DC NJOMBE:MRADI WA BBT NJOMBE TC USIWE CHANZO CHA MIGOGORO KWA VIJANA

 ‎

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

NJOMBE.Wakati Mradi wa Jenga Kesho iliyobora BBT Ukizinduliwa Nchini Kote ili kuwakwamua vijana na wimbi la umasikini,Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Juma Sweda, amewataka wataalamu wa kilimo Kuhakikisha wanawasimamia vijana hao ili mradi ulete tija katika maisha yao na taifa.

‎‎Katika Halmashauri ya mji wa Njombe mradi huo utatekelezwa katika kijiji cha Lwangu kata ya Kifanya ambako zaidi ya ekari 300 zimetengwa kwa ajili ya vijana 82 wa awamu ya kwanza ambao watazalisha mbegu za viazi mviringo huku mkuu huyo wa wilaya akisisitiza tija katika mradi huo.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Sera,Utafiti na Ubunifu Wizara ya Kilimo Adela Ng’atigwa amesema kwa kuwa  kilimo ndiyo mkombozi na kitakwenda sambamba na dira ya taifa ya 2050 cha  kuhakikisha vijana wanachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia uzalishaji hivyo mradi huo uwe chachu katika ukuaji wa uchumi kwa vijana.

‎‎Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Erasto Mpete kupitia mradi huo amesema Njombe iwe mfano katika utekeleaji mzuri wa miradi ya serikali kwa wataalamu kuwajibika na kuleta matokeo chanya.

‎‎Hata hivyo Ofisa Kilimo Halmashauri ya Mji wa Njombe Nolasco Kilumile amesema  kabla ya kuamua aina ya mbegu zotakazozalishwa wataanza kuwashirikisha vijana hao na kufanya utafiti utakaosaidia kupata masoko ya uhakika na watakuwa sambamba katika uendelevu wa mradi.

‎Kwa upande wao Baadhi ya vijana wanaotarajia kunufaika na  mradi wa BBT akiwemo Desderia Mtweve wameishukuru Serikali kwa kuzindua mradi huo kwani vijana wengi wamekosa ajira na wamesalia mitaani pasina shughuli maalumu za kujiingizia kipato.

‎‎Mradi wa BBT utatekelezwa nchini kote kwa kuwawezesha vijana kujikita na shughuli za kilimo badala ya kushinda mitaani na kujiunga na makundi ya kihalifu.