Global Publishers
October 1, 2026
0 views
0 Comments

DODOMA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 1, 2026, ameapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, walioapishwa ni Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera kuwa Waziri wa Nishati na Masanja Kung’u Kadogosa kuwa Waziri wa Ujenzi.
Aidha, Rais Samia amemuapisha Asha Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, akishughulikia masuala ya usimamizi wa fedha.
Baada ya kuwaapisha viongozi hao, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.
Hafla hiyo imefanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, huku viongozi hao wakianza rasmi majukumu yao katika nafasi walizoteuliwa na Rais.

