MZEE MPILI WA YANGA AFARIKI DUNIA,YANGA YAMLILIA

UONGOZI wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) umetangaza kwa masikitiko kifo cha mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, maarufu kama Mzee Mpili, kilichotokea usiku wa Septemba 27, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, marehemu Mpili alifariki dunia katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Uongozi umeeleza kuwa maziko yanatarajiwa kufanyika leo, Septemba 28, 2026, majira ya saa 10:00 jioni.

Shughuli za maziko zitafanyika katika Makaburi ya Msikiti Mkubwa yaliyopo Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa mpira, na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina,” imeeleza taarifa hiyo.