Infantino Athibitisha Kugombea tena Urais wa FIFA Mwakani

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Gianni Infantino, amethibitisha kuwa atagombea tena nafasi ya urais wa FIFA katika uchaguzi utakaofanyika Machi 2027, licha ya kukabiliwa na upinzani na shinikizo kutoka baadhi ya vyama vya soka duniani.

 

FIFA imethibitisha leo, Septemba 7, 2026, kwamba Infantino bado ana mpango wa kugombea muhula mwingine.

 

FIFA imesema kuwa hakuna kilichobadilika tangu Infantino alipotangaza mwezi Aprili kwamba angewania tena nafasi hiyo.

 

Infantino, mwenye umri wa miaka 56, amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 2016 na amewahi kuchaguliwa tena mwaka 2019 na 2023. Akishinda uchaguzi wa mwaka 2027, ataendelea kuiongoza FIFA hadi mwaka 2031 uamuzi wake wa kugombea tena unakuja wakati FIFA ikikabiliwa na mgawanyiko kuhusu uongozi wake.

 

Infantino amekosolewa baada ya mpango wa kuhusisha wawekezaji binafsi katika mashindano ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia, kukataliwa na hatimaye kuachwa mpango huo uliibua upinzani kutoka kwa baadhi ya mashirikisho makubwa ya soka.

 

Miongoni mwa mashirikisho yaliyomkosoa Infantino ni UEFA, AFC na CONCACAF. Hata hivyo, bado anaungwa mkono na baadhi ya vyama vya soka, hususan barani Afrika kupitia CAF na Amerika Kusini kupitia CONMEBOL.

 

Kwa sasa, Infantino ndiye mgombea pekee aliyethibitishwa rasmi kwa uchaguzi huo, ingawa Victor Montagliani, rais wa CONCACAF, ametajwa kama mmoja wa viongozi wanaoweza kumpinga.

Wagombea wengine wana hadi Novemba 18, 2026 kuwasilisha nia zao,uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 2027 mjini Rabat, Morocco, katika kongamano la FIFA.

 

Matokeo yake yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa uongozi wa soka duniani kutokana na mgawanyiko uliopo ndani ya shirikisho hilo.

 

Kwa sasa, Infantino anaendelea na majukumu yake kama rais wa FIFA huku akitarajiwa kukabiliana na changamoto kubwa zaidi za kisiasa katika safari yake ya kutafuta muhula mwingine wa uongozi.

Na Ashura karimu



TRC Yatangaza Nafasi 24 za Ajira, Waombaji Wapewa Hadi Septemba 10

Dodoma, Agosti 28, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Tanzania Railways Corporation (TRC), imetangaza nafasi 24 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, uwezo na uzoefu unaohitajika.

Nafasi hizo zimetangazwa kupitia tangazo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/53 la tarehe 28 Agosti 2026.

Nafasi zilizotangazwa

  1. Instructor II (Civil Engineer) — Nafasi 1
  2. Instructor II (Mechanical Engineer) — Nafasi 1
  3. Artisan II (Auto Electric) — Nafasi 5
  4. Technician II (Automobile) — Nafasi 4
  5. Technician II (Hydraulic Machineries) — Nafasi 2
  6. Engineer II (Signal & Telecommunication) — Nafasi 1
  7. Locomotive Driver II — Nafasi 10

Sifa za jumla kwa baadhi ya nafasi

Instructor II (Civil Engineer):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) au taaluma inayolingana nayo, yenye kiwango cha NTA Level 8 au sawa, kutoka taasisi inayotambuliwa. Anatakiwa kuwa na GPA isiyopungua 3.5, pamoja na kuwa anastahili kusajiliwa kama mwalimu wa ufundi na kusajiliwa na bodi husika kama Graduate Engineer/Professional.

Instructor II (Mechanical Engineer):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Mechanical Engineering au inayolingana nayo, yenye kiwango cha NTA Level 8 au sawa, kutoka taasisi inayotambuliwa, akiwa na GPA isiyopungua 3.5. Pia anatakiwa kuwa anastahili kusajiliwa kama mwalimu wa ufundi na kusajiliwa na bodi husika kama Graduate Engineer/Professional.

Artisan II (Auto Electric):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne pamoja na CBET Level II/III, Trade Test Grade I/II au NVA II/III katika fani ya Auto Electric au sifa inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Technician II (Automobile):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Diploma/NTA Level 6 katika Automobile Engineering, Automotive Mechanics au sifa nyingine inayohusiana na fani hiyo.

Technician II (Hydraulic Machineries):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Full Technician Certificate (FTC) au Ordinary Diploma in Mechanical Engineering yenye utaalamu wa Hydraulic Machineries au sifa inayolingana nayo.

Engineer II (Signal & Telecommunication):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Electrical Engineering, Telecommunication Engineering, Electronics Engineering au inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa na awe amesajiliwa na Engineers Registration Board (ERB) kama Graduate Engineer.

Locomotive Driver II:
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne, Cheti cha Uendeshaji Treni (Locomotive Driving Certificate) cha miaka miwili au Locomotive Shunting Certificate kutoka TIRTEC au taasisi inayotambuliwa, pamoja na leseni ya udereva ya Class F au G.

Masharti muhimu ya maombi

PSRS imesema waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania na kwa ujumla wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vyao vya elimu na taaluma, pamoja na transcripts na vyeti vya usajili wa kitaaluma kutoka bodi au mamlaka husika pale inapohitajika.

Aidha, mwombaji anatakiwa kupakia picha ya Passport Size ya hivi karibuni katika mfumo wa maombi.

PSRS imesisitiza kuwa result slips za Form IV na Form VI, testimonials pamoja na partial transcripts hazitakubalika kama nyaraka za maombi.

Waombaji wanapaswa pia kutaja referees watatu wanaotambulika na kutoa mawasiliano yao yanayoaminika.

Kwa waombaji wenye vyeti vya elimu vya nje ya Tanzania, vyeti hivyo vinapaswa kutambuliwa na mamlaka husika, ikiwemo TCU, NECTA au NACTVET, kulingana na aina ya sifa.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yanatakiwa kuwasilishwa mtandaoni kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Waombaji wanaweza kutumia:

portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, kusainiwa na kuelekezwa kwa:

Secretary,
President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 10, 2026.

PSRS imesema maombi yatakayowasilishwa kupitia njia nyingine tofauti na Recruitment Portal hayatazingatiwa.

Aidha, ni waombaji watakaoteuliwa pekee ndio watakaotaarifiwa kuhusu tarehe ya usaili.

Sekretarieti imeonya kuwa mtu atakayewasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

Kizimkazi: Viongozi Wamfariji Rais Samia Baada ya Msiba wa Mumewe

Kizimkazi, Zanzibar — Septemba 7, 2026: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi, wametembelea nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, kumpa pole kufuatia msiba wa mume wake, Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Viongozi hao wamefika nyumbani kwa Rais Samia kufuatia kifo cha Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Mzena, Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika msiba huo, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wameungana na Rais Samia na familia yake kutoa pole na faraja katika kipindi hiki cha majonzi.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alikuwa mume wa Rais Samia Suluhu Hassan na amefariki dunia baada ya kuugua na kupata matibabu katika Hospitali ya Mzena, Zanzibar.

Msiba huo umewakutanisha viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti, waliokwenda Kizimkazi kutoa pole na kushiriki katika kipindi cha maombolezo.

Mazishi ya Maalim Hafidh Ameir Hassan yamefanyika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini, viongozi wa Mahakama na Bunge, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi.

Vita ya LaLiga! Getafe na Celta Vigo Kwenye Uwanja wa Coliseum

Mchezo wa Getafe dhidi ya Celta Vigo utachezwa leo Jumatatu, Septemba 7, 2026 katika dimba la Coliseum, ukiwa ni mchezo wa nne wa LaLiga msimu wa 2026/27., mchezo unatarajiwa kuanza saa 20:00 usiku.

Getafe wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na pointi tatu baada ya kushinda mchezo mmoja na kupoteza miwili katika mechi tatu za mwanzo. Wamefunga bao moja pekee na kufungwa manne.

Jambo linaloonyesha changamoto yao kubwa kwa sasa ipo katika uzalishaji wa mabao. Hata hivyo, kucheza nyumbani kunaweza kuwapa nguvu zaidi, hasa kwa mtindo wa kocha Pepe Bordalás unaosisitiza nidhamu na uimara wa timu.

Kwa upande wa Celta Vigo, hali yao ni ngumu zaidi kwa kuwa wana pointi moja tu baada ya michezo mitatu, wakiwa wamepoteza miwili na kutoka sare moja. Wamefunga bao moja na kuruhusu manne, hivyo nao wamekuwa na tatizo la kupata matokeo mazuri pamoja na ufanisi mbele ya lango. Hata hivyo, Celta wana uwezo wa kutawala mpira zaidi, jambo linaloweza kuwapa nafasi ya kuilazimisha Getafe kucheza kwa kujilinda.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kihistoria, huu ni mchezo ambao umekuwa na ushindani mkubwa. Katika michezo 30 iliyopita, Getafe wana ushindi 11 dhidi ya tisa wa Celta Vigo, huku michezo mingine ikiisha sare. Mkutano wao wa mwisho Februari 2026 uliishia 0-0, ishara kwamba timu hizi zinaweza kuwa na mchezo wa tahadhari na wenye nafasi chache za wazi.

Kwa mtazamo wa kiufundi, Getafe wanaweza kutegemea faida ya uwanja wa nyumbani na kucheza kwa mipira ya haraka pamoja na kutumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Celta. Celta, kwa upande mwingine, wanahitaji kuongeza ubunifu katika eneo la mwisho na kuwa makini wanapopoteza mpira.

Na kwa wasomaji na mashabiki wote wa soka na ubashiri, kesho ni siku nyingine kubwa kwa soka la Ulaya! UEFA Champions League ya msimu wa 2026/27 inaanza rasmi kesho, Jumanne, Septemba 8, huku michezo kadhaa mikubwa ikitarajiwa kuwakutanisha baadhi ya vigogo wa soka barani Ulaya. Miongoni mwa michezo ya kuvutia ni Real Madrid dhidi ya Inter Milan, Porto dhidi ya Manchester City, Borussia Dortmund dhidi ya Villarreal na Club Brugge dhidi ya Aston Villa. Endelea kufuatilia Meridianbet kwa matokeo ya UEFA Champions League.

Makamu wa Rais Ndejembi Aungana na Waombolezaji Maziko ya Hafidh Ameir Hassan (Video +Picha)

Global Publishers
September 7, 2026
498 views
0 Comments


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameshiriki maziko ya Marehemu Hafidh Ameir Hassan, mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maziko hayo yamefanyika leo, Jumatatu, Septemba 7, 2026, katika eneo la Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maziko hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi Wakuu na Viongozi Wakuu Wastaafu, viongozi wa Serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Mahakama na Bunge, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na familia, ndugu, marafiki na waombolezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Matajiri wa Jiji Azam Fc na Namungo Kukipiga Leo Ligi Kuu ya NBC

Global Publishers
September 7, 2026
66 views
0 Comments

Klabu ya Azam FC leo Jumatatu, Septemba 7, 2026, inashuka dimbani kumenyana na Namungo FC katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi.

Kwenye msimamo kuelekea mtanange wa leo, timu hizi zinapishana kwa pointi na nafasi, kulingana na mwanzo wao wa msimu wa 2026/2027.

Azam FC,imecheza mechi tano,  inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 11.

Azam FC inalenga kupata ushindi leo ili kuisogelea Yanga SC na Simba SC zilizopo kileleni mwa msimamo, kila moja ikiwa na pointi 15.

Namungo FC kwa upande wao, imecheza mechi tano, lakini inasuasua kwenye msimamo ikiwa na pointi tatu pekee.

Na Peter Jinanai



Dkt. Mwinyi Atoa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Kifo cha Mumewe, Kuzikwa Leo Kizimkazi, Zanzibar

Global Publishers
September 7, 2026
852 views
0 Comments

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia leo, Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.

Katika salamu hizo, Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo na kuungana na Rais Dkt. Samia, familia, ndugu, jamaa pamoja na wote waliofikwa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi.

Amesema kifo hicho ni pigo kubwa kwa familia na wote waliokuwa karibu na marehemu, huku akimuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Rais Dkt. Samia pamoja na familia yake subira, nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan anatarajiwa kuzikwa leo Kizimkazi, Zanzibar, katika mazishi yatakayohudhuriwa na familia, ndugu, jamaa, viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu aisamehe roho ya Marehemu Hafidh Ameir Hassan na amjaalie makazi mema Peponi.

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.

Infantino Athibitisha Kugombea tena Urais wa FIFA Mwakani

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Gianni Infantino, amethibitisha kuwa atagombea tena nafasi ya urais wa FIFA katika uchaguzi utakaofanyika Machi 2027, licha ya kukabiliwa na upinzani na shinikizo kutoka baadhi ya vyama vya soka duniani.

 

FIFA imethibitisha leo, Septemba 7, 2026, kwamba Infantino bado ana mpango wa kugombea muhula mwingine.

 

FIFA imesema kuwa hakuna kilichobadilika tangu Infantino alipotangaza mwezi Aprili kwamba angewania tena nafasi hiyo.

 

Infantino, mwenye umri wa miaka 56, amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 2016 na amewahi kuchaguliwa tena mwaka 2019 na 2023. Akishinda uchaguzi wa mwaka 2027, ataendelea kuiongoza FIFA hadi mwaka 2031 uamuzi wake wa kugombea tena unakuja wakati FIFA ikikabiliwa na mgawanyiko kuhusu uongozi wake.

 

Infantino amekosolewa baada ya mpango wa kuhusisha wawekezaji binafsi katika mashindano ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia, kukataliwa na hatimaye kuachwa mpango huo uliibua upinzani kutoka kwa baadhi ya mashirikisho makubwa ya soka.

 

Miongoni mwa mashirikisho yaliyomkosoa Infantino ni UEFA, AFC na CONCACAF. Hata hivyo, bado anaungwa mkono na baadhi ya vyama vya soka, hususan barani Afrika kupitia CAF na Amerika Kusini kupitia CONMEBOL.

 

Kwa sasa, Infantino ndiye mgombea pekee aliyethibitishwa rasmi kwa uchaguzi huo, ingawa Victor Montagliani, rais wa CONCACAF, ametajwa kama mmoja wa viongozi wanaoweza kumpinga.

Wagombea wengine wana hadi Novemba 18, 2026 kuwasilisha nia zao,uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 2027 mjini Rabat, Morocco, katika kongamano la FIFA.

 

Matokeo yake yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa uongozi wa soka duniani kutokana na mgawanyiko uliopo ndani ya shirikisho hilo.

 

Kwa sasa, Infantino anaendelea na majukumu yake kama rais wa FIFA huku akitarajiwa kukabiliana na changamoto kubwa zaidi za kisiasa katika safari yake ya kutafuta muhula mwingine wa uongozi.

Na Ashura karimu



Jaji Warioba Aanguka Wakati Akihutubia Mkutano

Global Publishers
September 7, 2026
0 views
0 Comments

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameanguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini Tanzania, ambapo alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu.

Tukio hilo limetokea wakati wa mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), na kusababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda.

Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu, ametangaza mapumziko mafupi ili kuruhusu hali kutulia na hatua zinazohitajika kuchukuliwa.

Hadi sasa, taarifa zaidi kuhusu hali ya kiafya ya Jaji Warioba baada ya kuanguka kwake hazijawekwa wazi.

Mkutano huo ulikuwa ukijadili hali ya kisiasa nchini pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa demokrasia na siasa nchini Tanzania.

Zungusha, Kusanya, Shinda Na Pragmatic Play Drops & Wins 2026

Meridianbet imefungua ukurasa mpya wa burudani kwa wapenzi wa kasino kupitia Pragmatic Play Drops & Wins 2026, promosheni inayokupa zawadi na vizidishi vikubwa kwa mtindo unaoongeza msisimko kila unapocheza. Kama unapenda michezo ya kasino yenye nafasi ya kupata zawadi huku ukiendelea kuburudika, basi huu ni wakati wa kuingia kwenye michezo inayoshiriki na kuanza safari ya kukusanya. Kila mzunguko unakupeleka hatua moja karibu na zawadi inayokusubiri.

Sheria za mchezo huu ni rahisi na hazihitaji mambo mengi. Unachotakiwa kufanya ni kuweka dau kwenye michezo inayoshiriki, kisha kila raundi inayochezwa kwa fedha halisi itahesabiwa. Kadiri unavyoendelea kucheza, ndivyo unavyopata nafasi ya kukusanya vipande vya gurudumu. Ukifanikiwa kupata vipande vitatu vya gurudumu, unafungua mlango wa kupata zawadi, huku msisimko ukiendelea kuongezeka kila raundi inapozunguka.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kinachofanya promosheni hii kuwa ya kuvutia zaidi ni ukubwa wa zawadi zinazoweza kupatikana. Wachezaji wanaweza kukutana na vizidishi hadi x100,000 ya dau, huku mizunguko ya bure ikiwa pia miongoni mwa zawadi zinazoweza kupatikana. Hii ndiyo aina ya burudani inayofanya kila mzunguko kuwa na mvuto wake, kwa sababu huwezi kujua ni wakati gani mkusanyiko wako utakamilika na zawadi ikaingia.

Zaidi ya hapo, zawadi zinapatikana papo hapo kwenye michezo inayostahiki, na kila mchezaji anaweza kupata hadi zawadi mbili. Hivyo, ukianza safari yako leo, si lazima uridhike na zawadi moja pekee. Endelea kukusanya vipande, fuatilia maendeleo yako na uone kama bahati itakupa nafasi ya kufungua zawadi nyingine ndani ya promosheni hii inayosisimua.

Kwa hiyo, kama uko tayari kwa msisimko wa kila raundi na zawadi kubwa, Pragmatic Play Drops & Wins 2026 inakusubiri Meridianbet. Ingia kwenye michezo inayoshiriki, weka dau kwa fedha halisi, zungusha na anza kukusanya.