Taifa Group Yatoa Tahadhari Jukwaa Feki la Uwekezaji ‘TaifaAI’

Hashpower7113
September 5, 2026
96 views
0 Comments

TAIFA Group imewaonya wananchi kuhusu jukwaa feki la uwekezaji linalotumia jina “TaifaAI”, likidai kuhusishwa na mfanyabiashara Rostam Aziz na Taifa Group.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 4, 2026, Taifa Group imesema maudhui kuhusu jukwaa hilo yanasambazwa kupitia Facebook, Instagram na mitandao mingine ya kijamii, yakitumia jina, picha na utambulisho wa Rostam Aziz pamoja na Taifa Group.

Taifa Group imekanusha kuwa na uhusiano wowote na “TaifaAI”, ikisisitiza kuwa Rostam Aziz hajaanzisha, hajaidhinisha wala kulitangaza jukwaa hilo.

Kampuni hiyo imewaonya wananchi wasijiandikishe, wasitoe taarifa binafsi au za benki, wasitume fedha na wasifanye miamala na watu wanaodai kuiwakilisha “TaifaAI” au Taifa Group.

Aidha, Taifa Group imesema Rostam Aziz hatumii jina au nafasi yake kuhamasisha wananchi kujiunga na miradi ya uwekezaji au mifumo ya biashara mtandaoni inayowaahidi faida za haraka za kifedha.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa inachukua hatua kwa kuwasilisha taarifa za utapeli huo kwa mamlaka husika pamoja na watoa huduma wa mitandao ambako maudhui hayo yanasambazwa.

Taifa Group imewasihi wananchi kuwa waangalifu na kutegemea njia rasmi za mawasiliano za kampuni hiyo pekee kupata taarifa kuhusu shughuli zake.

Taarifa hii imetolewa na Taifa Group, Septemba 4, 2026.

MAKAMU WA RAIS DKT NDEJEMBI ASHIRIKI MISA TAKATIFUYA KUWEKWA WAKFU MHASHAMU VINCENT MPWAJI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa Wakfu Mhashamu Vincent Mpwaji, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, iliyofanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center – Dar es Salaam, leo tarehe 05 Septemba 2026.

 

Misa hiyo, imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, ambaye ni Askofu kiongozi katika uwekaji Wakfu, akisaidiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Henry Mchamungu.

 

Pia, Adhimisho hilo limehudhuriwa na Maaskofu kutoka Majimbo Katoliki mbalimbali nchini, Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Taasisi, Mapadre, Watawa, familia, ndugu, marafiki pamoja na waumini kutoka maeneo mbalimbali.

 

Masauni Aongoza Usafi Buguruni, Asema Agizo la Jumamosi Bado Lipo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni, ameongoza zoezi la usafi katika Soko la Buguruni jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kuwa agizo la kutumia siku ya Jumamosi kwa ajili ya usafi wa mazingira bado lipo na linapaswa kutekelezwa.

Masauni amesema usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na kwamba mamlaka za Serikali zinapaswa kuhakikisha agizo hilo linasimamiwa na kutekelezwa katika maeneo yote.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Masauni amekumbusha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akisimamia sekta ya mazingira, alitoa maelekezo ya siku ya Jumamosi kutumika kama siku maalumu ya usafi nchini.

Amesema pamoja na agizo hilo kutolewa, baadhi ya watu wamekuwa wakishindwa kulitekeleza kwa sababu mbalimbali.


“Leo nachukua nafasi hii kuwaambia kuwa maelekezo ya Makamu wa Rais Dk. Samia Hassan Suluhu, ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye nia njema ya kuhakikisha miji yote inakuwa safi, lile agizo halijafa,” amesema Masauni.

Amezitaka mamlaka zote za Serikali kuhakikisha zinasimamia utekelezaji wa agizo hilo na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi kila Jumamosi.

Masauni amesema usafi wa mazingira ni muhimu zaidi wakati wa msimu wa mvua, akieleza kuwa uchafu unaoweza kuziba mifumo ya maji unaweza kuongeza hatari ya mafuriko na kusababisha kuenea kwa magonjwa.

Ametaja kipindupindu na magonjwa mengine kuwa miongoni mwa madhara yanayoweza kujitokeza endapo mazingira yataachwa machafu.

Amesema kila mwananchi anapaswa kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha eneo analoishi au kufanyia biashara linakuwa safi.
“Nimeona sokoni watu wana maduka madogomadogo. Kuna shida gani kuweka usafi kwenye eneo ulilopo? Viongozi wakisimamia hilo la usafi, maeneo yote yatakuwa safi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Masauni ameiomba Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupewa nguvu zaidi kisheria na kiutendaji ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Amesema NEMC inapaswa kuwa na uwezo wa kutosha katika kusimamia sheria za mazingira, kudhibiti uchafuzi wa mazingira na kuchukua hatua dhidi ya watu wanaokiuka taratibu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema zoezi la usafi linaendelea na lengo ni kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi.

Mpogolo amesema Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kutekeleza maelekezo ya usafi kwa kusimamia usafi katika masoko, barabara na maeneo mbalimbali.
“Tumeendelea kusimamia agizo katika kila soko, kila barabara kuhakikisha usafi unaendelea kufanyika,” amesema Mpogolo.

Amesema juhudi za kuhakikisha mazingira yanakuwa safi zinapaswa kuendelea, huku akiwataka viongozi na wananchi kutokubali kuridhika bali kuongeza bidii katika kutekeleza majukumu yao.

Zoezi hilo la usafi katika Soko la Buguruni limekuja ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali na mamlaka za maeneo kuhakikisha usafi wa mazingira unasimamiwa kwa pamoja na wananchi wanashirikishwa katika kulinda mazingira yao.

Mechi za kibabe Ulaya Kuamua Hatma ya Pointi Wikendi hii

Je unajua kuwa Wikendi hii unaweza ukaokota mkwanja wa maana kwani tayari mechi za kibabe zipo kwaajili yako. Kule Uingereza, Italia mpaka Ujerumani. Tengeneza jamvi la ushindi hapa.

SERIE A kule Italia itaendelea Inter Milan watawaalika vijana wa Allegri Napoli kupambania pointi 3 kwenye dimba la San Siro mchezo ambao utakuwa ukitazamwa na watu wengi lakini wenye pesa ndefu pale Meridianbet.

Ikumbukwe kuwa Inter ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, huku wakiwa wameanza ligi vyema kabisa  baada ya kushinda mechi zake mbili huku wakiwa na kikosi kizuri kabisa cha kupata ushindi mnono.

Napoli wao wakiwa na kocha mpya wametoka kupoteza mechi iliyopita wakiwa nyumbani kwao hivyo wanatazamia kushinda mtanange huu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri za juu na hawataki kupoteza mechi ya pili mfululizo kwani uwezo wa kupambania timu wanao.

Timu zote zina wachezaji wakubwa na wazoefu kama pale Inter kuna Lautaro, Barella, Calhanoglu, Dimarco na wengine wengi, huku kwa Napoli wao wana De Bruyne, Hojlund, Anguissa, McTominay na wengine ambao kwa pamoja wanapamania timu kupata ushindi. Beti sasa hapa.

Msimu uliopita walipokutana kwenye ligi mechi zote mbili, Napoli waliondoka na pointi 4 kwa maan awlaishinda mechi ya kwanza wakiwa nyumbani, huku mechi ya pili wakitoa sare. Jisajili hapa kumpata mshindi.

Piga pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ligi kuu ya Hispania, LALIGA kuna mechi nyingi sana leo lakini sisi tutaiangazia mechi ya Athletic Bilbao dhidi ya Atletico Madrid chini ya kocha mkuu Diego Simeone ambao msimu huu wameanza kwa kasi ya ajabu, kasi ya kushinda taji la ligi kuu.

Lakini je unajua kuwa una nafasi ya kuibuka bingwa ndani ya Meridianbet ukibashiri mechi hii?. Bilbao ikiwa nyumbani inahitaji kupata matokeo ya pointi 3, mbele ya mashabiki zao baada ya kuondoka na ushindi kwenye mechi yake iliyopita.

Lakini mpaka sasa kwenye mechi 3 ambazo amecheza ameshinda mechi moja pekee, hivyo ushindi huu utakuwa na maana sana kwa upande wao kwani wachezaji waoa wazuri na dirisha kubwa wamelitendea haki.

Huku kwa Diego Simeone ni kama wamezaliwa upya kwani mpaka sasa hawajapoteza mechi yoyote kati ya hizo tatu ambazo wamecheza wakikusanya pointi 7 hadi sasa baada ya kutoa sare mechi moja.

Takwimu zinaonesha kuwa mara ya mwisho kukutana timu hizi mbili, Atletico waliondoka na ushindi hivyo Bilbao wanataka kulipa kisasi wakiwa nyumbani kwao. Je wataweza?. Jisajili hapa.

Jumamosi hii pale katika dimba la City Ground kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kabisa kati ya Nottingham Forest dhidi ya Tottenham Spurs ambao wameanza msimu vibaya baada ya kupigika kwenye mechi zao mbili mpaka sasa.

Forest mpaka sasa wameonyesha dalili za kuwa timu ngumu kupambana nayo baada ya kutoa sare dhidi ya Liverpool, matokeo ambayo yaliyowaongezea morali baada ya kuonyesha uwezo wa kushambulia na kutumia vizuri nafasi zao.

Kikosi hicho kinaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza kwa kasi, hasa kinapopata nafasi ya kushambulia kupitia mipira ya kushtukiza. Pale kwa wakali wa ubashiri Meridianbet wameipa mechi hii Odds kubwa na machaguo zaidi ya 1000. Jisajili hapa.

Huku kwa upande wa Tottenham, hali ni tofauti. Spurs wameanza msimu wakiwa chini ya presha baada ya kupoteza michezo yao ya awali na kushindwa kufunga bao. Hilo limeweka jukumu kubwa kwa kocha Roberto De Zerbi kutafuta suluhisho katika safu ya ushambuliaji. Nani kuondoka na ushindi leo?. Suka jamvi hapa.

Makamu wa Rais Ashiriki Misa ya Kuwekwa Wakfu Askofu Msaidizi Dar

Global Publishers
September 5, 2026
36 views
0 Comments

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, leo Septemba 5, 2026, ameshiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Mhashamu Vincent Mpwaji kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.
Adhimisho hilo limefanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, likihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na waumini kutoka maeneo tofauti.Misa hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, ambaye alikuwa Askofu kiongozi katika uwekaji wakfu huo.Amehudumu pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya, pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu.

Sherehe hiyo ya kidini pia imewakutanisha Maaskofu kutoka majimbo mbalimbali ya Kanisa Katoliki nchini, viongozi wa madhehebu tofauti ya Kikristo, viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali.

Aidha, Mapadre, Watawa, familia, ndugu, marafiki na waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini wamehudhuria kushuhudia tukio hilo muhimu katika Kanisa Katoliki.

Kuwekwa wakfu kwa Mhashamu Vincent Mpwaji kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam ni hatua muhimu katika huduma yake ya kiroho na uongozi wa Kanisa, huku akitarajiwa kushirikiana na viongozi wengine katika kutekeleza majukumu ya kichungaji ndani ya Jimbo hilo.

KIGOMA YATANGAZA MAFANIKIO UDHIBITI WA EBOLA

 MKOA Kigoma unaelezwa kupiga hatua kubwa katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umesababisha idadi kubwa ya vifo katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kwamba kwa sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa mkoani humo.

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akizungumza katika kikao cha wadau wa afya kutathmini hatua zilizochukuliwa kudhibiti ugonjwa huo alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo hatua Zaidi za kudhibiti hali hiyo zimeendelea kutekelezwa.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma, Dk.Rashid Chuachua alisema kuwa malengo na mikakati iliyowekwa imefanya kazi na kuufanya mkoa huo kuwa salama hadi sasa ambapo ametoa wito kwa wataalam wa afya na wadau mbalimbali kuhakikisha hatua Zaidi zinachukuliwa kuhakikisha ugonjwa huo hauingii mkoani humo sambamba na kuwataka kila moja kutoa taarifa anapoona kuna mtu mwenye dalili ya mgonjwa.

 Akitoa taarifa kwa wajumbe wa kikao hicho hatua mbalimbali zilizochukuliwa na timu ya afya ya mkoa, Mratibu wa magonjwa ya mlipuko mkoa Kigoma, Albert Paschal alisema kuwa hatua muhimu za kudhibiti ugonjwa huo zimetekelezwa na kufanikisha kuufanya mkoa huo kubaki salama hadi sasa ikiwemo kutoa elimu kwa wahudumu wa afya mkoani humo.

Paschal alizitaja hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji katika mipaka yote inayoingia mkoani humo, mkoa umeanzisha maabara tembezi ya vipimo, mipaka isiyo rasmi imetambuliwa na viongozi wa vijiji wamepewa elimu na maelekezo ya kutoa taarifa za dalili ya mgonjwa na kwenye baadhi ya mipaka yenye idadi kubwa ya wasafiri kumefungwa vifaa vya kupima joto la wagonjwa sambamba na uwepo wa utayari wa magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance).

Pamoja na hatua hiyo Katibu wa CCM mkoa Kigoma,Christopher Pallangyo amepongeza hatua za udhibiti wa ugonjwa huo mkoani Kigoma akitaka pia hatua Zaidi zichuliwe kwenye vizuizi mbalimbali vya barabarani kwa kuwepo kwa watoa huduma za afya ambap pia wataratibu zoezi la kukagua watu wanaopita maeneo hayo.

MKALAMA: BARAZA LA MADIWANI LAONYA KUINGILIWA MAJUKUMU

 

‎Na Elisante John, Singida

‎Jumamosi, Septemba 5, 2026

‎Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida imesema haitakubali majukumu ya Baraza la Madiwani kuingiliwa na mtu yeyote kwa maslahi binafsi, ikisisitiza kuwa itaendelea kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, taratibu na misingi ya utawala bora.

‎Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mohamed Juma, wakati akihitimisha mkutano wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri mjini Nduguti, huku akitaka taasisi hiyo kuheshimiwa katika kutekeleza majukumu yake.

Juma amesema kuwa, Baraza la Madiwani limeanzishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi, likiongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo hakuna mtu anayepaswa kulidharau, kulichezea au kuingilia utekelezaji wa majukumu yake.

‎Amesema alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Baraza hilo kukutana kama Kamati kushughulikia tuhuma dhidi ya mmoja wa watumishi wa Halmashauri, anayedaiwa kukiuka misingi na maadili ya utumishi wa umma.

ila kutaja jina la kiongozi anayedaiwa kuingilia shughuli za Halmashauri wala mtumishi anayekabiliwa na tuhuma hizo, Juma aliiagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuandika barua kwa haraka kwenda kwa Mkuu wa Mkoa, ili kuomba ridhaa ya kuitisha kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kushughulikia tofauti zilizojitokeza kati ya pande hizo.

‎Katika hatua nyingine, Baraza hilo lilimtunuku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, hajati Asia Messos, tuzo ya pongezi kwa kutambua mchango wake katika kusimamia majukumu ya Halmashauri, kuimarisha utawala bora na kuongeza mapato, hatua iliyosaidia kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Baadhi ya madiwani, akiwamo Anthony Kahema wa Nkalakala, Linza John wa Matongo, Salumu Lindi wa Ibaga na Zainabu Kihara wa viti maalumu, waliunga mkono kutolewa kwa tuzo hiyo, wakisema hajati Messos amekuwa akionesha usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na anastahili kupewa pongezi pamoja na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

‎Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, hajati Messos alishindwa kujizuia na kutoa machozi ya furaha, akilishukuru Baraza kwa kutambua mchango wake katika kusimamia shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Hajati Messos alisema mafanikio hayo hayakuwa yake binafsi, bali ni matokeo ya ushirikiano kati yake na watumishi wenzake, akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kusimama pamoja katika kuleta maendeleo.

‎“Nimepokea tuzo na zawadi hii kwa furaha sana. Kazi hii sikuifanya peke yangu, bali pamoja na watumishi wenzangu wote 1,527 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Wote pokeeni zawadi hii na nawaomba endeleeni kuchapa kazi na tusimame imara ili kuiletea wilaya yetu maendeleo,” alisema hajati Messos.

WAZIRI KOMBO AAGANA NA MHE. MASSALA, BALOZI WA DRC NCHINI TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amekutana na kuagana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mheshimiwa Jean Pierre Massala, ambaye amehitimisha muda wake wa uwakilishi nchini Tanzania.

Mkutano huo umefanyika leo, Septemba 4, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Waziri Kombo alimpongeza Balozi Massala kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa pande mbili kati ya Tanzania na DRC, hususan katika maeneo ya maendeleo, biashara na uwekezaji.

Waziri Kombo amesema Tanzania imeazimia kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati na DRC katika sekta mbalimbali, zikiwemo uchukuzi, madini, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya pamoja yenye manufaa kwa wananchi wa nchi hizo mbili.

Miongoni mwa miradi ya kipaumbele ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), inayolenga kuunganisha Tanzania na DRC kupitia Burundi, pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ya Mawimbi ya Mwanga kutoka Kigoma nchini Tanzania hadi Kalemie, Mkoa wa Tanganyika nchini DRC, kupitia Ziwa Tanganyika.

Aidha, Tanzania na DRC zimekubaliana kuharakisha uanzishwaji wa Tume ya Pamoja ya Kiuchumi (JEC), ambayo inalenga kurahisisha utekelezaji wa miradi ya pamoja na kutengeneza fursa mpya za kiuchumi kwa nchi hizo.

Kwa upande wake, Balozi Massala ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha uwakilishi nchini na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kimkakati katika sekta mbalimbali za maendeleo kati ya Tanzania na DRC.

 

DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA HALMASHAURI YA BAHI

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumamosi, Septemba 5, 2026, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na kuweka jiwe la msingi la mradi huo, unaolenga kuboresha mazingira ya utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Kaimu Mhandisi wa Wilaya ya Bahi, Sassoche Mtenya Maduhu, amesema jengo hilo linatarajiwa kugharimu jumla ya Sh bilioni 4.868 na litajengwa kwa awamu.

Amesema hadi kufikia Agosti 30, 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ilikuwa imepokea jumla ya Sh bilioni 1 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo hilo, ambapo Sh milioni 994.546 zimetumika.

Katika fedha hizo, Sh milioni 980.247 zimetumika kumlipa mkandarasi M/s Hamble Ulpan Engineering Company Limited, huku Sh milioni 14.3 zikitumika kwa ununuzi wa vyuma vilivyoagizwa kutoka Kiwanda cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi umefikia asilimia 100, ukiwa umehusisha maandalizi ya eneo la ujenzi, uchimbaji na ujenzi wa msingi, ujenzi wa nguzo na ring beam, ujenzi wa kuta pamoja na uwekaji wa mifumo ya awali ya maji, umeme na TEHAMA.

Mradi huo pia umechangia ajira 152 kwa wananchi, wakiwemo wanawake 89 na wanaume 63, huku kukamilika kwake kukitarajiwa kuimarisha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi wa watumishi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bahi, Mhe. Kenneth Nollo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo, akisema litakapokamilika litakuwa jengo la kisasa litakaloboresha mazingira ya kazi na utoaji wa huduma katika Halmashauri hiyo.

 

Trump Atishia Kushambulia Eneo la Kimkakati la Pickaxe Mountain nchini Iran

WASHINGTON, Marekani — Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Marekani inaweza kuishambulia Pickaxe Mountain, eneo la Iran lenye ngome kubwa za kijeshi na miundombinu ya chini ya ardhi, wakati wowote hivi karibuni.

Pickaxe Mountain, lililopo karibu na kituo cha kurutubisha uranium cha Natanz ambacho tayari kimeharibiwa kwa kiasi kikubwa, lina majengo mawili ya vichuguu yaliyojengwa kwa kina chini ya ardhi na kulindwa kwa kiwango kikubwa.

Trump ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, huku akipunguza uzito wa mzozo wa kijeshi kati ya Marekani na Iran.

Amesema vita hivyo ni jambo dogo kwa Marekani, siku moja baada ya Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, kusema kuwa hataki kuuita mzozo huo vita.

“Watu wengi hawauiti vita. Mimi nauita mzozo wa kijeshi kwa sababu ni jambo dogo kwetu. Si jambo kubwa,” Trump alisema alipoulizwa kuhusu kauli ya Vance.

Trump pia alirejea operesheni za kijeshi ambazo Marekani imewahi kufanya Venezuela na Iran, akisisitiza kuwa Marekani ina uwezo mkubwa wa kijeshi.

Mwezi Julai, Marekani ilibadilisha mfumo wake rasmi wa Defense Casualty Analysis System, ambapo wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa katika kile kilichokuwa kikiorodheshwa kama vita sasa wanaainishwa chini ya kundi la “Overseas Operations”.

Wakati huo huo, serikali ya Iran imeendelea kukataa kurudi nyuma licha ya kampeni kubwa ya kijeshi inayolenga kuishinikiza.

Kutokana na hali hiyo, Trump anaonekana kutumia mkakati wa shinikizo la kiuchumi na tishio la kuongeza mashambulizi ya kijeshi.

Katika kipindi cha mzozo huo, Trump amekuwa akitangaza mara kwa mara kwamba kuna maendeleo katika mazungumzo au kusitisha vitisho vya mashambulizi ya kijeshi dakika za mwisho, hasa pale masoko ya kimataifa yanapoanza kuyumba.