Global Publishers
September 10, 2026
0 views
0 Comments

Viongozi, wanasiasa, mabalozi pamoja na wageni mbalimbali wameendelea kumtembelea na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa Mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Miongoni mwa waliofika kutoa pole ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, ambaye amemtembelea Rais Samia nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 10, 2026.
Aidha, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, pamoja na ujumbe wake, wamefika Kizimkazi kumfariji Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo.
Makatibu Wakuu pamoja na Naibu Makatibu Wakuu nao wamewasili nyumbani kwa Rais Samia kutoa pole na kushiriki katika kipindi hiki cha majonzi.
Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.
Ziara hizo za viongozi na wageni mbalimbali zimeendelea kuwa sehemu ya utaratibu wa kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha msiba.
