Baraza la uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani, limemchagua Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa umoja huo.
Hoja ya kumchagua Mhe. Zungu kuwa Rais wa Mkutano huo imetolewa na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Uingereza (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle, na kuungwa mkono na baadhi ya nchi ikiwemo Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Uamuzi huo umefikiwa leo Oktoba 6, 2026, ikiwa ni siku ya pili ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaoendelea jijini Arusha katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).



