NA MATUKIO DAIMA MEDIA
NJOMBE.Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 15.9 za mradi wa taasisi ya Bodi ya maji ya Bonde la Rufiji Iringa ,Fedha ambazo zilitengwa kwaajili Utekelezaji wa violezi 54 ili kuweka mipaka katika chanzo cha mto Mbukwa kilichopo wilaya ya Wanging’ombe .
Hayo yamesemwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe Noely Mseo wakati Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika kipindi cha miezi sita kuanzia Aprili hadi Septemba 2026.
Aidha,Mseo amewataka wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa, hatua inayolenga kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na kulinda rasilimali za umma.
Thadei Mbilinyi ni Mmoja wa Wananchi Mkoani Njombe amesema jamii inapaswa kuendelea kupambana na Rushwa katika maeneo yao.
Hata hivyo,kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu;Tutimize Wajibu wetu.



