Watu 32 Wafariki, 37 Wajeruhiwa Moro, Hospitali ya Rufaa Morogoro Yathibitisha – Video

Global Publishers
October 9, 2026
810 views
0 Comments


Watu 32 wamefariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali mbili za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2026 katika maeneo ya Mkambarani na Mvomero, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, vifo 28 vimetokana na ajali ya basi lililogongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Mkambarani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kati ya miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo, miili 11 bado haijatambuliwa jinsia.

Katika ajali nyingine iliyotokea eneo la Mvomero, watu wanne wamefariki dunia baada ya gari la Polisi kuhusika katika ajali na lori.

Kwa ujumla, ajali hizo mbili zimesababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37, kwa mujibu wa taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Tukio hilo linaongeza uzito wa changamoto ya usalama barabarani na kuibua majonzi kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao.

Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu hali za majeruhi, utambulisho wa waliofariki na chanzo cha ajali hizo hazijaainishwa katika taarifa iliyotolewa.