Global Publishers
October 6, 2026
0 views
0 Comments
MARA: Jeshi la Polisi linamshikilia Wakili Keneth Nkiko, mkazi wa Mwigobero mwenye umri wa miaka 28, kwa tuhuma za kumuua Magreth Richard (22).
Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo linadaiwa kutokea Oktoba 5, 2026, ambapo Nkiko anatuhumiwa kumpiga Magreth kichwani kwa kitu butu na baadaye kumchoma kwa kitu chenye ncha kali katika maeneo mbalimbali ya mwili.
Uchunguzi wa awali unaelezwa kubaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu Magreth kuwa na mahusiano na wanaume wengine.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo, huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
