Global Publishers
October 5, 2026
18 views
0 Comments

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limeanza kuchunguza tukio la askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani anayesambaa kwenye mitandao ya kijamii akionekana kumshambulia dereva wa gari kubwa aina ya lori.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Oktoba 5, 2026, uchunguzi huo unaendelea sambamba na utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo kwa kuzingatia misingi ya kisheria na kuwachukulia hatua wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vilivyo kwenye Mnyororo wa Haki Jinai.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limetoa wito kwa wananchi wote kuzingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya kihalifu, likisisitiza kuwa halitakuwa na muhali kwa yeyote atakayebainika kutenda matukio ya uhalifu.

