Same Kilimanjaro
Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Mhe. David Mathayo, amempokea Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, aliyewasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Same kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi katika wilaya hiyo.
Ndugu Mwanri amewasili Same jana ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi, ambapo a alitembelea Majimbo ya Same Mashariki na Same Magharibi kwa ajili ya kukutana na viongozi, wanachama wa CCM pamoja na wananchi katika maeneo mbalimbali.
Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu huyo alisikiliza na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Chama Cha Mapinduzi, pamoja na changamoto na maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Same.
Ziara hiyo hili hitimishwa kwa mkutano wa hadhara, ambapo Ndugu Mwanri atazungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM kuhusu masuala mbalimbali ya chama na maendeleo ya jamii.

