapung’o Foundation imetoa msaada wa magunia 30 ya mahindi na kilo 250 za sukari kwa Shule ya Msingi Bagaza iliyopo Kata ya Butobela wilayani Geita.

Msaada huo unalenga kusaidia upatikanaji wa uji shuleni hapo kwa wanafunzi zaidi ya 1,700 na kuwatengenezea mazingira bora ya kujifunzia ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu na ufaulu.

Mratibu wa Mapung’o Foundation, Marco Victor amekabidhi msaada huo kwa niaba ya taasisi na kueleza kuwa taasisi hiyo imejizatiti kusaidia mahitaji ya wanafunzi kwa manufaa ya jamii.

Ofisa Elimu wa Kata ya Butobela, John Otieno amekiri kuwa msaada huo utasaidia kuinua kiwango cha elimu na kuleta ahueni ya michango ya chakula kwa wazazi.

Otieno amewaomba wadau wengine kuiga mfano wa Mapung’o Foundation kwa kujitolea kuchangia vyakula mashuleni, akieleza kuwa hatua hiyo inaimarisha afya na maendeleo ya elimu kwa watoto.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bagaza, Damasi Madata, amesema shule hiyo hutumia debe tatu za mahindi kwa siku kwa ajili ya uji hivo magunia 30 ya mahindi pamoja na kilo 250 za sukari vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuendesha programu ya lishe shuleni.

WAFANYABIASHARA WA LIBRARY ZA VIDEO IRINGA WATISHIA KUTOFANYA KAZI NA UMOJA MOVIES

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

UMOJA wa wafanyabiashara wa filamu maarufu kama Library za Video mkoani Iringa umeazimia kusitisha kwa muda kufanya kazi na kampuni ya Umoja Movies, ili kutoa nafasi kwa viongozi na wawakilishi wa wadau kukutana na kampuni hiyo kujadili changamoto zinazodaiwa kujitokeza katika mfumo mpya wa usambazaji wa kazi za filamu.

Akizungumza na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Library Mkoa wa Iringa, Joshua Sanga  amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau kuhusu mfumo mpya uliowekwa na kampuni hiyo, hivyo kuna umuhimu wa pande zote kukutana na kutafuta suluhisho.

Sanga alisema moja ya hoja zinazohitaji ufafanuzi ni suala la usalama wa mfumo huo, hususan namna unavyolinda kazi pamoja na taarifa zilizohifadhiwa katika kompyuta za watumiaji.

Kwa mujibu wa Sanga  wafanyabiashara wanahitaji kupewa maelezo ya kutosha kuhusu mfumo huo na namna unavyofanya kazi kabla ya kuanza kuutumia kwa kiwango kikubwa.

Alisema ni muhimu kampuni kuwashirikisha wadau wanaotumia mfumo moja kwa moja kabla ya kuanzisha mabadiliko makubwa, ili kupata maoni yao na kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza kabla ya utekelezaji kamili.

Mwenyekiti huyo amesema wafanyabiashara wa filamu na kampuni wanapaswa kukaa pamoja na kujadiliana ili kubaini namna mfumo huo utakavyoweza kuwa na manufaa kwa pande zote.

“Umoja Movies inafanya biashara kwa lengo la kupata mapato, huku wadau nao wakitegemea kazi hizo kama chanzo cha kipato, hivyo ni muhimu kuwepo kwa usawa wa maslahi,” amesema.

Ameongeza kuwa wamependekeza utekelezaji wa mfumo huo usitishwe kwa muda ili kutoa nafasi kwa viongozi na wawakilishi wa wafanyabiashara kufanya mazungumzo na kampuni.

“Kuanzia sasa napendekeza kampuni kusitisha utekelezaji wa mfumo huo kwa muda ili kutoa nafasi kwa viongozi na wawakilishi wa wadau kukutana na kampuni na kujadili kwa kina changamoto zilizopo pamoja na namna bora ya kuendesha mfumo huo,” amesema.

Sanga alisema iwapo kampuni itaendelea na mfumo huo bila kufikiwa kwa makubaliano, umoja huo utaangalia njia nyingine zitakazowawezesha wanachama wake kuendelea kufanya kazi na kujipatia kipato.

Amefafanua kuwa hatua hiyo hailengi kuvunja ushirikiano uliopo, bali inalenga kuhakikisha maslahi ya wafanyabiashara na wadau wengine katika sekta hiyo yanazingatiwa.

Amesisitiza kuwa umoja huo una malengo ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa filamu pamoja na kuibua fursa kwa vijana wenye vipaji na wanaotegemea biashara hiyo kama chanzo cha ajira na kipato.

Amesema Mkoa wa Iringa una vijana wengi wenye uwezo na vipaji ambao wanahitaji mazingira rafiki ya kuendeleza shughuli zao na kujipatia kipato.

“Nawaomba wanachama tuendelee kushikamana na kuwa na sauti moja katika masuala yanayotuhusu, kwa sababu umoja ndio msingi wa kupata suluhisho la changamoto zetu. Kupitia ushirikiano huo tunaweza kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ya filamu na kuhakikisha sekta hiyo inanufaisha pande zote,” amesema.

Kwa upande wake, Katibu wa Wafanyabiashara wa Library za Video, Erick Mushi, amesema baadhi ya watumiaji wamedai kukumbana na changamoto za kiufundi katika matumizi ya mfumo huo, ikiwemo kutofanya kazi kwa ufanisi katika baadhi ya kompyuta zinazotumia matoleo tofauti ya mfumo wa Windows.

Mushi amesema changamoto hizo zimejitokeza baada ya mfumo kuanza kutumika, hivyo wameomba kupewa muda wa kutosha kuujifunza, kuufanyia majaribio na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kabla ya utekelezaji wake kwa kiwango kikubwa.

Amesema wanaamini mazungumzo kati ya kampuni na wafanyabiashara yanaweza kusaidia kupata suluhisho litakalolinda maslahi ya pande zote na kuwezesha biashara ya filamu kuendelea katika mazingira mazuri.TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Msiba Kibaha: Polisi Wawili Wapoteza Maisha Kwa Kugongwa na Gari, Waagwa Tumbi

Pwani. Jeshi la Polisi limewapoteza askari wake wawili katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Maili Moja, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, baada ya kugongwa na gari wakati wakiwa katika eneo la kivuko cha watembea kwa miguu.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Agosti 25, 2026, majira ya saa 1:40 katika barabara kuu ya Dar es Salaam–Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T.804 ERM, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mlandizi, liliwagonga watembea kwa miguu katika eneo la zebra.

Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Josia Isaya Arute, mwenye umri wa miaka 34, mkazi wa Mlandizi.

Inadaiwa kuwa wakati dereva huyo akifika katika eneo hilo, magari kadhaa yalikuwa yamesimama ili kuwawezesha watembea kwa miguu kuvuka. Hata hivyo, gari hilo lilipita upande wa magari hayo na kuwagonga waliokuwa wakivuka.

Miongoni mwa waliogongwa walikuwa askari wawili wa Polisi, Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa.

Izdory alifariki dunia kutokana na ajali hiyo, wakati Rehema alipata majeraha kichwani na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi kwa ajili ya matibabu.

Kwa bahati mbaya, Rehema alifariki dunia asubuhi ya Agosti 26, 2026, wakati akiendelea kupata matibabu.

Baada ya ajali, dereva wa gari hilo aliondoka katika eneo la tukio. Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanya msako na kulifanikiwa kulikamata gari hilo katika eneo la Kwa Mfipa, Kibaha, likiwa limefichwa.

Gari hilo limepelekwa Kituo cha Polisi Kibaha kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi za kisheria.

Askari hao wameagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi kabla ya kusafirishwa kwenda mikoani kwa ajili ya mazishi.

Ibada hiyo ya kuaga imeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, na kuhudhuriwa na askari wa vyeo mbalimbali pamoja na ndugu na waombolezaji.

Mwili wa Rehema Juma Magawa umepelekwa Korogwe, Tanga, huku mwili wa Izdory George Michael ukisafirishwa kwenda Sumbawanga Vijijini, Rukwa, ambako mazishi yao yatafanyika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeendelea kutoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuheshimu alama za barabarani, hususan maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu, ili kuepusha vifo na majeraha yanayotokana na ajali.

Msiba Kibaha: Polisi Wawili Wapoteza Maisha Kwa Kugongwa na Gari, Wameagwa Tumbi

Msiba Kibaha: Askari Wawili wa Polisi Wapoteza Maisha Kwa Ajali ya Gari

Miili ya askari yaagwa Tumbi

Leo, Agosti 26, miili ya askari hao imeagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi kabla ya kusafirishwa kwenda mikoani kwa ajili ya mazishi.

Ibada hiyo ya kuaga imeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase, na kuhudhuriwa na askari wa vyeo mbalimbali pamoja na ndugu na waombolezaji.

Mwili wa Rehema Juma Magawa umepelekwa Korogwe, Tanga, huku mwili wa Izdory George Michael ukisafirishwa kwenda Sumbawanga Vijijini, Rukwa, ambako mazishi yao yatafanyika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeendelea kutoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuheshimu alama za barabarani, hususan maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu, ili kuepusha vifo na majeraha yanayotokana na ajali.

Meridianbet yawasha moto, TSh milioni 75 zawikwa kwenye Prize Drops

Meridianbet imewasha moto wa zawadi kupitia Rewards Burst Prize Drops, promosheni inayowapa wachezaji nafasi ya kunasa zawadi za papo hapo wakati wa kushiriki mchezo unaokidhi vigezo. Hapa, kila raundi inaweza kubeba sapraizi mpya, kuanzia zawadi za fedha taslimu hadi vizidishi vinavyoweza kufika mbali.

Kile kinachovutia zaidi ni nafasi ya kushinda hadi TSh 75,000,000 kama zawadi kuu. Kila mwezi, mchezaji mmoja anaweza kuchaguliwa kwa bahati na kutwaa zawadi hiyo kubwa. Lakini fursa hazipo kwa mshindi huyo pekee, maelfu ya zawadi hutolewa kila mwezi, huku wachezaji wakiwa na nafasi ya kupata vizidishi kila siku kuanzia x5 hadi x1,000.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa mfano, mchezaji anayecheza dau la TSh 600 na kupata kizidishi cha x500 anaweza kupata TSh 300,000. Hii inatokana na hesabu ya dau linalokidhi masharti wakati Prize Drop inapotolewa, na kiwango cha juu cha dau kinachozingatiwa ni TSh 3,000. Kwa hiyo, unapokutana na kizidishi kikubwa, dau linalostahili linaweza kuleta zawadi yenye tofauti kubwa.

Kuingia kwenye promosheni ni rahisi na hakuna safari ndefu. Ingia kwenye akaunti yako, weka dau linalostahili, chagua mchezo unaoshiriki na cheza. Kisha, bahati ndiyo itaamua kama Prize Drop itatua kwako. Kwa kuwa zawadi zinapatikana kila siku na maelfu ya zawadi zipo kila mwezi, kila raundi inayokidhi masharti inaweza kuwa mwanzo wa sapraizi nyingine.

Uko tayari kuona Burst ya zawadi? Basi usiache nafasi ipite. Rewards Burst Prize Drops inakupa nafasi ya kuwania zawadi kuu ya TSh 75 milioni, huku vizidishi vikifikia x1,000.