DAR ES SALAAM, Septemba 24, 2026 — Staa wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel, ameendelea kuonyesha namna anavyomthamini mume wake, mwanamuziki Salmin Ismail Hoza, maarufu kama Kusah, baada ya kumuandikia ujumbe wa kimahaba kupitia mitandao ya kijamii.
Katika ujumbe huo aliouweka leo, Septemba 24, 2026, Aunty Ezekiel ameashiria mshikamano wao kama wanandoa, akisema hakuna kitu kinachoweza kuwatenganisha.

Akiambatanisha ujumbe huo na picha yao, mwigizaji huyo aliandika:
“Unstoppable together…..👑❤️”
Ujumbe huo umeibua maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki ambao wameonekana kufurahishwa na namna wawili hao wanavyoendelea kuonyesha mapenzi yao hadharani.
Baadhi ya mashabiki waliwasifia kwa kuonekana kuendana, huku wengine wakitumia maneno ya utani kuzungumzia namna wanavyoweka wazi mapenzi yao kwenye mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa maoni yaliyotolewa na mashabiki ni pamoja na “One & Only ”, “Sema wanaendana ” na “Mshangazi ni mmoja tuu hapa mjini .”
Shabiki mwingine aliandika kwa utani: “Mnatupa foili za chips barabarani punguzeni pilipili mtaniuwa ,” akimaanisha namna wanavyowapa mashabiki hisia kupitia picha na ujumbe wao wa kimapenzi.
Wengine walitania kwamba wanandoa hao wanapaswa kuendelea na mambo yao ya kimapenzi bila kuwapa mashabiki presha, huku mmoja akiandika, “MNGEPOST ATA USIKU JAMENI MNATAKA SINGO TUJISIKIEJE 😢.”
Kwa ujumla, ujumbe huo wa Aunty Ezekiel umeendelea kuibua hisia za mashabiki kuhusu uhusiano wake na Kusah, huku wengi wakionekana kufurahia kuona wawili hao wakionyesha upendo na mshikamano wao.

