NCAA YAJULIKANA ZAIDI DUNIANI – Matukio Daima Habari

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema kazi kubwa inayofanywa na Tanzania Safari Channel (TSC) katika kutangaza vivutio vya utalii nje ya mipaka ya Tanzania imechangia kuwavutia wageni wanaoshiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kutembelea vivutio mbalimbali nchini.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa kupitia maudhui yanayowasilishwa na TSC kuhusu uzuri na utajiri wa vivutio vya Tanzania, wageni wameendelea kupata hamasa ya kuvitembelea na kujionea wenyewe.

Akizungumza katika ziara ya makatibu wa Mabunge Duniani IPU ambao wametembelea hifadhi ya Ngorongoro, Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Badru amesema wanahakika kuwa umaarufu wa NCAA duniani unaweza ukawa umetokana na chanel hiyo kutokana na program zinazorushwa ambazo zinaonyesha umahususi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Aidha amesema NCAA imewachagulia viongozi hao kutembelea hifadhi hiyo hususani eneo la kreta ambalo haliwezi kupatikana sehemu nyingine yeyote duniani kutokana na wanyama wanaopatikana humo pamoja na manthari yake.

Sambamba na hayo ineelezwa kuwa wingi wa wageni wanafika nchini na kutembelea vivutio vya utalii kutaongeza tija ya kuongeza Utalii na kuvuta wawekezaji zaidi katika sekta ya Utalii.

Mkutano wa 153 wa IPU licha ya kujadili masuala ya kibunge umeweka alama katika sekta ya Utalii.