Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Oktoba 4, 2026, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Kasisi na Canon Charles Mika Lundu kuwa Askofu wa Dayosisi ya Handeni.
Katika ibada hiyo, pia inafanyika hafla ya uzinduzi rasmi wa Dayosisi ya Handeni, iliyotenganishwa na Dayosisi ya Tanga.
Ibada hiyo inafanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Kristu Mfalme, Chanika, Handeni, mkoani Tanga.



